DART somo la 6: Dart operator na jinsi zinavyofanya kazi.
Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu operator kwenye Dart, kazi zake na jinsi ya kuzitumia.
Operator ni nini?
Operator hizi ni aalama ambazo hutumikakwa ajili ya kubadili value ama kufanya mahesabu mbalimbali. Ukisha elewa maana ya operator itakubidi uelewe maana ya operand. Sasa ili uelewe vyema viwili hivi nitakupa mfano:
2 + 3 = 5 katika mfano huu namda 2 na 3 ni operand na namba alama ya kujumlisha (+) ni operator. Operator zimegawanyika katika makundi mbalimbali ambayo ni
- Arithmetic operator
- Assignment operator
- Relational operator
- Type test operator
- Logical operator
- Bitwise operator
- Conditional operator
- Casecade notational operator
Katika somo hili tutakwenda kuiangalia aina moja ya operator ambayo ni arithmetic operator.
ARITHMETIC OPERATOR
Operator hizi ni zile ambazo tumezoea katika matendo ya hesabu. Ambazo ni
- Addition ( + ) Hitumika kujiumlisha mfano 10 +4 = 14
- Substruction ( - ) Hutumika kutoa mfano 10 - 4 = 6
- Divide ( / ) hutumika kugawanya mfano 10 / 5 = 2
- Multiplication ( * ) hii hutumika kuzidisha mfano 3 * 6 = 18
- Modulus ( % ) hii ni sawa na kugawanya ila badala ya kutoa jibu itatoa namba iliyobaki. Mfano 10 % 3 jibu ni 1. Hii inakupa namba iliyobaki.
- Division ( ~/) hii hutumika kugawanya ila yenyewe itakupa jibu tu pila ya kuleta desimali kama kuna kilichobaki. Mfano 10 ~/3 hapa jibu ni 3. Bila ya kuleta desiali
- Urinary minus ( -() ). Hii hutumika kubadili alama iliyopo kwenye operand. Kama ni negative inakuwa positive na kama ni positive inakuwa negative. Mfano - (10 - 4) = -6 utaona hapo jibu ni - 6 kwa kuwa tumebadli 10 kutoka positive kuwa negative. Kisha tukatoa negative 10 kutoa negative 4 jibu negative 6.
Agalia mfano hapo chini
void main() {
print(5 + 6);
print(7 - 5);
print(10 / 3);
print(10 ~/ 3);
print(10 % 3);
print(-8 - 4);
print(3 * 4);
}
URINARY OPERATOR
Hizi ni operator ambazo zinafanya kazi ya incrementon ( ++ ) na decrementation ( – - ) kwenye value. Kufanya increment ni kuongeza namba moja kwenye value. Mfano ++20 inakuwa 21. Na decrement ni kutoa namba moja kwenye value. Mfano - - 20 inakuwa 19.
Sasa kwenye Dart kuna post na pre. Unaposema post maana yake hizi alama zinakaa mbele ya value na kazi yake ni kutuma namba halisi kabla ya increment ama decrement mfano 20++ hapa itakupa jibu 20 kwa kuwa ndio namba halisi kabla ya increment. Na 10 - - itakupa jibu 10 kwa kuwa ndio namba halisi kabla ya decrement.
void main() {
var a, b, c, d;
a = 10;
b= 20;
c = 30;
d = 14;
print(a++);
print(++b);
print(c--);
print(--d);
}
ASSIGNMENT OPERATOR
Hizi ni operator ambazo hutumika kwa ajili ya kuipa variable thamani yaani value. Hapo awali tuisha jifunza alama ya ( = ) katika kuipa variable value yake. Sasa hapa tutakwend akuchanganya na operator nyingine ili kuweza ku assign value kwenye variable:-
Miongoni kwa assignment opetaror ni kama :-
- Assignment operator ( =) hiitumesha izungumzia
- Add and assign ( +=) hii kari yake ni kuongeza value operand ya kulia kwenye value ya operand y...
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Bongolite - Game zone - Play free game 👉2 ai web app 👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉4 Kitabu cha Afya 👉5 Simulizi za Hadithi Audio 👉6 web hosting
Post zinazofanana:
DART somo la 32: Inheritance kwenye construct method:
Katika masomo yaliopita tumesha jifunza jinsi inheritance inavyokuwa, ila hatujaona kwa namna gani utaweza ku inherit constructor method. Somo hili litashughulika na swla hilo.
Soma Zaidi...DART somo la 30 :Jinsi ya kutengeneza setter na geter kwenye OOP
Katika somo hili tutakwenda kujifunza zaidi kuhusu method za getter na setter. Tutakwenda kuona hasa zinavyotumika na zinavyotengenezwa.
Soma Zaidi...DART somo la 18: Dart method zinazotumika kwenye List data type
Katika somo hili utakwenda kujifunza method yhinginge zinazofanya kazi kwenye list data type kwenye Dart.
Soma Zaidi...DART somo la 27: DART OOP: maana ya constructor method na jinsi inavyotumika kwenye OOP
Katika somo hili utakwenda kujifunza jins ya kutengeneza constructor method, pia utajifunza matumizi yake kwenye OOP.
Soma Zaidi...DART somo la 23: Jinsi ya kusoma mafaili kwa kutumia Dart
Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kusoma na kuandika faili kwa kutumia Dart programming.
Soma Zaidi...DART somo la 13: function kwenye dart
Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu function kwenye dart, jisni ya kziandika na matumizi yake.
Soma Zaidi...