Post hii inahusu zaidi dawa ya pyrantel pamoate ni dawa ambayo usaidia kutibu minyoo ambayo kwa kawaida ukaa kwenye utumbo mdogo.
1. Pyrantel pamoate ni aina mojawapo ya dawa ambayo utumika kutibu minyoo ambayo ukaa kwenye utumbo mdogo yaani kwa kitaalamu kwenye intestinal nematode hiyo ndiyo kazi yake na pia inaweza kufanya kazi kama dawa za Albendazole na mebendazole kwa sababu ya kupambana na aina ya minyoo inayotibiwa na na dawa hizo ambayo ni hookworm na pinworn.
2. Dawa hii pia ipo kwenye mfumo wa vidonge na pia utafunwa na kumezwa bila maji na pia utumika kabla ya kula kitu chochote ili kuweza kukabiliana vizuri na minyoo ambayo iko tumboni, kwa matumizi yake au namna ya kutumia ni kwa kadiri ya maagizo ya daktari au mtaalamu wa afya.
3. Pia dawa hii utumika kwa watu wote wakubwa na wadogo isipokuwa watoto wadogo chini ya miaka miwili na akina Mama wajawazito wenye mimba changa hawapaswi kutumia dawa hii kwa kuepukana na mimba kutoka, kwa hiyo wajawazito wanapaswa kufuata utaratibu wa wataalamu wa afya hasa wakiwa kliniki na sio kununua dawa na kutumia kwa sababu wanaweza kujiletea matatizo makubwa.
4. Pia dawa hii huwa na maudhi madogo madogo kama vile maumivu ya kichwa, maumivu ya tumbo, kichefuchefu na kutapika, kizunguzungu, kuchoka mara kwa mara kwa watumiaji wa dawa za pyrantel pamoate wakiona dalili kama hizi ni vema kabisa kufahamu kwamba ni matokeo ya dawa na pia hali ikiwa mbaya ni vema kabisa kuwaona wataalamu wa afya.
5. Pia jamii inapaswa kuelewa kwamba dawa hii haitumiki kiholela ni kufuata utaratibu wa wataalamu wa afya na kujua matumizi yake, endapo ikitumika visivyo inaweza kuleta matokeo mabaya kwa watumiaji hasa wajawazito na watoto chini ya miaka miwili, kwa hiyo kwa upande wa wajawazito ni vizuri kufuata masharti ya kliniki hasa mimba ikiwa changa katika matumizi ya dawa na pia mtoto anapaswa kupelekwa kliniki ikitokea kama anaumwa ili apewe dawa zake.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Posti hii inahusu zaidi matumizi ya dawa za vidonda vya tumbo, ili kuweza kutumia dawa hizi ni vizuri kabisa kufuata mashariti kama ifuatavyo.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi dawa ya hydralazine katika matibabu ya magonjwa ya moyo, dawa hii imetoka kwenye kundi la vasodilators, na pia usaidia sana kwenye matibabu ya magonjwa ya moyo.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi tiba ya jino,ni tiba ya kawaida kwa watu walio na matatizo ya meno, kwa kawaida tunafahamu kwamba jino huwa halina dawa ila dawa yake huwa ni kungoa lakini Leo nawaletea habari njema kwamba jino sio kungoa tena ila Kuna tiba ambayo
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi dawa ambazo zinatumika kwenye matibabu ya kansa, dawa hizi usaidia kuharibu seli ambazo ambazo hazistahili kwa kitaalamu huitwa malignant seli.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi njia kuu nne ambazo utumika kumpatia mgonjwa dawa, Ili kumpatia mgonjwa dawa Kuna njia za kutumia kama ifuayavyo.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi dawa ya mucolytic katika kutibu kikohozi kwa watu wazima na watoto.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi dawa ya streptomycin ni dawa mojawapo ya kupambana na bakteria hasa wanaoshambulia mfumo wa hewa.
Soma Zaidi...