Mgawanyo wa tiba ya kifua kikuu

Post hii inahusu zaidi mgawanyiko wa tiba ya kifua kikuu, kwa kawaida tiba hii imegawanyika katika sehemu kuu mbili.

Mgawanyo wa tiba ya kifua kikuu.

1.Tiba ya kifua kikuu imegawanyika katika makundi mawili na kila kundi huwa na dawa zake kutofautiana na kundi jingine, makundi menyewe ni kama ifuatavyo.

 

2. Kundi la kwanza ambalo kwa kitaalamu huitwa initial phase, kundi hili lina madawa ya rifampin, isoniazid,pyrazinamide na ethambutol dawa hizi utumika kwa miezi miwili kwa mgonjwa anayeanza matibabu yaani mgonjwa mpya.

 

 

3. Na pia mgonjwa uongezewa dawa nyingine mpya ya streptomycin, na zile za mwanzo nazo utumika ambazo ni isoniazid, rifampin, ethambutol na pyrazinamide dawa hizi utumika kwa miezi miwili tena kwa mgonjwa mpya.

 

 

 

4. Pia mgonjwa uongezewa mwezi mwingine mmoja kwa dawa zile za mwanzo ambazo ni isoniazid, rifampin, pyrazinamide and ethambutol kwa hiyo kwa ujumla mgonjwa mpya utumia miezi mitano katika matibabu.

 

 

5. Kipindi cha pili utumia miezi tisa ikiwa mgonjwa alipotumia dawa kwenye kipindi cha kwanza akaona na baada ya siku chache ugonjwa ukajiridia tena na matibabu uanza upya kama ifuatavyo.

 

 

6. Kwenye miezi minne ya mwanzo mgonjwa utumia dawa zifuatazo rifampin na isoniazid kwa kipindi cha miezi minne na pia mgonjwa uongezewa dawa nyingine moja ambayo ni ethambutol kwa kipindi cha miezi mitano yaani miezi minne ya kwanza mgonjwa utumia rifampin, isoniazid, na katika kipindi cha miezi mitano ya mwisho mgonjwa utumia rifampin, isoniazid na ethambutol kwa miezi mitano kwa hiyo kipindi cha mwisho utumia miezi mitano katika matibabu.

 

 

 

7. Katika siku za mwanzoni mgonjwa anapogunduliwa kubwa na kifua kikuu anaweza kuambukiza watu wengine ila baada ya kuanza dawa kwa kipindi cha wiki mbili mgonjwa hawezi kuambukiza wengine kwa hiyo ni vizuri zaidi na kuchukua tahadhari kwa sababu ugonjwa huu utibiwa kwa mda mrefu ingawa watu wanapona lakini tahadhari ni ya muhimu.

 

 

 

8. Kwa hiyo tunapaswa kutoa elimu kwa watu kuhusu ugonjwa huu kwamba unapina na pia kuachana na mila na desturi za kuwatenga watu wenye ugonjwa huu na pia kuwaficha watu wenye ugonjwa huu kwa sababu ya mila na desturi kwa sababu kadri watu wanabyofichwa kwenye majumba na kuhudumiwa wakiwa wamefichwa usababisha kuongezeka kwa ugonjwa huu kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine na kudai kwamba familia fulani kuna kifua kikuu , kwa hiyo jamii inapaswa kuelezwa kwamba ugonjwa huu unatibika na watu wanapona.

 

 

 

 

9. Pia tunapaswa kuacha imani kwamba kila mtu mwenye kifua kikuu ana maambukizi ya Virusi vya Ukimwi siyo kweli kwa sababu tumeona jinsi kifua kikuu kinavyoonezaa kwa hiyo watu watoe hofu kwamba sio kila mwenye kifua kikuu ni mwathirika wa maambukizi ya Virusi vya, ila kupima maambukizi ni vizuri ili kujua afya zetu.

 

 

 

 

10. Pia na dawa tulizoziona za kutibu kifua kikuu ni lazima kuzipata hospitali sio mitaani au madukani kwa sababu kuna maelekezo ya kufuata katiks matumi na tutaweza kuchambua dawa moja na nyingine hapo mbeleni.Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/12/16/Friday - 12:02:02 am     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 522


Download our Apps
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-