Katika somo hili utakwenda kujifunza jins ya kutengeneza constructor method, pia utajifunza matumizi yake kwenye OOP.
Constructor method ni nini?
Hii ni method ambayo hutumika kutengeneza object moja kwa moja, ama kuweka property kwenye object moja kwa moja. Constructor method haina return value. Pia jina ma construct method linatakiwa liwe sawa na jina la class husika.
Katika somo hili tutaendelea utumia kifano yetu ya somo lililopita il tupate kuelewa zaidi. Utaona tofauti ya kutumia constructor na kutokutumia.
Class gari
Kwanza tutatengeneza class gari kama tulivyoona katika somo lililopita.
class gari{
String? jina;
String? rangi;
int? matairi;
}
Baada ya hapo ndani ya class body tutatengeneza constructor method, ambayo itakuwa na jina sawa na jina la class.
class gari{
String? jina;
String? rangi;
int? matairi;
gari(){
}
}
Properties zetu tutazipitisha kama parameter kwenye constructor method.
class gari{
String? jina;
String? rangi;
int? matairi;
gari(String jina, String rangi, int matairi){
}
}
Sasa tunakwenda kutumia properties zetu kwenye construct function. Tunapotaka kutumia property ndani ya class tunatumia keyword this. Katika somo liliopita hatukutuia keyword this ila tulitumia ina la class moja kwa moja ni kwa sababu tulitumia prpperty nje ya class.
class gari {
//properties
String? jina;
String? rangi;
int? matairi;
//method
gari(String jina, String rangi, int matairi){
print(" Tunauza gari aina ya ${jina}. Ina rangi ${rangi}. Ina matairi ${matairi}.");
this.jina = jina;
this.rangi = rangi;
this.matairi = matairi;
}
}
Hatuwa iliobaki ni kutengeneza object na kuweka property. Kwa mujibu wa somo lililopita tulitakiwa tufanye hivi:-
gari toyota = gari();
toyota.jina = 'Toyota avalon';
toyota.rangi = "Nyeusi mpauko";
toyota.matairi = 4;
Ila kwa kuwa tmetumia constrct method, tutaweza kutengeneza object na kuweka value kwenye properties zake moja kwa moja kw akufanya hivi:-
gari toyota = gari( "Toyota Avalon", "nyeusi", 4);
Zingatia huo mpagilio naendana na mpangilio wa parameter kwenye construct method. Hivyo code zote zitaonekana hivi:-
class gari {
//properties
String? jina;
String? rangi;
int? matairi;
//method
gari(String jina, String rangi, int matairi){
print(" Tunauza gari aina ya ${jina}. Ina rangi ${rangi}. Ina matairi ${matairi}.");
this.jina = jina;
this.rangi = rangi;
this.matairi = matairi;
}
}
void main(){
gari toyota = gari( "Toyota Avalon", "nyeusi", 4);
}
...
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Umeionaje Makala hii.. ?
Katika somo hili utajifunza maana ya class kwenye OOP paradigm, kisha utajifunza jinsi ya kutengeneza class.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujfunza kuhusu String method zinazotumika kwenye Dart.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu namna ambavyo program inaweza kufanya maamuzi kulingana na mashart fulani.ama namna ambavyo program inaweza ku run code zaii ya mara moja kulingana na mashart. Hapa tutazingumzia flow of control statement
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu operator kwenye Dart, kazi zake na jinsi ya kuzitumia.
Soma Zaidi...Katika somo hili tutakwenda kuingia ndani zaidi kwenye somo la function. Hapa tutakwenda kuona aina za function.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kuandika data kwenye faili. Kwanza utajifunza kutengeneza folda, kisha faili na kuweka data, kisha utajifunza kufuta fali.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu switch case na jinsi inavyofanya kazi kwenye Dart.
Soma Zaidi...Katika somo hili tutakwenda kujifunza kuhusu method ambazo hutumika kwenye map data type
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza aina za data zinazotumika kwenye Dart.
Soma Zaidi...Jinsi ya kuchukuwa user input kwenye Dart kwa ajili ya kuongeza user interaction kwenye program.
Soma Zaidi...