picha

DART somo la 15: parameter kwenye function za Dart

Katika somo hili tutakwenda kuzungumzia kuhusu parameter kwenye Dart function. Pia tutakwenda kuona mambo mengine yanayohusu function

Prameter zinatakiwa zifuate utaratibu:

Unapoweka parameter unaziweka kwenye mpangilio, hivyo hata wakati wa kuweka argument unatakiwa ufuate utaratibu huo huo. Mfano kama function ina parameter 2 ya umri na jinsia, basi wakati wa kuweka argument ifuate utaratibu ho huo. Pia unatakiwa kuzingatia na aina zake za data. Kama parameter inahitaji namba wewe unaweka string hapa utasababisha error.

 

import 'dart:io';

haloo(umri, jinsia){

 print('umri wako ni miaka ${umri} na jinsia yako ni $jinsia');

}

 

void main(){

 print('Andika umri wako');

 int umri = int.parse(stdin.readLineSync()!);

 print('Andika jinsia yako');

 String jinsia = stdin.readLineSync()!;

 haloo(umri, jinsia);

}

Sasa hapo kama utachanganya mpangilio wa aprameter aina za data utaishia kupata error


 

Unaweza kuwa na default parameter

Default parameter ni parameter ambayo inakuwa umeshawekwa, hivyo mtumiaji wa program hana haja ya kujaza kitu. Kwa mfano katika program yetu ya hapo juu tunakwenda kuongeza parameter nyingine ambayo itaonyesha makazi. Tutaweka Tanzania kama default parameter

 

Ili uweze kuandika default parameter utaiweka ndani ya mabano {} utai declare kwa alama ya ( = ). Mfano {makazi = ‘Tanzania’}

 

import 'dart:io';

haloo(umri, jinsia, {makazi ='Tanzania'}){

 print(' umri wako ni miaka ${umri} na jinsia yako ni $jinsia unaishi ${makazi}');

}

 

void main(){

 print('Andika umri wako');

 int umri = int.parse(stdin.readLineSync()!);

 print('Andika jinsia yako');

 String jinsia = stdin.readLineSync()!;

 haloo(umri, jinsia);

}

 

Pia unaweza kuweka parameter ambayo sio lazima ijazwe hivyo inakuwa ni optional. Parameter hii inaweza kuwa ni default parameter. Na endapo hutakuwa na default arameter yenyewe itabeba value null kumaanisha haina kitu. Kwa mfano hapo tunataka kuongeza parameter ya kuweka jina la mkoa. Hiyo ttaifanya sio lazima ijazwe yaani option.

 

Ili kuweka optional parameter tutaiweka ndani ya mabano [] kisha utaweka aina yake ya data ikifuatiwa na alama ya ? mfano [String? mkoa]

import 'dart:io';

haloo(int umri, String jinsia, [String? mkoa]){

 print(' umri wako ni miaka ${umri} na jinsia yako ni $jinsia unaishi $mkoa');

}

 

void main(){

 print('Andika umri wako');

 int umri = int.parse(stdin.readLineSync()!);

 print('Andika jinsia yako');

 String jinsia = stdin.readLineSync()!;

 print('Andika Mkoa u">...

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 2023-11-24 Topic: DART Main: ICT File: Download PDF Views 873

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya    👉2 Kitau cha Fiqh    👉3 Madrasa kiganjani    👉4 Tafasiri ya Riyadh Swalihina    👉5 Bongolite - Game zone - Play free game    👉6 kitabu cha Simulizi   

Post zinazofanana:

DART somo la 31: inheritance kwenye DART OOP

Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu inheritance, na inavyoweza kutumika kwenye Dart OOP.

Soma Zaidi...
DART somo la 44: Jinsi ya ku install mysql kwenye program ya dart

Katika somo hili utajifunza jinsi ya kuunganisha databse na Dart. Pia utajifunza jinsi ya kuset environment kwenye kompyuta ili kuweza kutumia Dart sdk kwenye CMD.

Soma Zaidi...
DART somo la 40: factory constructor

Katika somo hiliutakwenda kujifunza aina nyingine ya constructor ambayo hutumika kwenye Dart. aina hiyo ni factory constructory.

Soma Zaidi...
DART somo la 2: syntax za dart

Katika somo hili tutatkwenda kuziona baadhi ya xyntax yaani kanunu za uandishi wa code za dart.

Soma Zaidi...
DART somo la 13: function kwenye dart

Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu function kwenye dart, jisni ya kziandika na matumizi yake.

Soma Zaidi...
DART somo la 12: Kuchukuwa user input kwenye Dart

Jinsi ya kuchukuwa user input kwenye Dart kwa ajili ya kuongeza user interaction kwenye program.

Soma Zaidi...
DART somo la 5: Reserved keywords kwenye lugah ya Dart

Katika soo hili utakwenda kujifunza kuhusu reserved keywords katika Dart

Soma Zaidi...
DART somo la 3: Aina za Data

Katika somo hili utakwenda kujifunza aina za data zinazotumika kwenye Dart.

Soma Zaidi...
DART somo la 29: Dart encapsulation

Katika somo hili tutawenda kujifunza kuhusu encapsulatio kwenye Dart OOP na jinsi inavyoweza kutumika.

Soma Zaidi...
DART somo la 11:break and continue statement kwenye Dat loop

Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu break na continue kwenye Dart loop za for loop na while loop.

Soma Zaidi...