Dawa ya fangasi uumeni
Fangasi wanaweza kuathiri watu wa marika yeto, pia kuathiri maeneo mengi ya mwili. Lakini hapa nitakuletea fangasi wanaoathiri uume, sababu zao, dalili zao na dawa inayotumika kutibu fangasi hawa wa kwenye uume.



Dalili za fangasi wa kwenye uume
1.Upele na ukurutu kwenye uume
2.Vidoadoa vyeupe kwenye uume
3.Uume kuwa na umajimaji kwenye ngozi yake
4.Kwa ambao hawajatahiriwa kutakuwa na uchafu mweume kwenye ngozi ya govi
5.Miwasho kwenye uume na kuhisi kuunguwa



Nini sababu ya fangasi hawa wa kwenye uume?
Fangasi wa kwenye uume husababishwa na aina ya fangasi inayojulikana kama candida. fangasi hawa wanapenda sana maeneo yenye majimaji. Hususan sehemu za siri ambapo ndipo panakuwa na majimaji mengi. Fangasi hawa wanaweza kuambukizwa kwa kupitia ngono. Usafi wa sehemu za siri ukawa ni mbovu hali inaweza kuwa mbaya zaidi.



Watu walio hatarini kupata fangasi wa uumeni
1.Watu walio na Uchafu wa mwili hasa sehemu za siri
2.Watu walio na kisukari
3.Watu wenye viribatumbo (kitambi)
4.Watu wenye kinga dhaifu kama waathirika wa VVU ama walioanza matibabu ya saratani
5.Watu ambao hawajatahiriwa



Dawa zinazotumika kutibu fangasi wa uumeni
Fangasi hawa wanaweza tu kutibiwa kwa dawa za fangasi za kupaka yaani za losheni kama:-
1.Miconazole (lotrimin AF, Ceruex, Desenex, Ting Antifungal)
2.Imidazole (canesten, Selezen)
3.Clotrimazole (Lotrimin AF, Anti-Fungal, Cruex, Desenex, Lotrimin AF Ringworm)



Pia endapo hali itaendelea, mgonjwa anaweza kutumia dawa za kumeza, baada ya kupata ushauri kwa daktari. Dawa hizi ni kama:-
1.Fluconazole (Diflucan) hii ni ya kumeza pia hutumika pamoja na ya kupaka inayoitwa hydrocortisone cream. Tiba hii hasa ni kwa wale ambao hali imekuwa mbaya sana (balanitis).



TIBA MBADALA ZA KUTIBU FANGASI WA UUMENI
1.Mafuta ya majani ya chai
2.Kitunguu thaumu
3.Siki ya epo
4.Mafuta ya nazi
5.Mafuta ya karafuu



Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi, ama tuachie maoni yako hapo chini.