DART somo la 19: method zinazotumika kwenye set data type kwenye Dart
Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu set data type pamoja na method ambazo hufanya kazi kwenye set.
Set zinafanan sana na list ila kuna utofauti katika matumizi, kwanza seti hutumia mabano {}, pia set data zake ni unique yaani haziakiwi kujirudia,, pia data kwenye set zinakuwa katuka aina moja ya data, huwezi kuchanganya namba na string.
Katika somo hili tutatumia string ya somo lililopita ili kufanyia mazoezi.
{'bongoclass', 'facebook', 'google', 'youtube', 'microsoft'}
Mfano
void main(){
var text1 = <String> {'bongoclass', 'facebook', 'google', 'youtube', 'microsoft'};
print(text1);
}
Hii itatupa matokeo
{bongoclass, facebook, google, youtube, microsoft}
Apo utaona kuna kitu kipya <String> hii hutumika kuonyesha aina ya data anbayo ipo kwenye set.
Methos zinazotumika:
Method zinazotumika katika set hufanana na zile ambazo tumezona kwenye list. Hapa nitakuorodheshea tu chache.
- add()
- addAll()
- elementAt()
- Contains
- remove()
- forEach
- clear()
1. elementAt() hii hutumika katika ku display item kwa kuangalia index yake. Ni sawasawa na kutumia index kama tulivyojifunza huko nyuma. Hapa nitakupa mifano miwili
void main(){
var text1 = <String> {'bongoclass', 'facebook', 'google', 'youtube', 'microsoft'};
print(text1.elementAt(3));
}
2.clear() hii hutumika kufuta item zote kwenye set husika, na ku display empty set.
void main(){
var text1 = <String> {'bongoclass', 'facebook', 'google', 'youtube', 'microsoft'};
text1.clear();
print(text1);
}
Set operation
Hapa tunakwenda kufanya matendo ya set, hizi ni hesabu maalumu ambazo hutumiwa kwenye set data type. Matendo haya ni:-
- Union
- Intesection
- substracting
Union hii huhusika na kuunganisha set mbili ili kupata set moja.
void main(){
var set1 = <String> {'bongoclass', 'facebook', 'google', 'youtube', 'microsoft'};
...Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Madrasa kiganjani 👉2 Bongolite - Game zone - Play free game 👉3 Kitau cha Fiqh 👉4 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉6 kitabu cha Simulizi
Post zinazofanana:
DART somo la 5: Reserved keywords kwenye lugah ya Dart
Katika soo hili utakwenda kujifunza kuhusu reserved keywords katika Dart
Soma Zaidi...DART somo la 17: method za namba zinazotumika kwenye dart
Katika somo hili utakwenda kuziona method za dart zinazotumika kwenye namba. pia utajifunzakuhusu math library
Soma Zaidi...DART somo la 12: Kuchukuwa user input kwenye Dart
Jinsi ya kuchukuwa user input kwenye Dart kwa ajili ya kuongeza user interaction kwenye program.
Soma Zaidi...DART somo la 44: Jinsi ya ku install mysql kwenye program ya dart
Katika somo hili utajifunza jinsi ya kuunganisha databse na Dart. Pia utajifunza jinsi ya kuset environment kwenye kompyuta ili kuweza kutumia Dart sdk kwenye CMD.
Soma Zaidi...DART somo la 33 concept ya polymorphism
Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu concept ya polymorphism.
Soma Zaidi...DART somo la 4: Jinsi ya kuandika na kutumia variable kwenye Dart
Katika somo lililopita tumejifunza kuhusu sintaksia za dart. Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kutengeneza variable kwenye Dart.
Soma Zaidi...