DART somo la 3: Aina za Data
Katika somo hili utakwenda kujifunza aina za data zinazotumika kwenye Dart.
Dart ni kama lugha nyinginezo za kompyuta, karibia aina za data zinazotumuka kwenye dart ni sawa katika language nyinginezo. Aina hizo za data ni :-
- Namba
- String
- Boolean
- Lists
- Map
- Runes
- Namba ni aina za data ambazo ni namba tu.
Namaba zinaweza kuwa ni int yaani namba nzima ama double yaani namba zenye desimali.
void main(){
print(2);
print(1.5);
}
- String
Hizi ni data zilizo katika mfumo wa mchanganyiko wa herufi, namba, na alama za uandishi. String huandikwa ndani ya alama za funga na fungua semi mbili (“) ama moja (‘). Jambo la kuzingatia ni kuwa utakayoa anza nayo ndio umalizie nayo. Yaani ukitumia (“) mwanzo basi na mwisho utumie (“)
void main(){
print("bongoclass");
print('info@example.com');
print("#@?");
}
Pia unaweza kuunganisha string zaidi ya moja yaani kufanya concatnation. Kuna njia 3 ambazo hutumika kuunganisa string zaidi ya moja. Njia hizo ni kama
- Kwa kutumia alama ya kujumlisha +
- Kwa kutenganisha string mbili kwa kuacha nafasi kati yao
- Kwa kutumia interpolation yaani unaunganisha string na variable.
void main(){
//concatnation kwa kutumia +
print("karibu "+"Bongoclass");
//kwa kucha nafasi kati ya string mbili
print('karibu ' 'Bongoclass');
//kufanya interpolation
//x ni variable. Tutajifunza zaidi kwenye somo lijalo
var x = 'bongoclass';
print('karibu ${x}');
}
Kwenye string unaweza ku break line kwa kutumia back slash () ikifuatiwa na herufi n hii ni sawa na matumizi ya <br> kwenye html
void main(){
print(' karibu bongoclass upate kujifunza');
}
Kuna changamoto nyingine angalia mfano huu
void main(){
print("mama anauza ng'ombe");
}
Hapa utaona hakuna error. Ila sasa wacha tutumia single quotation mark (‘)
void main(){
print('mama anauza ng'ombe');
}
Hapo kwenye neno ng’ombe hiyo alama ya apostroph (‘) haiwezi kuendana na hizo funga semi. Hivyo kutatua tatizo hilo tutatumia back slash 2WD ().
void main(){
print('mama anauza ng'ombe');
}
...
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Simulizi za Hadithi Audio 👉2 web hosting 👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉4 Kitau cha Fiqh 👉5 Madrasa kiganjani 👉6 Tafasiri ya Riyadh Swalihina
Post zinazofanana:
DART somo la 40: factory constructor
Katika somo hiliutakwenda kujifunza aina nyingine ya constructor ambayo hutumika kwenye Dart. aina hiyo ni factory constructory.
Soma Zaidi...DART SOMO LA 16: String method zinazotumika kwneye Dart
Katika somo hili utakwenda kujfunza kuhusu String method zinazotumika kwenye Dart.
Soma Zaidi...DART somo la 17: method za namba zinazotumika kwenye dart
Katika somo hili utakwenda kuziona method za dart zinazotumika kwenye namba. pia utajifunzakuhusu math library
Soma Zaidi...DART somo la 21: Jinsi ya kutengeneza library kwenye Dart
Katika somo hili utajifunza kuhusu dart library. Pia tutakwend aktengeneza library yetu wennyewe kwa ajili ya kufanya mazoezi zaidi.
Soma Zaidi...DART somo la 15: parameter kwenye function za Dart
Katika somo hili tutakwenda kuzungumzia kuhusu parameter kwenye Dart function. Pia tutakwenda kuona mambo mengine yanayohusu function
Soma Zaidi...DART somo la 29: Dart encapsulation
Katika somo hili tutawenda kujifunza kuhusu encapsulatio kwenye Dart OOP na jinsi inavyoweza kutumika.
Soma Zaidi...