Dawa ya minyoo

Dawa ya minyoo

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu dawa za minyoo

DAWA YA MINYOOMinyoo ni wadudu aina ya parasite ambao wanaingia kwenye miili ya kiumbe hai kama wanyama na binadamu, na wanajipatia chakula chao humo na kuishi. Kwa binadamu kuna minyoo aiina nyingi sana inayo weza kuwaathiri. Ila zipo aina tatu ambazo zinaonekana ni zaidi kuathiri binadamu. Nazo ni kama:-

 

1.Minyoo aina ya Roundworms hawa wanaingia kwenye miili yetu kupitia vyakula tunavyokula ama vinywaji endapo hivyo vyakula ama vinywaji vitakuwa na mayai yao. Minyoo hawa wanataga na kuishi kwenye utumbo. Minyoo hawa ni pamoja na threadworm, ascaris, hookworm na trichuris.

 

2.Minyoo aina ya tapeworm, hawa hishi kwenye tumbo, mara nyingi tunaweza kuwapata minyoo hawa kwa kula chakula ambacho hakikupikwa ama hakikuwiva vyema kama nyama, mihogo mibichi n.k

 

3.Flukeworms, minyoo hawa huingia mwilini mwetu na kuishi kwenye damu, tumbo, mapafu ama kwenye ini. Unaweza kuwapata minyoo hawa kwa kuogelea ama kuoga kwenye maji yenye minyoo hawa. Mimnyoo hawa husababisha pia ugonjwa ujulikanao kama kichocho (schistosomiasis).

 

Ni dawa gani hutibu minyoo?Kwa ufupi tiba ya minyoo hutofautiana kulingana na aina ya minyoo na kiasi cha athari ndani ya mwili. Kwa kiasi kikubwa dawa aina ya  HYPERLINK "https://www.bongoclass.com/dawa/Mebendazole" Mebendazole imekuwa ikitumika kwa kiasi kikubwa sana maeneo mengi. Na hii ni kwa sababu dawa hii inatumika sana kutibu minyoo aina ya threadworm ambao minyoo hawa ndio wanaathiri watu zaidi. Pia inaweza kutibu aina nyinginyingi za minyoo. Dawa nyingine za kutibu minyoo ni:-

 

1.Levamisole2.Tiabendazole3.Ivermectin4.Niclosamide5.Praziquantel6.Albendazole7.Diethylcarbamazine

 

Dawa hizi zinafanyaje kazi?Yes hili ni swali zuri sana. Sasa inakupasa ujuwe namna ambavyo dawa hizi zitakusaidia kutibu minyoo. Dawa hizi zinafanya kazi kama ifuatavyo:-

 

A.Mebendazole, albendazole na tiabendazole hizi kuzuia minyoo isifyonze chakul (sugar) kutoka kwenye miili yetu. Hivyo wanaweza kufa kwa njaa. Ila dawa hii itauwa minyoo lakini sio mayai yao ambayo wameyataga tayari.

 

B.Praziquantel na ivermectin, dawa hizi husaidia kuwazubaisha minyoo kwenye utumbo, hivyo wanaweza kutolewa kwa njia ya haja kubwa.

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu Rajabu
Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Dawa Main: Post File: Download PDF Views: 2528

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Tafasiri ya Riyadh Swalihina     👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉5 kitabu cha Simulizi     👉6 Dua za Mitume na Manabii    

Post zinazofanana:

Fahamu kuhusu dawa za Doxorubicin na Daunorubicin

Post hii inahusu zaidi dawa za Doxorubicin and Daunorubicin katika kupambana na kansa.

Soma Zaidi...
Dawa ya Vidonda vya tumbo

Nitakujuza dawa ya kutibu vidonda vya tumbo, na kutibu vidonda vya tumbo sugu

Soma Zaidi...
Dawa za mitishamba za kutibu meno

Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu dawa za mitishamba za kutibu meno

Soma Zaidi...
Fahamu kuhusu dawa ya pyrantel pamoate

Post hii inahusu zaidi dawa ya pyrantel pamoate ni dawa ambayo usaidia kutibu minyoo ambayo kwa kawaida ukaa kwenye utumbo mdogo.

Soma Zaidi...
Dawa ya chango na maumivu ya hedhi

Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu dawa ya chango na maumivu ya hedhi

Soma Zaidi...
Matumizi ya dawa ya vidonda vya tumbo

Posti hii inahusu zaidi matumizi ya dawa za vidonda vya tumbo, ili kuweza kutumia dawa hizi ni vizuri kabisa kufuata mashariti kama ifuatavyo.

Soma Zaidi...