Zijuwe aina za minyoo na tiba yake. Dawa 5 za kutibu minyoo ya aina zote
DAWA YA MINYOO
Minyoo ni wadudu aina ya parasite ambao wanaingia kwenye miili ya kiumbe hai kama wanyama na binadamu, na wanajipatia chakula chao humo na kuishi. Kwa binadamu kuna minyoo aiina nyingi sana inayo weza kuwaathiri. Ila zipo aina tatu ambazo zinaonekana ni zaidi kuathiri binadamu. Nazo ni kama:-
1.Minyoo aina ya Roundworms hawa wanaingia kwenye miili yetu kupitia vyakula tunavyokula ama vinywaji endapo hivyo vyakula ama vinywaji vitakuwa na mayai yao. Minyoo hawa wanataga na kuishi kwenye utumbo. Minyoo hawa ni pamoja na threadworm, ascaris, hookworm na trichuris.
2.Minyoo aina ya tapeworm, hawa hishi kwenye tumbo, mara nyingi tunaweza kuwapata minyoo hawa kwa kula chakula ambacho hakikupikwa ama hakikuwiva vyema kama nyama, mihogo mibichi n.k
3.Flukeworms, minyoo hawa huingia mwilini mwetu na kuishi kwenye damu, tumbo, mapafu ama kwenye ini. Unaweza kuwapata minyoo hawa kwa kuogelea ama kuoga kwenye maji yenye minyoo hawa. Mimnyoo hawa husababisha pia ugonjwa ujulikanao kama kichocho (schistosomiasis).
Ni dawa gani hutibu minyoo?
Kwa ufupi tiba ya minyoo hutofautiana kulingana na aina ya minyoo na kiasi cha athari ndani ya mwili. Kwa kiasi kikubwa dawa aina ya Mebendazole imekuwa ikitumika kwa kiasi kikubwa sana maeneo mengi. Na hii ni kwa sababu dawa hii inatumika sana kutibu minyoo aina ya threadworm ambao minyoo hawa ndio wanaathiri watu zaidi. Pia inaweza kutibu aina nyinginyingi za minyoo. Dawa nyingine za kutibu minyoo ni:-
1.Levamisole
2.Tiabendazole
3.Ivermectin
4.Niclosamide
5.Praziquantel
6.Albendazole
7.Diethylcarbamazine
Dawa hizi zinafanyaje kazi?
Yes hili ni swali zuri sana. Sasa inakupasa ujuwe namna ambavyo dawa hizi zitakusaidia kutibu minyoo. Dawa hizi zinafanya kazi kama ifuatavyo:-
A.Mebendazole, albendazole na tiabendazole hizi kuzuia minyoo isifyonze chakul (sugar) kutoka kwenye miili yetu. Hivyo wanaweza kufa kwa njaa. Ila dawa hii itauwa minyoo lakini sio mayai yao ambayo wameyataga tayari.
B.Praziquantel na ivermectin, dawa hizi husaidia kuwazubaisha minyoo kwenye utumbo, hivyo wanaweza kutolewa kwa njia ya haja kubwa.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowJe umeipenda post hii ?
Maumivu ya mgongo hutokea sana kwa wajawazito. Ijapokuwa ni hali ya usumbufu sana ila hakikisha hautumii madawa kiholela kutoka maduka ya dawa ama miti shamba. Kwani ukikisea kidogobinawezabhatarisha afya ya mtoto
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi dawa za cyclophosphamide na mustargen katika kupambana na ugonjwa wa Kansa.
Soma Zaidi...Hapa utajifuanza dalili za presha ya kushuka, na dawa ya presha ya kushuka na nJia za kuzuiaama kudhibiti presha ya kushuka
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi dawa ya Carvedilol na kazi yake, ni dawa inayotibu au kuzuia mapigo ya moyo ambayo yako juu na kusababisha kulegeza kwa mishipa ya moyo.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu dawa mbadala za vidonda vya tumbo
Soma Zaidi...Post hii inahusu dawa ya aspirin katika kupunguza maumivu,ni dawa ambayo upunguz maumivu ya Kawaida, kushusha homa na pia usaidia kwenye magonjwa ya moyo hasa kuzuia stroke kama imetokea mda ndani ya masaa ishilini na manne
Soma Zaidi...Post hii inahusu dawa za kutuliza kifafa, zipo dawa mbalimbali za kutuliza kifafa Leo tutaona dawa mojawapo inayoitwa phenobarbital katika kutuliza kifafa.
Soma Zaidi...Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu dawa za mitishamba za kutibu meno
Soma Zaidi...