Menu



Dawa ya Albendazole katika kutibu Minyoo.

Posti hii inahusu zaidi dawa ya Albendazole katika kutibu Minyoo, ni Aina mojawapo ya dawa ambayo usaidia kutibu Minyoo inayosababishwa na bakteria mbalimbali.

Dawa ya Albendazole Katika kutibu Minyoo.

1. Hii ni dawa ambayo imechaguliwa kutibu Minyoo katika makundi ya madawa ya kutibu Minyoo dawa hizo ni kama vile mebendazole, levamisole ,Niclosamide Thiabendazole, praziquantel  na piperazine hizi ni dawa ambazo nazo zipo kwenye kundi Moja la Albendazole ambazo utibu minyoo mbalimbali, Albendazole ufanya kazi hii kwa kuzuia kutengenezwa kwa miclotube ya wadudu au bakteria ambao ushambulia mwili wa binadamu.

 

Kwa kufanya hivyo wadudu hawa hawawezi tena kuendelea kufanya kazi Yao ya Maambukizi kwenye sehemu mbalimbali za mwili wa binadamu.

 

2.Albendazole utibu vizuri pale ambapo mgonjwa utumia dawa kabla hajala chochote kwa hiyo basi dawa hizi ni vizuri zitumiwe pale asubuhi ambapo mgonjwa anakuwa hajala kitu chocho, pia ni vizuri mgonjwa akiwa anatumia dawa hii atumie pia vyakula vyenye mafuta  ,dawa hizi huwa kwenye mfomo wa vidonge na kwa watoto wenye umri juu ya miaka miwili  dawa Yao inakuwa kwenye maji kwa hiyo wanapaswa kuitikisa kabla ya kuitumia kwa hiyo hii dawa huwa kwenye muuundo wa vidonge na kwa watoto juu ya umri wa miaka miwili huwa kwenye mfumo wa maji.

 

3. Dawa hizi za Albendazole hazitumiki kwa watoto wenye umri chini ya miaka miwili kwa sababu ambao wameitumia wanasey kuwa watoto wanapatwa sana na degedege na pia wanaweza wenye mimba hawapaswi kutumia dawa ya minyoo ya Albendazole kwa hiyo baada ya kujua madhara yanayotokea kwa watoto wenye Chini ya umri wa miaka miwili wakitumia dawa hizi tunapaswa kutoa elimu ya kutosha kwa jamii Ili kuweza kuepuka madhara makubwa ambayo yanaweza kujitokeza kwa watoto na akina Mama wenye mimba iwapo wanaotumia dawa hizi kwa hiyo inabidi waambiwe wazi dawa wanazopaswa kutumia.

 

4. Kwa wagonjwa wanaotumia dawa hizi wanaweza kupata matokea mbalimbali ambayo ufanya miili yao kutokuwa kawaida kama vile  maumivu madogo madogo ya tumbo, kichwa kuuuma, kichefuchefu, kutapika na kuharisha kwa baadhi ya wagonjwa , kizunguzungu Homa kupanda , uchovu wa mara kwa mara. Haya yakitokea kwa mgonjwa anayetumia dawa za Albendazole hasiogope Bali yataisha Ila hali ikizidi kabisa mgonjwa anapaswa kuwaona wataalamu wa afya kwa msaada zaidi.

Download app yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiw ana App yetu. Bofya liln hapo chini kuweza ku download

Download Now Bongoclass

           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu image Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Dawa Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Views 4984


Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 Madrasa kiganjani     👉5 Simulizi za Hadithi Audio     👉6 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

IJUE DAWA YA AMOXLINE (antibiotic) NA MATUMIZI YAKE
Posti hii inahusu zaidi dawa ya amoxline .jinsi inavyofanya kazi mwilini.pamoja na matumizi yake. Soma Zaidi...

Neno la awali
Asalaamu alykum warahmatullah wabarakaatuh Sifanjema zinamstahikia Allah Mola wa viumbe, muumba wa mbingu na ardhi na vilivyomo. Soma Zaidi...

Dawa ya vidonda vya tumbo
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu dawa za vidonda vya tumbo Soma Zaidi...

Dawa ya kutibu ugonjwa wa PID
PID ni mashambulizi ya bakteria kwenye mfumo wa uzazi kwa wanawake. Hapa nitakujulisha dawa Soma Zaidi...

Fahamu tiba ya jino
Post hii inahusu zaidi tiba ya jino,ni tiba ya kawaida kwa watu walio na matatizo ya meno, kwa kawaida tunafahamu kwamba jino huwa halina dawa ila dawa yake huwa ni kungoa lakini Leo nawaletea habari njema kwamba jino sio kungoa tena ila Kuna tiba ambayo Soma Zaidi...

Dawa za Anesthesia katika kutuliza maumivu.
Unapotaka kufanyiwa baadhi ya matibabu unatakiwa kupewa ganzi ama nusu kaput ili kulifanyia usihisi maumivu. Dawa hizi zinajulikana na Anesthesia. Soma Zaidi...

mtu anapo anza tumia arv kwa mara ya Kwanza inaweza mletea shda Zaid na kutetereka afya
Soma Zaidi...

Fahamu kuhusu dawa ya propranolol ambayo hutibu magonjwa ya moyo
Post hii inahusu zaidi dawa ya propranolol katika matibabu ya magonjwa ya moyo, dawa hii ipo kwenye kundi la beta blockers na ufanya Kazi mbalimbali hasa kwa wagonjwa wa moyo. Soma Zaidi...

Fahamu kuhusu dawa ya streptomycin
Post hii inahusu zaidi dawa ya streptomycin ni dawa mojawapo ya kupambana na bakteria hasa wanaoshambulia mfumo wa hewa. Soma Zaidi...

Fahamu dawa za kisukari
Post hii inahusu zaidi dawa za kisukari, kwa sababu ya kuwepo kwa ugonjwa wa kisukari vilevile kuna dawa zake ambazo utumika kurekebisha sukari kama imepanda au kushuka. Soma Zaidi...