Fahamu dawa za 5-fluorouracil,Tegafur na uracili

Post hii inahusu zaidi dawa za 5-fluorouracil, Tegafur na uracili katika kupambana na kansa.

Fahamu kuhusu dawa za 5- fluorouracil, Tegafur na uracili katika kupambana na kansa,

1. Hizi ni dawa ambazo upatikana kwenye kundi la antimetabolite, dawa hizi usaidia kupambana na kansa za kwenye matiti, kansa ya damu ,kansa za kwenye kizazi na aina nyingine kadri ya wataalamu wa afya, dawa hizi ufanya kazi ya ya kuingilia nuclear ambayo kwa kitaalamu huitwa DNA na kuhakikisha kwamba seli ambazo hazihiitajiki zinaacha kabisa kuendelea kuzalishwa na kukomaa kabisa.

 

2. Kwa matumizi ya dawa hizi za 5-fluoro uracili, Tegafur na uracili usaidia kuondoa kabisa au kufubaisha zile seli za kansa ambazo zilikuwa zimekwisha zalishwa tayari na kuhakikisha kwamba zinapungua kabisa na haziendelei kuzalishwa , kwa watumiaji wazuri wa dawa na wale waliowahi kuanza matibabu hasa wa kansa ngazi ya kwanza na ya pili,wanaweza kupona ugonjwa huu.

 

3. Katika matumizi ya dawa hizi mgonjwa anapaswa kula mlo kamili na pia kula wingi wa matunda kwa sababu dawa hizi zina tabia ya kumaliza mgonjwa nguvu na pia kumbuka kuna baadhi ya seli ambazo tayari zimeshaanza kushambuliwa,na zingine zimeharibiwa na dawa kwa sababu kama dawa inatumika haijarishi aina ya seli  bali ufyeka seli zote, kwa hiyo kwa mgonjwa huyu matunda na mlo kamili ni lazima.

 

4. Vile vile dawa hizi zina maudhui madogo madogo ambayo ujitokeza na maudhi haya utofautiana kutoka kwa mgonjwa mmoja kwenda mwingine,na maudhi hayo ni kama vile vidonda kwenye midomo, kichefuchefu na kutapika,uchofu na kuishiwa nguvu, hamu ya kula kuwa ndogo hali ambayo usababisha mgonjwa kukonda kwa hiyo uangalizi wa mgonjwa huyu ni lazima hasa kwa upande wa chakula kwa sababu uchagua vyakula kwa hiyo anapaswa kupewa vyakula anavyovipenda.

 

5. Na kwa matumizi ya mda mrefu dawa hizi  usababisha nywele kuondoka na kubadilika kusiko kwa kawaida vile  vile kwa matumizi ya dawa hizi mgonjwa anaweza pia kuwa na viupele kwenye ngozi kwa hivyo usafi ni kawaida kwa mgonjwa huyu ili kuweza kuepukana na vi upele na kama mgonjwa yuko kwenye umri wa kuzaa anaweza kuwa mgumba kwa matumizi ya dawa hizi kwa mda mrefu na pengine hamu ya tendo la ndoa kupungua,

 

6. Kwa sababu ya kuwepo kwa maudhi madogo madogo pengine maudhui haya yanaweza kugeuka kuwa kama ugonjwa kwa hiyo matibabu ya matokeo ya dawa nayo yanatakiwa kwa mfano kama mgonjwa hana hamu ya kula ni vizuri kupewa dawa ya hamu ya kula, au kama mgonjwa anaharisha na kutapika ni vizuri kabisa kupewa dawa za kutapika na kuharisha au kama mgonjwa ana shida ya kuwa na choo kigumu ni vizuri kuwepo kwa dawa za kusaidia tatizo hilo, kwa hiyo matibabu ya matokeo ya dawa ni lazima ili kuweza kuhakikisha mgonjwa anaendelea vizuri.

 

7. Vile vile kama maudhui yamekuwa na matokeo mabaya ni vizuri kumbadilishia mgonjwa dawa na kumpatia dawa ambayo atatumia bila shida au kwa kuwepo maudhi madogo madogo ambayo hayamletei shida, pamoja na kuwepo kwa maudhi hayo pia dawa hizi hazipatiswi kutumiwa na watu ambao wana aleji au mzio wa 5-fluorouracil, Tegafur na uracili , kwa sababu kuna dawa nyingine ambazo wanaweza kutumia ili kuweza kuendelea na matibabu.

 

8. Vile vile dawa hizi hazitumiki kiholela zinapaswa kutumika kwa utaratibu wa wataalamu wa afya na pia wagonjwa wa kansa ni vizuri kabisa kupewa uangalizi wa karibu kwa hiyo sio vizuri kabisa kumeza dawa hizi kiholela.

 

9. Vile vile jamii inapaswa kufahamu kwamba ugonjwa huu wa kansa ya matiti,kansa ya kizazi na pia kansa  ya damu zinatibika kabisa kwa kutumia dawa hizi za 5-fluorouracil, Tegafur na uracili, kitu cha kwanza cha kufahamu ni kwamba mgonjwa anapaswa kufuata utaratibu wote wakati wa matibabu na pia kutunzwa vizuri na kupewa chakula cha kutosha na vilevile mgonjwa anapaswa kuwahi matibabu mapema kabisa , yaani kuanza matibabu kwenye ngazi ya kwanza na ya pili na pia mgonjwa akiongezea na matunzo pamoja na kumtia moyo kwa upande wa kansa ngazi ya kwanza na ya pili mgonjwa anaweza kupona .

 

10. Vile vile jamii inapaswa kuelezwa wazi kwamba kwa wagonjwa wanaoanza dawa wamechelewa wakiwa kwenye ngazi ya tatu na ya nne ni vigumu kupona haraka na kwa sababu ya kuwepo kwa matokeo ya dawa ambayo pengine ni makali kama kuharisha na kutapika , kupungua kwa seli mwilini na matokeo mengine kama tulivyoona hapo nyuma.kwa hiyo w agonjwa wa ngazi ya tatu na ya nne kupona kwao ni vigumu na kwa hivyo baadhi yetu wakiona dalili yoyote ambayo siyo ya kawaida ni vizuri, kama vile na uvumbe ambayo hayaeleweki ni vizuri kabisa kuwahi hospitali ili kama ni kansa matibabu yaanze mapema.

 

11. Vile vile jamii inapaswa kuachana na mila na desturi za kuogopa ugonjwa huu wa kansa na kwa wakati mwingine wengine wanafikia kiwango cha kuwatelekeza wagonjwa wao hospitalini  na kwa wakati mwingine wakihofia kuambukizwa na ugonjwa huo na wengine wanafikia kiwango cha kuamini kwamba mtu ambaye ana kansa hawezi kupona , kwa hiyo wafahamu kwamba wagonjwa wa kansa wakiwahi matibabu wanaweza kupona kabisa na kurudia hali zao za kawaida, ila shida watu wanashindwa kuwahi matibabu hali inayoendelea kuleta shida zaidi.

 

12. Kwa hiyo ni vizuri kabisa kuwa hudumia wagonjwa wa kansa na kuepuka na tabia ya kuwatenga kwa sababu kansa haijathibitishwa kwamba inaenea kutoka kwa mtu mmoja kwenda mwingine na kwa hiyo wagonjwa wanapaswa kuwekwa kutunzwa vizuri na kuwekwa kwenye hali ya kawaida kwani ni kama ugonjwa mwingine.

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Dawa Main: Afya File: Download PDF Views 848

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh    👉2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉3 Madrasa kiganjani    👉4 Bongolite - Game zone - Play free game    👉5 Simulizi za Hadithi Audio    👉6 kitabu cha Simulizi   

Post zinazofanana:

Fahamu dawa ya maumivu aina ya indomethacin

Post hii inahusu zaidi dawa ya kutibu au kutuliza maumivu, kwa majina huiitwa indomethacin ni dawa inayotumika kutuliza maumivu ya Kawaida.

Soma Zaidi...
Fahamu kuhusu kundi la diuretics

Post hii inahusu zaidi kundi la diuretics,ni kundi mojawapo kati ya makundi ya dawa zinazosaidia katika matibabu ya magonjwa ya moyo.

Soma Zaidi...
Dawa za fangasi ukeni

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu dawa za fangasi ukeni

Soma Zaidi...
Dawa ya maumivu ya jino

Somo Hili linakwenda kukuletea dawa ya maumivu ya jino

Soma Zaidi...
Fahamu kuhusu dawa ya kaoline

Post hii inahusu dawa ya kaoline katika kutibu au kuzuia kuharisha ni dawa ambayo imependekezwa kutumiwa hasa kwa wale walioshindwa kutumia dawa ya loperamide.

Soma Zaidi...
Fahamu dawa ambazo uchangia kupungua kwa nguvu za kiume

Post hii inahusu zaidi dawa mbalimbali ambazo uchangia katika kupunguza nguvu za kiume , hii ni kwa sababu ya wataalamu mbalimbali wanavyosema

Soma Zaidi...
Dawa ya fangasi uumeni

kama unasumbuliwa na fangasi uumeni, nitakujuza dawa yake, sababu za fangasi uumeni, matibabu yake na njia za kuwaepuka

Soma Zaidi...
Fahamu matumizi ya Dawa iitwayo Aspirin.

Aspirini Ni dawa ya kutuliza maumivu.Majina yanayoaminika zaidi katika kutuliza maumivu sasa yanapatikana kwa njia mbadala inayookoa gharama kwa kutumia Aspirini. Aspirini inayopendwa na familia kwa miongo kadhaa, mara nyingi hutumiwa kupunguza maumivu y

Soma Zaidi...