Dawa ya kutibu UTI

Dawa ya kutibu UTI

Nitakujuza dalili za UTI na dawa za kutibu UTI. Pia tutaona njia za kujikinga na UTI pamoja na dalili za UTI

Dawa ya kutibu UTI

Dawa ya UTI na UTI iliyo sugu
Kama ulishawahi kujiuliza masalikama chanzo cha UTI, sababu zake, njia za kukabiliana na uti vipi uti inaenezwa na ni zipi dawa zake. Makala hii ni kwa ajili yako, nimeiandaa kwa ufupi na kwa ufanisi kiasi cha kuweza kukuridhisha kwa majibu ya maswali yako. Kama utakuwa na mawazo zaidi, tuachie maoni yako hapo chini.



Ugonjwa wa UTI ni nini?
UTI ni kifupisho cha maneno Urinary Track Infection. Ni maambukishi na mashambulizi ya bakteria aina ya E.coil katika mfumo wa mkojo. Mwanzoni bakteria huingia kwenye kibofu, figo ama sehemu yeyote kwenye mfumo wa mkojo. Kisha bakteria huyu anaanza kushambulia na kuathiri mfumo huu na ndipo dalili za UTI huanza kuonekana kama maumivu wakati wa kukojoa. Dalili za uti huonekana kuanzia siku 3 mpaka 8 toka kuambukizwa.



Ni zipi sababu za UTI
Sababu kuu za ugonjwa wa UTI ni bakteria aina ya E.coil. Bakteria huyu huishi kwenye utumbo. Sasa endapoa atapata njia kutoka kwenye utumbo kupitia haja kubwa na akaingi kwenye mfumo wa mkojo hasa hasa kwa wanawake anasababisha UTI. Pia bakteria wanaoishi kwenye uke, mkundu na kuzunguka sehemu za siri wanaweza rahisi kupata njia na kuingia kwenye mfumo wa mkojo na kusababisha uti. Pia UTI inaweza kusababishwa na baadhi ya magonjwa ya ngono kama gonorrhea, chlamydia na mengine.



Ugonjwa wa uti unaenezwa vipi?
Mtu ataweza kupata UTI kama atafanya chochote ambacho kitaletwa bakteria wanaoishi kwenye utumbo kwenye kwenye nia ya mkojo. Kwa mfano kama wakati wa kuchamba alichamba kwa kuelekea mbele kisha bakteria waliotoka kupitia haja kubwa wakafikia kwenye uume ama uuke, hawa wataingi ndani na kusababisha uti. Si kawaida sana uti kuambukizwa kupitia ngono lakini inaweza kutokea. Na ndio maana inashauriwa ukakojoe baada ya kufanya ngono.



Pia maeneo ya chooni mtu anaweza kupata UTI ila pia hii hutokea mara chache sana na ni kwa wanawake ama kwa wale ambao wanajisaidi kwenye vyoo vya kukaa na si kucuchuchumaa ama kusimama hata hivyo si ahisi kwani lamda kama choo ni kichafu ndipo utapata UTI. Hata hivyo watu hawa wapo hatarini zaidi kupata UTI



1.Kama ulishawahi kupata UTI
2.Kama una kisikari
3.Kama una kiriba tumbo
4.Kama unatumia baadhi ya njia za kidhibiti uzazi kama spermicides au diaphrahm
5.Kama una vijiwe kwenye figo au kibofu na vijiwe hivi vikawa vinazuia mkojo kutoka kwa urahisi.
6.Kama ni mjamzito



Ni zipi dalili za UTI?
1.Maumivu wakati wa kukojoa na wakati mwingine yanafanana na kuhisi kuunguwa
2.Mkojo kuwa mchafu kkama wa mawingi ivi na unatowa harufu kali sana
3.Pia mgonjwa anaweza kuona damu ama kama usaha kwenye mkojo
4.Maumivu chini ya tumbo na mgongo
5.Homa
6.Kupatwa na baridi na hatimaye utetemeka
7.Kichefuchefu
8.Kutapika
9.Kuhisi uchovu sana.



NJIA ZA KUJIKINGA NA UTI
1.Kunywa maji mengi na ya kutosha
2.Dhibiti kisukari kama na kisukari
3.Punguza kula vitu vyenye sukari kwa wingi
4.Unapochamba jifute kuelekea nyuma
5.Punguza michepuko
6.Kojoa baada ya kushiriki tendo la ndoa
7.Kojoa pindi unapohisi mkojo
8.usitumie kondomu isiyo na vilainishi



Dawa ya uti
1.Amoxicillin/augmentin
2.Cetriaxone(rocephin)
3.Trimethoprim/sulfamethoxazole
4.Cephalexin
5.Ciprofloxacin (cipro)
6.Fosfomycin
7.Levofloxacin
8.Nitrofurantoin (mecrodantin)



Dawa kama ciprofloxacin na levofloxacin hutumika kutibu UTI sugu, hivyo si vyema kutumiwa kwa uti ya kawaida. Hata hivyo kabla ya kutumia dawa hizi hakikisha unapata ushauri wa daktari kwanza.





                   



Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu Rajabu
Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Dawa Main: Post File: Download PDF Views: 3210

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 ai web app     👉4 Dua za Mitume na Manabii     👉5 web hosting     👉6 Simulizi za Hadithi Audio    

Post zinazofanana:

Matibabu ya Fangasi ukeni na dawa za fangasi wanaoshambulia uke.

Fangasi wanaweza kushambulia uke, kwa juu kwenye mashhav ya uke ama kwa ndani. Hali hii inaweza kusababisha miwasho na maumivu pia. Inaweza kusababisha michubuko na kutofurahia tendo la ndoa. Makala hii inakwenda kukujuza dawa na matibabu ya fangasi ukeni

Soma Zaidi...
Fahamu dawa ya diazepam katika kutuliza kifafa

Post hii inahusu zaidi dawa ya diazepam katika kutuliza kifafa, ni dawa ambayo matumizi yake yanaweza kuingilia pote kwenye kutuliza kifafa na pia kwa wagonjwa wa akili.

Soma Zaidi...
Dawa za fangasi ukeni

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu dawa za fangasi ukeni

Soma Zaidi...
Dawa ya UTI

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu dawa ya UTI

Soma Zaidi...
Fahamu dawa ya cardiac glycoside katika matibabu ya magonjwa ya moyo

Post hii inahusu zaidi dawa ya cardiac glycoside katika matibabu ya magonjwa ya moyo,dawa maalum ambayo imo kwenye kundi hili la cardiac glycoside ni digoxin, ni dawa muhimu ambayo utumika kwenye mfumo wa vidonge mara nyingi.

Soma Zaidi...
Fahamu zaidi kuhusiana na Dawa inayotibu shinikizo la damu. iitwayo LASIX

Lasix (Furosemide) iko katika kundi la dawa zinazoitwa vidonge vya maji (loop diuretics) vidonge vya maji. Lasix hutumiwa kupunguza uvimbe mwilini unaosababishwa na kushindwa kwa moyo, ugonjwa wa ini, au ugonjwa wa figo. Kwa matibabu ya dalili nyingi.La

Soma Zaidi...