Utaijuwa Dawa ya maumivu ya jino, sababu za maumivu ya jino na njia za kujikinga na maumivu ya jino
Dawa ywa maumivu ya jino.
Maumivu ya jino ma kwa jina lingine hufahamka kama odontalgia, ni maumivu makali yanayoweza kutokea kwenye ufinzi, mdomo na mifupa inayolishika jino. Maumivu haya yanaweza kuwa makali sana kiasi cha mtu kuomba msada. Wakati mwingine maumivu haya hutokea baada ya kula vitu ama kufanya jambo lakini hii sio lazima. Huwenda pia yakatokea bila hata ya sababu yeyote ile.
Je na wewe ni miongoni mwa wanaosumbuliwa na maumivu ya meno. Makala hii ni kwa ajili yako. Utajifunza sababu za maumivu ya jino, yanatokeaje, utakabiliana vipi na dawa gani utumie. Kama ukipenda makala hii usiwache kututupia maoni hapo chini:-
Sababu za kutokea maumivu ya jino:
1.Kuwa na majeraha kwenye jino ama kuzungukia jino. Majeraha ni kawaida sana kusababisha kubenduka na kukatika kwa meno.
2.Maambukizi na mashambulizi ya jino yaliyosababishwa na wadudu.
3.Kusaga ma kugonga meno hasa wakati wa usiku unapolala
4.Kuwa na magonjwa kwenye ufinzi
Dalili za maumivu ya jino
1.Maumivu wakati unapotafuna
2.Kuhisi mabadiliko endapo hali ya hewe itabadilika
3.Kuvimba kwa shavu ama kidevu
4.Mafinzi kutoa damu ama kutoma majimaji
5.Maumivu ya kichwa
6.Homa
7.Maumivu ya sikio
8.Kupotea kwa ladha ya chakula
9.Maumivu ya shingo
Dawa ya maumivu ya jino
Kuna matibabu kadha anaweza kupatiwa mgonjwa kama kung’oa jino, kuuwa bakteria kama ndio sababu. Pia kutumia dawa za kupunguza maumivu. Miongoni mwa dawa za maumivu ya meno ni:-
1.Ibuprofen
2.Naproxen
3.Acetaminophen
NITAJILINDA VIPI MA MAGONJWA YA MENO?
1.Punguza kula vitu vyenye sukari nying kwa wingi kama pipi
2.Safisha kinywa kwa mswaki kara kwa mara
3.Usilale na mabaki ya chakula mdomoni.
Dawa za mitishamba za kutibu meno
1.Kutumia muarobaini, unatafuna vijani vichanga na kuelekeza kwenye jino linalouma
2.Tafuna karafuu kuelekea kwenye jino linalouma
3.Tafuna kitunguu thaumu kuelekea jino linalouma
4.Bandua gome la muembe kish alichune gamba la juu, kisha chemsha hilo gamba kisha kunywa.
Umeionaje Makala hii.. ?
Aspirini Ni dawa ya kutuliza maumivu.Majina yanayoaminika zaidi katika kutuliza maumivu sasa yanapatikana kwa njia mbadala inayookoa gharama kwa kutumia Aspirini. Aspirini inayopendwa na familia kwa miongo kadhaa, mara nyingi hutumiwa kupunguza maumivu y
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi dawa ya Parental Artusnate ni dawa inayotumika kutibu ugonjwa wa malaria sugu kama tutakavyoona hapo baadaye.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi dawa ya Rifampin kama dawa mojawapo ya kutibu kifua kikuu.
Soma Zaidi...Albenza (albendazole) hutumika kutibu magonjwa ya minyoo ya ndani ikiwa ni pamoja na maambukizi ya minyoo ya tegu. Albenza inafanya kazi kukomesha kuenea kwa maambukizo ya minyoo kwenye chanzo, na kukata chanzo chao cha nishati, na hivyo kuzuia kuenea k
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi dawa za kisukari, kwa sababu ya kuwepo kwa ugonjwa wa kisukari vilevile kuna dawa zake ambazo utumika kurekebisha sukari kama imepanda au kushuka.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi dawa ya macrolide ni mojawapo ya dawa ya kutibu au kupambana na bakteria na upambana na bakteria wafuatao streptococcus pyogenes, staphylococcus aureus na haihusiki na haemophilia influenza ambao usababisha maambukizi kwenye mfumo w
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi dawa ya Mebendazole kama Dawa ya kutibu Minyoo, ni dawa inayotumiwa na watu wengi pale wanapokuwa na minyoo, walio wengi wamefanikiwa kupona kwa kutumia Dawa hii.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi dawa ya phenoxy-methyl penicillin ambayo upambana na aina ya bakteria ambao utoa sumu Ili kuzuia dawa isifanye kazi.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi dawa ya fluconazole ni dawa ya kutibu fangasi za aina au za sehemu mbalimbali,
Soma Zaidi...Asalaamu alykum warahmatullah wabarakaatuh Sifanjema zinamstahikia Allah Mola wa viumbe, muumba wa mbingu na ardhi na vilivyomo.
Soma Zaidi...