image

DART somo la 4: Jinsi ya kuandika na kutumia variable kwenye Dart

Katika somo lililopita tumejifunza kuhusu sintaksia za dart. Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kutengeneza variable kwenye Dart.

Nini maana ya variable?

Variable ni jina ambalo hutumika kuhifadhia data kwenye program. Jina la variable huitwa identifier. Kwa mfano ukisema x = 6 yaani x ni sawa na 6. Hivyo tunasema x ni variable ambayo inahifadhi 6

 

Sheria za variable:

  1. Haitakiwi kuanza na special character
  2. Haitakiwi kuanza na namba
  3. Haitakiwi kuanza na underscore
  4. Variable ni case sensitivity kwa maana unatakiwa uzingatie matumizi ya herufi ndogo na kubwa. Mfano Juma na juma ni majina mawili tofauti.

 

Jinsi ya kuandika variable:

Kwanza utaanza na jina la variable (identifier) ikifuatiwa na alama ya (=) ikifuatiwa na value ya hiyo variable. Wakati mwingine utaanza na kutaja aina ya data ikifuatiwa na jina la vaiable likifuatiwa na alama ya (=) ikifuatiwa na value

Kwenye Dart kuna njia njingi za kuandika variable kuliko baadhi ya luga nyinginezo:-

  1. Kwa kutumia keyword var
  2. Kwa kutumia dynamic
  3. Kwa kutumia const
  4. Kwa final

 

  1. Utaanza na neno  var likifuatiwa na jina la variable. Kisha utaweka alama ya = iikifuatiwa na value (thamani) ya variable. Unapotumia var  dart yenyewe itaelewa aina ya data aina ya data itakayotumika.

 

Mfano

void main(){

 var web = 'bongoclass';

 print(web);

}

Wakati mwingine kwa sababu za ki usalama utahitaji aina maalumu ya data kwenye variable yako. Hapa utataja aina ya data moja kwa moja

void main() {

String web = 'bongoclass';

print(web);

}

Kama ukiweka aina nyingine iliyo tofauti, na ambayo umeitaja itakuletea error. Angalia mfano hapo chini

import 'dart:ffi';

void main() {

Int web = 'bongoclass';

print(web);

}

Hapo kuna error kwa sababu aina ya data nilio target ni int yaani namba lakini value nilioweka ni string.

 

Pia unaweza kutengeneza variable zaidi ya moja kwenye mstari mmoja kwa kutumia aina ya data moja. Angalia mfano hapo chini variable a, b na c ni int yaani namba. Zote nimezitengeneza kwa pamoja.

void main() {

int a, b, c;

a = 5;

b = 10;

c = 2;

print(a +b +c);

}

Hapo jibu ni 17

 

Pia unaweza kubadili value ya variable kwa kuitumia tena. Ila hakikisha type ">...



Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 319


Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

DART SOMO LA 16: String method zinazotumika kwneye Dart
Katika somo hili utakwenda kujfunza kuhusu String method zinazotumika kwenye Dart. Soma Zaidi...

DART somo la 35: Enum kwenye Dart:
Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu enum na inavyotumika kwenye Dart. Soma Zaidi...

DART somo la 13: function kwenye dart
Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu function kwenye dart, jisni ya kziandika na matumizi yake. Soma Zaidi...

DART somo la 29: Dart encapsulation
Katika somo hili tutawenda kujifunza kuhusu encapsulatio kwenye Dart OOP na jinsi inavyoweza kutumika. Soma Zaidi...

DART somo la 3: Aina za Data
Katika somo hili utakwenda kujifunza aina za data zinazotumika kwenye Dart. Soma Zaidi...

DART somo la 19: method zinazotumika kwenye set data type kwenye Dart
Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu set data type pamoja na method ambazo hufanya kazi kwenye set. Soma Zaidi...

DART somo la 8: Matumizi ya switch case
Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu switch case na jinsi inavyofanya kazi kwenye Dart. Soma Zaidi...

DART somola 42: Asynchronous programming
Katika somo hili tutakwenda kujifunza concept nyingine ya asynchronous programming. Soma Zaidi...

DART somo la 11:break and continue statement kwenye Dat loop
Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu break na continue kwenye Dart loop za for loop na while loop. Soma Zaidi...

DART somo la 36: Abstract class kweye Dart
Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu abstract class na abstract method kwenye Dart. Soma Zaidi...

DART somo la 9: for loop na for in loop kwenye dart, kazi zake na jinsi ya kuadika
Katika somo hli utakwend akujifunza kuhusu loop kwenye Dart. Loop zimegawanyika katika makundi mnne ambayo ni for loop, while loop, for in loop na do while loop. Soma Zaidi...

DART somo la 5: Reserved keywords kwenye lugah ya Dart
Katika soo hili utakwenda kujifunza kuhusu reserved keywords katika Dart Soma Zaidi...