Fahamu kuhusu dawa za magonjwa ya moyo
Post hii inahusu zaidi dawa za magonjwa ya moyo, ni dawa ambazo utumika kusaidia pale moyo kama umeshindwa kufanya kazi ipasavyo.
Dawa za kutibu magonjwa ya moyo.
1. Kwanza kabisa kabla hatujaanza kuchambua dawa moja baada ya nyingine tunapaswa kufahamu kabisa kuhusu magonjwa ya moyo, ambapo kwa lugha ya kitaalamu magonjwa ya moyo huitwa cardiac failure , magonjwa ya moyo ni hali ambayo utokea kama moyo umeshindwa kufanya kazi yake vizuri kwa mfano moyo kushindwa kusukuma damu kwenye sehemu mbalimbali za mwili.
2. Kwa kawaida kuna dalili mbalimbali ambazo zinaweza kujitokeza kama moyo haufanyi kazi vizuri na dalili hizi ni pamoja na uchovu wa mara kwa mara, kushindwa kupumua vizuri, na wakati mwingine kifua kubana , kukonda kusiko kwa kawaida hata kama mgonjwa anakuwa anatumia chakula na dalili nyingine zinaweza kujitokeza kutoka kwa mgonjwa mmoja kwenda kwa mwingine.
3. Kutokana na kuwepo kwa magonjwa ya moyo kuna dawa mbalimbali ambazo utumika kutibu magonjwa ya moyo na lengo la dawa hizi ni kuhakikisha kwamba moyo unafanya kazi yake ipasavyo na kuhakikisha kwamba maumivu mbalimbali hayatokei kwa mgonjwa na pia dawa hizo zinatofautiana kutoka kwa dawa moja kwenda kwa nyingine kadri ya tatizo lilivyo.
4. Kuna dawa za moyo ambazo usaidia kama presha iko juu kitendo hiki kwa kitaalamu huitwa high blood pressure, hali hiyo uitwa magonjwa ya moyo kwa sababu kuna kipindi moyo unatumia nguvu kubwa kusukuma damu kwenye sehemu mbalimbali za mwili, hali hii ya moyo kutumia nguvu kusukuma damu utokea kwasababu ya mishipa ya damu kuwa nyembamba na kusababisha damu kutoweza kufika sehemu mbalimbali za mwili kusababisha moyo kutumia nguvu hali inayosababisha shinikizo la damu. Kwa hiyo kuna dawa za kutibu hali hiyo ya shinikizo la damu.
5. Pia kuna dawa za moyo ambazo usaidia kwenye matibabu ya kupambana na shinikizo kali la damu ambalo usababisha kiharusi, kwa kitaalamu huitwa stroke na myocardial infarction, kwa kawaida tunafahamu kwamba iwapo shinikizo la damu limekuwa sugu usababisha kiharusi ,kwa hiyo pia tutaweza kuona dawa za kutibu hali hiyo.
6 pia kuna dawa vile vile ambazo usaidia kutibu hali ya presha kuwa chini, kuna kipindi baada ya presha kubaki kwenye hali yake ya kawaida yenyewe inashuka hali inayosababisha matatizo kwa mgonjwa kama matibabu hayajatolewa, kwa hiyo tutaweza kuona dawa za kutibu hali hiyo.
7. Pamoja na kujua aina mbalimbali za magonjwa ya moyo tutaona jinsi dawa zinazotumika kutibu magonjwa ya moyo jinsi zinavyofanya kazi , kwanza dawa hizi uondoa chumvi kwenye moyo na maji yaliyozalishwa kwenye moyo na kusababisha moyo kuwa kawaida na kuweza kufanya kazi vizuri,kwa hiyo ili moyo ufanye kazi unahitaji chumvi na maji sawia yaani viwe vya kawaida, kwa hiyo maji yakiwa mengi kuzidi na chumvi ikizidi kwenye moyo ni hatari sana.
8. Pia dawa hizo usaidia kupandisha presha kama imeshuka na kuiweka kwenye hali ya kawaida, dawa ambayo kwa kawaida utumika uhakikisha kwamba presha hatishuki ovyo ovyo.
9. Pia dawa hizo upanua mishipa ya damu kama ni midogo na kusababisha damu kuweza kupita vizuri na kwenda kwenye sehemu mbalimbali za mwili na kushusha presha na ikiwa ya kawaida.
10. Baada ya kufahamu kazi za dawa hizi za magonjwa ya moyo na kufahamu magonjwa mbalimbali ya moyo ni vizuri kufahamu kwamba kila ugonjwa wa moyo huwa na dawa zake maalum ambazo utumika kutibu ugonjwa huo kwa hiyo ni vizuri kabisa kufuata utaratibu wa wataalamu wa afya.
11. Kwa hiyo baada ya kufahamu tofauti za magonjwa ya moyo ni vizuri kupima kwanza ili kufahamu kwamba upo kwenye kundi gani na kupewa dawa kadri ya tatizo.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Dua za Mitume na Manabii 👉2 kitabu cha Simulizi 👉3 Simulizi za Hadithi Audio 👉4 ai web app 👉5 web hosting 👉6 Tafasiri ya Riyadh Swalihina
Post zinazofanana:
Dawa ya kutibu ugonjwa wa PID
PID ni mashambulizi ya bakteria kwenye mfumo wa uzazi kwa wanawake. Hapa nitakujulisha dawa
Soma Zaidi...Faida za vidonge vya zamiconal
Posti hii inahusu zaidi faida za vidonge vya zamiconal, ni baadhi ya faida ambazo upatikana kutokana na vidonge vya zamiconal,ni vidonge ambavyo utibu au kusaidia kwenye matatizo ya viungo vya uzazi.
Soma Zaidi...Fahamu dawa ya hydralazine katika matibabu ya magonjwa ya moyo
Post hii inahusu zaidi dawa ya hydralazine katika matibabu ya magonjwa ya moyo, dawa hii imetoka kwenye kundi la vasodilators, na pia usaidia sana kwenye matibabu ya magonjwa ya moyo.
Soma Zaidi...Ushauri kabla ya kubeba mimba.
Posti hii inahusu zaidi ushauri kwa akina Mama na wachumba kabla ya kubeba mimba, kabisa ya kubeba mimba akina Mama na wachumba wanapaswa kufanya yafuatayo.
Soma Zaidi...Ifahamu dawa ya kupunguza maumivu
Post hii inahusu dawa ya aspirin katika kupunguza maumivu,ni dawa ambayo upunguz maumivu ya Kawaida, kushusha homa na pia usaidia kwenye magonjwa ya moyo hasa kuzuia stroke kama imetokea mda ndani ya masaa ishilini na manne
Soma Zaidi...Fahamu kuhusu dawa ya propranolol ambayo hutibu magonjwa ya moyo
Post hii inahusu zaidi dawa ya propranolol katika matibabu ya magonjwa ya moyo, dawa hii ipo kwenye kundi la beta blockers na ufanya Kazi mbalimbali hasa kwa wagonjwa wa moyo.
Soma Zaidi...