Dawa ya UTI

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu dawa ya UTI

Dawa ya UTI na UTI iliyo suguKama ulishawahi kujiuliza masalikama chanzo cha UTI, sababu zake, njia za kukabiliana na uti vipi uti inaenezwa na ni zipi dawa zake. Makala hii ni kwa ajili yako, nimeiandaa kwa ufupi na kwa ufanisi kiasi cha kuweza kukuridhisha kwa majibu ya maswali yako. Kama utakuwa na mawazo zaidi, tuachie maoni yako hapo chini.

 

Ugonjwa wa UTI ni nini?UTI ni kifupisho cha maneno Urinary Track Infection. Ni maambukishi na mashambulizi ya bakteria aina ya E.coil katika mfumo wa mkojo. Mwanzoni bakteria huingia kwenye kibofu, figo ama sehemu yeyote kwenye mfumo wa mkojo. Kisha bakteria huyu anaanza kushambulia na kuathiri mfumo huu na ndipo dalili za UTI huanza kuonekana kama maumivu wakati wa kukojoa. Dalili za uti huonekana kuanzia siku 3 mpaka 8 toka kuambukizwa.

 

Ni zipi sababu za UTISababu kuu za ugonjwa wa UTI ni bakteria aina ya E.coil. Bakteria huyu huishi kwenye utumbo. Sasa endapoa atapata njia kutoka kwenye utumbo kupitia haja kubwa na akaingi kwenye mfumo wa mkojo hasa hasa kwa wanawake anasababisha UTI. Pia bakteria wanaoishi kwenye uke, mkundu na kuzunguka sehemu za siri wanaweza rahisi kupata njia na kuingia kwenye mfumo wa mkojo na kusababisha uti. Pia UTI inaweza kusababishwa na baadhi ya magonjwa ya ngono kama gonorrhea, chlamydia na mengine.

 

Ugonjwa wa uti unaenezwa vipi?Mtu ataweza kupata UTI kama atafanya chochote ambacho kitaletwa bakteria wanaoishi kwenye utumbo kwenye kwenye nia ya mkojo. Kwa mfano kama wakati wa kuchamba alichamba kwa kuelekea mbele kisha bakteria waliotoka kupitia haja kubwa wakafikia kwenye uume ama uuke, hawa wataingi ndani na kusababisha uti. Si kawaida sana uti kuambukizwa kupitia ngono lakini inaweza kutokea. Na ndio maana inashauriwa ukakojoe baada ya kufanya ngono.

 

Pia maeneo ya chooni mtu anaweza kupata UTI ila pia hii hutokea mara chache sana na ni kwa wanawake ama kwa wale ambao wanajisaidi kwenye vyoo vya kukaa na si kucuchuchumaa ama kusimama hata hivyo si ahisi kwani lamda kama choo ni kichafu ndipo utapata UTI. Hata hivyo watu hawa wapo hatarini zaidi kupata UTI

 

1.Kama ulishawahi kupata UTI2.Kama una kisikari3.Kama una kiriba tumbo4.Kama unatumia baadhi ya njia za kidhibiti uzazi kama spermicides au diaphrahm5.Kama una vijiwe kwenye figo au kibofu na vijiwe hivi vikawa vinazuia mkojo kutoka kwa urahisi.6.Kama ni mjamzito

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Dawa Main: Afya File: Download PDF Views 2024

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Simulizi za Hadithi Audio    👉2 Kitau cha Fiqh    👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉4 kitabu cha Simulizi    👉5 Kitabu cha Afya    👉6 Bongolite - Game zone - Play free game   

Post zinazofanana:

Ushauri kabla ya kubeba mimba.

Posti hii inahusu zaidi ushauri kwa akina Mama na wachumba kabla ya kubeba mimba, kabisa ya kubeba mimba akina Mama na wachumba wanapaswa kufanya yafuatayo.

Soma Zaidi...
IJUE DAWA YA AMOXLINE (antibiotic) NA MATUMIZI YAKE

Posti hii inahusu zaidi dawa ya amoxline .jinsi inavyofanya kazi mwilini.pamoja na matumizi yake.

Soma Zaidi...
Dawa za kutibu fangasi kwenye kucha

Makala hiii inakwenda kukueleza dawa za kutibu fangasi kwenye kucha.

Soma Zaidi...
Fahamu dawa za kutuliza aleji au mzio

Post hii inahusu zaidi dawa hydrocortisone kwa kutuliza aleji au mzio, kwa kawaida Kuna mda mtu anapotumia dawa Fulani anakuwa na mabadiliko mbalimbali kama vile kifua kubana , viupele na mambo kama hayo.

Soma Zaidi...
Dawa ya chango na maumivu ya hedhi

Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu dawa ya chango na maumivu ya hedhi

Soma Zaidi...
Matumizi ya dawa ya vidonda vya tumbo

Posti hii inahusu zaidi matumizi ya dawa za vidonda vya tumbo, ili kuweza kutumia dawa hizi ni vizuri kabisa kufuata mashariti kama ifuatavyo.

Soma Zaidi...
Dawa za Anesthesia katika kutuliza maumivu.

Unapotaka kufanyiwa baadhi ya matibabu unatakiwa kupewa ganzi ama nusu kaput ili kulifanyia usihisi maumivu. Dawa hizi zinajulikana na Anesthesia.

Soma Zaidi...
Fahamu dawa ya sulfonamide dawa inayopambana na maambukizi ya bakteria mwilini.

Post hii inahusu zaidi dawa ya sulphonamide ni mojawapo ya dawa ambayo usaidia kutibu magonjwa mbalimbali yanayosababishwa na bakteria ni dawa au antibiotics ya mda mrefu na pia matumizi yake sio makubwa sana kwa sababu ya kuwepo kwa antibiotics zenye ngu

Soma Zaidi...
Dawa ya Vidonda vya tumbo

Nitakujuza dawa ya kutibu vidonda vya tumbo, na kutibu vidonda vya tumbo sugu

Soma Zaidi...