DAWA YA FANGASI
Fangasi ni katika magonjwa yanayoathiri watu wengi sana. Fangasi wanaweza kuathiri ngozi, nywele na kucha. Unaweza kujitibu fangasi kwa kwenda duka la dawa na kununua dawa bila ya kuhitaji usimamizi maalumu wa daktari ila hii ni kwa dawa za fangasi za kupaka. Za kunywa na sindano hakikisha unapata ushauri wa daktari kwanza. Kumbuka matibabu ya fangasi yanategemea aina ya fangasi wanaokusumbuwa.Aina za fangasi
1.Fangasi wa kwenye kucha
2. Fangasi wa Mapunye
3. Fangasi aina ya candida
4. Fangasi wa Mdomoni na kooni
5. Fangasi wa kwenye uke
6. Fangasi wanaoshambulia mfumo wa damu na ogran kama moyo, figo n.k
7. Fangasi aina ya Blastomyces
8. Fangasi wa sehemu za siriAina za dawa za kitubu fangasi.
Dawa za kutibu fangasi nazo zimegawanyika kama:-
1.Dawa za kupaka na kupulizia
2.Dawa za kumeza majimaji na vidonge
3.Sindano
4.Dawa za kuweka ili zimumunyike, hizi sana huwekwa kwenye uke.Orodha ya dawa za fangasi
1.Clotrimazole
2.Econazole
3.Miconazole
4.Terbinafine
5.Fluconazole
6.Ketokonazole
7.AmphotericinKazi za dawa za fangasi.
Dawa hizi zina kazi kuu 2 nazo ni:-
1.Kuuwa fangasi
2.Kuzuia fangasi kuzaliana na kukuwa.Athari zinazoweza kutokea wakati wa kutumia dawa za fangasi.
Haya ni matokea yanayoweza kutokea unapoanza kutumia dawa hizi. Si jambo la kuogopa.1.Miwasho
2.Kujihisi ovyoovyo
3.Kuharisha
4.Ukurutu
5.Unaweza kupata aleji