Usisumbuliwe tene na fangasi ukeni, zijuwe hapa dalili za fangasi ukeni, tiba yake na njia za kukabiliana na fangasi ukeni
DAWA YA FANGASI UKENI
Fangasi ukeni wanaweza kuwa ni tatizo kubwa na wakati mwengine wanaweza kuleta aina, madhara na kupoteza ladha ya mapenzi. Fangasi ukeni ni rahisi kutibika kama mwanamke atatumia dawa kwa uangalifu. Unaweza kutibu fangasi ukeni kwa kutumia dawa za kupata kutoka katika maduka ya dawa. Kama hali haina nafuu muonedaktari anaweza kukuandikia dawa za kumeza ama sindano ikibidi. Kunawada nyingine si za kupaka ila ni vidonge, hivi mwanamke ataweza ukeni na kitamumunyika chenyewe.
Makala hii inakwenda kukuletea tiba na dawa za fangasi ukeni, sababu zake, namna ya kupambana na fangasi hawa na dalili za fangasi ukeni. Pia tutaona madhara ya fangasi ukeni endapo watachelewa kutibiwa. Soma mkala hii hadi mwisho huwenda ikakusaidia sana.
1.Dawa ya fangasi ukeni ya kupaka
A.Clotrimazole
B.Miconazole
C.Tioconazole
D.Terconazole
E.Butoconazole
Ni vyema kumuona daktari kwanza kabla hujatumia dawa hizi. Kwa mfano terconazole na butoconazole zinahitaji maelezo kutoka kwa daktari kwa usalama zaidi wa afya yako.
2.Dawa ya fangasi ukeni ya kumeza
Endapo dawa za kupaka hazikuonyesha ahueni, mgonjwa atabadilishiwa dawa na kupewa za kumeza ama sindano.fluconazoe (diflucan) hii ni nzuri sana kwa wenye fangasi silizoshindikana kwa dawa za kupaka. Pata kwa nza maelezo ya daktari kabla ya kutumia. Dawa hii haitumiwi na wajawazito. Ukitumia dawa hii unaweza kuona mabadiliko kama maumivu ya tumbo au tumbo kuvurugika na maumivu ya kichwa.
3.Dawa ya fangasi ukeni walio sugu (azole resistant therapy).
Dawa hii sio ya kumeza, maana ni hatari sana. Napi asio ya kupaka. Dawa hii hutumika endapo ddawa za hapo juu zimeshindikana. Kwanamke atapewa dawa hii aiingize kwenye uke wake.
Nini kinasababisha fangasi ukeni?
Fangasi ukeni husababishwa na ina ya fangasi wanaoitwa candida albican. Kikawaida ukeni kuna bakteria na fangasi aina ya candida kwa kiwango maalumu. Pia kuna aina ya fangasi waitwao lactobacillus hawa huzuia ongezeko la fangasi candida wasiwe wengi kupitiliza. Sasa endapo fangasi candida wakizaliana kwa wingi na kupitiliza kiwango ndipo madhara yanaanza kuonekana. Swali la kijuliza hapa inakuwaje fangasi hawa wanazaliana zaidi?
Sababu za kuzaliana fangasi ukeni kwa wingi:
A.Kama mwanamke anatumia dawa za antibiotics
B.Kama mwanamke ana mimba
C.Kisukari kilichoshindwa kudhibitiwa
D.Mfumo wa kinga kudhoofu
E.Kutumia dawa za kudhibiti uzazi wa mpango dawa za kumeza.
Namna ya kujilinda na fangasi wa ukeni
1.Jiepushe kuvaa nguo za ndani zilizobana sana
2.Jizuie kusafisha uke kwa kemikali
3.Jiepushe na baadhi ya vifaa vya wanawake vilivyowekewa manukato kama pedi zenye manukato, badhi ya sabuni zenye manukato za kusafishia uke n.k
4.Kama huna ulazima wa kutumia antibiotics wacha kutumia
5.Usivae nguo zenye majimaji, hakikisha nguo zako ni kavu, ni vuema zile za ndani zikawa ni za pamba.
Dalili za fangasi ukeni
1.Miwasho ukeni
2.Maumivu wakati wa kukojo ana wakati wa kushiriki tendo landoa. Maumivu haya yanaweza kuwa kama unaunguwa ivi
3.Kuvimba kwa papa na kuwa nyekundu
4.Uke kuuma
5.Uke kuota upele ama ukurutu
6.Kutokwa na uchafu ukeni
7.Uke kutoa majimaji memngi
ATHARI ZA KUTOTIBU FANGASI
A.Kuendelea kupata maumivu
B.Kutoa harufu
C.Kuchubuka na hatimaye vidonda
D.Kujikuna muda wote
E.Kutokuwa na raha
F.Maumivu wakti wakukohoa na kushiriki tendo la ndoa
G.Kukosa hamu ya kushiriki tendo ka ndoa.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowJe umeipenda post hii ?
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu dawa za vidonda vya tumbo
Soma Zaidi...Ukiwa mjamzito uwe makini sana katika kuchagua matumizi ya dawa. Vinginevyobinawwza kuwa hatari. Hapa nitakujuza dawa ambazo ni hatari kutumia kwa ujauzito wako.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi ushauri kwa akina Mama na wachumba kabla ya kubeba mimba, kabisa ya kubeba mimba akina Mama na wachumba wanapaswa kufanya yafuatayo.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi dawa za Doxorubicin and Daunorubicin katika kupambana na kansa.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi Dawa ya Rifampicin na kazi zake, hii ni dawa mojawapo inayotibu kifua kikuu kati ya Dawa zilizoteuliwa kutibu ugonjwa wa kifua kikuu.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi dawa ya amoxline .jinsi inavyofanya kazi mwilini.pamoja na matumizi yake.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu dawa ya chango na dawa ya maumivu ya hedhi
Soma Zaidi...Posti hii inahusu dawa ya salbutamol na kazi yake ya kutibu ugonjwa wa Asthma, ni dawa mojawapo ambayo imetumia na watu wengi na wamefanikiwa kwa kiwango kikubwa, kwa hiyo zifuatazo ni kazi ya Dawa hii ya salbutamol katika kutibu Asthma.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi dawa ya Albendazole ni mojawapo ya dawa ambazo usaidia kutibu minyoo, na pia imefanikiwa sana kadri ya watumiaji wa dawa hiyo.
Soma Zaidi...