DART somo la 22: Jinsi ya kutumia html library kwenye Dart

Katika somo hili tutakwenda kujifunz ajinsi ya kutumia library ya html kwenye Dart. somo hili litakupeleka kujifunza jinsi ya ku display dart output kwenye faili la html.

Somo letu litakuwa katika njia mbili, ya kwanz ani ya online na ya pili ni ya offline. Kwanza tutaanza na njia ya online. Hapa tutakwenda kutumia Dart pad ambayo ni text ediroe iliyoandaliwa na waanzilishi wa Dart. editor hii ina feature zote.

 

Kwanza tutatengeneza mafaili yetu ya html, la css, na html. Kisha tutakwenda ku pest code hizo kwenye pad editor ya online.

 

Ili uweze ku run html code kwenye dart kwanza tutatakiwa ku import html . hivyo basi ingia kwenye dart pad, anza ku import dart library

import 'dart:html';

void main()

{

 

}

 

Kisha kwenye hiyo dart pad kwa juu kuna palipo andikwa html bofya hapo kisha pest code za html.

<!DOCTYPE html> 

<html> 

<head>

<title>Bongoclass</title>  

<link rel = "stylesheet" href = "styles.css">

</head>

 

<body> 

<h1 id="header"></h1>

  <p>Karibu bongoclass</p>

</body>

</html>

 

Kisha angalia palipoandikwa CSS pesa code hizo za css

body {

 

background-color: black;

 

}

 

h1 {

color: ForestGreen;

font-family: Arial, Helvetica, sans-serif;

}

 

Baada ya hapo bofya palipoandikwa run kwa juu upande wa kulia. Kama umefuata vyema maelekezo utaona upande wa kulia kuna palipoandikwa karibu bongoclass

 

Kwama unatumia simu kutakuwa na utofauti kidogo lakini maelezo hayo niliotoa yanatosheleza.

Mpaka kufikia hapo umeona faili letu la html limesoma. Sasa tunataka output za dart zionekane kwenye html. Mfano tunataka tukiprint text kwenye dart zisome kwenye html file. Kufanya hivi kwanza utatakiwa kuweka id kwenye html zako wapi unataka kuona hizo output.

 

Tuseme tunataka kuweka title mafunzo ya Dart na tunataka title hii isome kwenye <h1> tag. Hii tag itaitwa selector hivyo basi hii selector tutaiita wneye code za dart kw akutumia id  yake. Mfano <h1 id="header"></h1> hapo id ya selector yetu ni header. Rejea mafunzo yetu ya css kujifunz zaidi kuhusu selectors.

 

Unaweza kuwa na selector zaidi ya moja kwenye faili na zote zikawa na id zao. Kumbuka id haitakiwi kufanana. Pia kwenye Dart unaweza kuita selector zaidi ya moja. Sasa function inayotumika kuita hizo selector kwenye dart ni  querySelector()   ndani ya hiyo function utaweka hiyo id ya selector yako.

Mfano 

querySelector(‘#header’)

Hivyo basi tutatengeneza variable kwa ajili ya ku access hiyo selector yetu

var header = querySelector('#header');

 Kisha tutakwenda kuitumia variable yetu ili kupeleka data zetu kwenye faili la html

 header.text = "Mafunzo ya Dart";

 

Code nzima zitaonekana hivi:-

import 'dart:html';

 

void main()

{

var header = querySelector('#header');

header?.text = "Mafunzo ya Dart";

}


 


 

Unaweza kuongeza function nyingibne na hata click event. Rejea mafunzo yetu ya javascript utajifynza mengine jinsi ya kutumia id ili kucheza na html. Sasa ngoja turudi kwenye njia yetu ya offline.

 

Kwa kutumia webstorm IDE

Hii ni software kwa ajili ya kutengeneza web app. Watengenezaji wa software hii ni jetbrain. Unawez aku download free kwenye website yao ya jetbrain. Link nimetoa kwenye somo la kwanza. Rejea jinsi ya kuitumia, kwanz autatakiwa ku download dart plugin. plugin hii ni free. kisha utachaguwa Bare-bones Web App kama inavyoelekewa kwenye picha namba tatu hapo chini:-

 

Ukishafunguwa software hii tengeneza project mpya kw akuboofya palipoandikwa new project. Kwenye list chaguwa Dart  kama inavyo onueshwa kwenye picha namba 1 hapo chini. kisah weka jina la project yako kama inavo onyeshwa kwnye">...

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: DART Main: ICT File: Download PDF Views 459

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh    👉2 Simulizi za Hadithi Audio    👉3 kitabu cha Simulizi    👉4 Kitabu cha Afya    👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉6 Madrasa kiganjani   

Post zinazofanana:

DART somo la 30 :Jinsi ya kutengeneza setter na geter kwenye OOP

Katika somo hili tutakwenda kujifunza zaidi kuhusu method za getter na setter. Tutakwenda kuona hasa zinavyotumika na zinavyotengenezwa.

Soma Zaidi...
Dart somo la 25: DART OOP Nini maaan ya class na vipi utaweza kuitengeneza

Katika somo hili utajifunza maana ya class kwenye OOP paradigm, kisha utajifunza jinsi ya kutengeneza class.

Soma Zaidi...
DART somo la 44: Jinsi ya ku install mysql kwenye program ya dart

Katika somo hili utajifunza jinsi ya kuunganisha databse na Dart. Pia utajifunza jinsi ya kuset environment kwenye kompyuta ili kuweza kutumia Dart sdk kwenye CMD.

Soma Zaidi...
DART somo la 10: while loop na do while loop kwenye Dart

Katika somo hili utakwend akujifunza kuhusu while loop na do while loop zinavyofanya kazi katika Dart.

Soma Zaidi...
DART somo la 15: parameter kwenye function za Dart

Katika somo hili tutakwenda kuzungumzia kuhusu parameter kwenye Dart function. Pia tutakwenda kuona mambo mengine yanayohusu function

Soma Zaidi...
DART somo la 45: Jinai ys kutuma mysql database

Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kutumia database ya mysql kwenye Dart. hakikisha umeelewa vyema na kutekeleza yalioelekezwa kutoka kwenye somo lililopita.

Soma Zaidi...
DART somo la 40: factory constructor

Katika somo hiliutakwenda kujifunza aina nyingine ya constructor ambayo hutumika kwenye Dart. aina hiyo ni factory constructory.

Soma Zaidi...
DART - somo la 1: Kazi za dart programming na historia yake

Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu kazi za dart language. Pia nimekuandalia istoria fupi ya lugha ya DART.

Soma Zaidi...
DART somola 42: Asynchronous programming

Katika somo hili tutakwenda kujifunza concept nyingine ya asynchronous programming.

Soma Zaidi...
DART somo la 19: method zinazotumika kwenye set data type kwenye Dart

Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu set data type pamoja na method ambazo hufanya kazi kwenye set.

Soma Zaidi...