Post hii inahusu zaidi dawa ya kutibu ukoma,na dawa hiyo ni dawa ya Dapsoni, hii dawa usaidia kuzuia nerve zisiendelee kupoteza kazi yake pia na ngozi iendelee kuwa kawaida
1. Ukoma ni mojawapo ya ugonjwa ambao uharibu nerve na mfumo mzima wa fahamu ambapo mgonjwa mara nyingi ushindwa kuhisi vitu vya hatari kama moto kwa sababu ya kuharibika kwa mfumo wa fahamu, pia na viungo kama vidole uweza kukatika yeye bila kuwa na taarifa yoyote Ile hali ambayo upelekea na ngozi ya mwili kutonawili ,kwa hiyo hata jamii uwatenga wagonjwa hawa, kwa matumizi ya dawa ya dapsoni utibu uaribifu wa nerve na kuzuia uaribifu wa ngozi na kumweka mgonjwa kwenye hali nzuri na akakubarika katika jamii.
2. Dawa hii kwa kawaida IPO kwenye mfumo wa vidonge na utumiwa kila kila siku kwa kadri ya maagizo ya wataalamu wa afya, matibabu ya ugonjwa huu dawa uanza kutumika kidogo kidogo na baadae dozi uongezeka kuanzia mwezi wa kwanza mpaka wa pili, na matibabu yake ni marefu kidogo kwa sababu utumia takribani miezi kumi na minane na matibabu yanaweza kuendelea kwa kutegemea hali ya mgonjwa kwa sababu kuna wagonjwa ambao uanza matibabu mwanzoni mara tu wanapoona dalili Ila Kuna wale wanaoanza kwa kuchelewa na Kuna wale wanaofuatwa kutoka majumbani kwao kwa kulazimishwa Ili kuzuia kuendelea kuongezeka kwa ugonjwa.
3. Kwa sababu tofauti tofauti na matibabu utofautiana kwa sababu Kuna wanaopenda kupona haraka, Kuna ambao hawajali na Kuna wanaolazimishwa kutumia dawa, kwa hiyo kupona utegemea bidii ya mgonjwa kuanza matibabu na uaminifu katika matumizi ya dawa, dawa hii ikitumiwa uweza kukaa mwilini kuanzia masaa mawili mpaka masaa nane baada ya kuitumia, kwa hiyo ikitumiwa tu uenda kufanya kazi kwenye ngozi,nyama za mwili kwa kitaamu muscle na pia dawa hii inaenda kwenye ini na kweye Figo ambapo inawezekana kukaa kwa mda wa wiki tatu hivi, kwa hiyo kwa watumiaji wa dawa hii wanapaswa kunywa sana maji Ili kuweza kuondoa sumu ya dawa inayokaa kwenye ini na Figo.
4. Dawa hii inatumika na watu wenye ukoma na pia wale ambao Wana dalili za ukoma na haujajitikeza kwa kadri ya maagizo ya wataalamu wa afya na pia watu ambao hawapaswi kutumia dawa hii ni wale wenye aleji na dapson drug na pia wale ambao maudhi madogo madogo yamekuwa mengi kiasi cha kwamba hawezi kuendelea kutumia dawa hii.
5. Pia katika matumizi dawa hii huwa na maudhi madogo madogo kama vile kichefuchefu na kutapika, kuharisha mapigo ya moyo kwenda mbio, maumivu ya kichwa, mwili kukosa nguvu kukosa hamu ya kula,ikiwa maudhi haya yameongezeka zaidi ni vizuri kabisa kuwaona wataalamu wa afya na pia maudhi madogo madogo kwa wagonjwa wa ukoma ni makubwa kidogo kwa hiyo jamii inapaswa kuwa karibu na wagonjwa hawa kuepuka tabia mbaya ya kuwanyanyapaa na kuona kwamba sio binadamu , wanapaswa kutunzwa vizuri kwa sababu dawa wanazozitumia ni kali.
6. Pia kwa wale walio na matatizo ya moyo na presha wanapaswa kuwaona wataalamu wa afya kabla ya kutumia dawa Ili kuweza kupata ushauri zaidi na pia dawa hizi hazitolewi kiholela holela Bali ni kwa utaratibu wa wataalamu wa afya.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
kama unasumbuliwa na fangasi uumeni, nitakujuza dawa yake, sababu za fangasi uumeni, matibabu yake na njia za kuwaepuka
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi dawa ya phenoxy-methyl penicillin ambayo upambana na aina ya bakteria ambao utoa sumu Ili kuzuia dawa isifanye kazi.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi dawa zinazosaidis katika kutuliza magonjwa ya akili, dawa hii kwa kitaamu huiitwa chlorpromazine ni dawa ambayo utumiwa na watu wenye tatizo la magonjwa ya akili na kwa kiasi kikubwa huwa sawa.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi dawa za fangasi na matumizi yake kwa kutumia dawa ya fluconazole kama dawa mojawapo ya fangasi.
Soma Zaidi...Zipo dawa nyingi ambazo hufahamika katika kutibu fangasi kwenye mdomo ama kinywa. Miongoni mwa dawa hizo hapa nitakuletea baadhi yao. kama wewe pia unasumbuliwa na fangasi wa mdomo basi post hii itakusaidi sana.
Soma Zaidi...Zijuwe aina za minyoo na tiba yake. Dawa 5 za kutibu minyoo ya aina zote
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi dawa ya macrolide ni mojawapo ya dawa ya kutibu au kupambana na bakteria na upambana na bakteria wafuatao streptococcus pyogenes, staphylococcus aureus na haihusiki na haemophilia influenza ambao usababisha maambukizi kwenye mfumo w
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi dawa ya sulphonamide ni mojawapo ya dawa ambayo usaidia kutibu magonjwa mbalimbali yanayosababishwa na bakteria ni dawa au antibiotics ya mda mrefu na pia matumizi yake sio makubwa sana kwa sababu ya kuwepo kwa antibiotics zenye ngu
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi dawa ya streptomycin ni dawa mojawapo ya kupambana na bakteria hasa wanaoshambulia mfumo wa hewa.
Soma Zaidi...