Fahamu kuhusu dawa ya mucolytic dawa ya kutibu kikohozi

Post hii inahusu zaidi dawa ya mucolytic katika kutibu kikohozi kwa watu wazima na watoto.

Fahamu dawa ya mucolytic katika matibabu ya kikohozi.

1. Dawa ya mucolytic ni mojawapo ya dawa ambayo imependekezwa katika matibabu ya kikohozi ni dawa ambayo utumiwa na watu wengi na imeweza kuleta matokeo makubwa kwa watumiaji, dawa hii ufanya kazi ya kutenganisha vikohozi vilivyokusanyana na kuvifanya viwe virahini na kuzibua sehemu mbalimbali ambazo zimezibwa na vikohozi hivyo kwa kufanya hivyo vikohozi uweza kuwa raini na hata mgonjwa akikohoa hawezi kutumia zaidi.

 

2.Na vile vile kama kuna mikusanyiko mbalimbali ya uchafu kwenye sehemu ya mfumo wa hewa uweza kutenganisha uchafu huo na hali huwa kawaida na pia mgonjwa anaweza kutoa uchafu huo kwa kukohoa bila matatizo zaidi kwa sababu ni mwepesi dawa hizi inawezekana kupitishwa mdomoni na kufanya kazi kupitia kwenye mzunguko wa damu na kuleta matokeo mazuri.

 

3. Pia wakati ematumizi ya dawa hizi ya mucolytic kuna maudhi madogo madogo ambayo ujitokeza nayo ni kama kichefuchefu na kutapika,na pia kufanya sehemu za kwenye mfumo wa hewa kulegea kwa mda na pia mgonjwa kuishiwa nguvu baada ya kuzitumia na pia mgonjwa kuhisi kizunguzungu na kuchoka ,kwa hiyo mgonjwa akisikia hayo hapaswi kujiuliza bali anapaswa kufahamu kwamba ni matokeo ya dawa.

 

4. Vile vile dawa hizi uweza kutumiwa na watu mbalimbali ila kwa wale wenye matatizo ya pumu na presha ya kupanda wanapaswa kutumia dawa hizi kwa uangalifu kwa sababu iwapo dawa hizi zinatumika na pia mgonjwa wa pumu akijisikia vibaya na akatumia dawa za pumu pamoja na hizi za kikohozi anaweza kusababisha mapafu kupanuka zaidi na kuleta madhara makubwa zaidi kuliko kama tulivyotegemea, basi katika matumizi ya dawa hizi ni vizuri kabisa kuongea na wataalamu wa afya.

 

5. Kwa sababu hii ni dawa ya kikohozi na zipo madukani kwa wingi kwa hiyo hatupaswi kuzitumia kiholela bali tuzingatie ushauri wa madaktari na wataalamu wengine wa afya.



Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/12/23/Friday - 08:07:42 pm     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 809


Download our Apps
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-