Kumuandaa maiti kabla ya kufa na baada ya kufa, mambo muhimu anayopasa kufanyiwa maiti wa kiislamu

3.

Kumuandaa maiti kabla ya kufa na baada ya kufa, mambo muhimu anayopasa kufanyiwa maiti wa kiislamu

3.0 MAMBO YA FARADH KWA MAITI YA MUISLAMU.

3.0 MAMBO YA FARADH KWA MAITI YA MUISLAMU.
3.1 Kuna aina Kuu mbili za Faradh.
Fardh A’in.
Ni faradh inayomlazimu kila mtu binafsi kuitekeleza, haina uwakilishi.
Mfano; kusimamisha swala, kufunga saumu, kuhiji, kutoa zaka, n.k.



Faradh Kifaya.
Ni faradh ya kuwakilishana, wachache wakitekeleza hutosheleza hitajio.
Mfano; kuswalia maiti, n.k. lakini akikosekana wa kuwakilisha, waislamu wote wanaohusika watawajibika.

3.2 Mambo ya lazima kufanyiwa maiti wa Kiislamu.
- Kila nafsi itaonja mauti (kifo). Qur’an (3:185) na (4:78).
Mambo manne yafuatayo ni lazima kufanyiwa maiti ya kiislamu:
1.Kuoshwa (Kukoshwa).
2.Kuvikwa sanda (kukafiniwa).
3.Kuswaliwa.
4.Kuzikwa.



Mambo muhimu anayofanyiwa Muislamu (mtu) anayekaribia kufa.
Mtu akikaribia kufa huwa hajiwezi kwa lolote lile pamoja na elimu, ujuzi alionao, hivyo huhitajia kufanyiwa mambo yafuatayo;
i.Kuogeshwa, kugishwa mswaki na kumpaka mafuta au manukato kama kuna uwezekano.
ii.Kumlaza kwa ubavu wa kulia au chali na kumuelekeza Qibla iwapo kuna uwezekano.
iii.Kumpa maji ya kunywa.
iv.Kutamka (kumsomea) – Shahada “Laa ilaha illallaah”
Abu Said na Abu Hurarirah wamesimulia kuwa, Mtume wa Allah amesema: “Wasomeeni watu wenu wanaokaribia kufa; ‘Laailahaillallaah”



Pia Mu’az bin Jabal amesema kuwa Mtume (s.a.w) amesema: “Yule ambaye maneno yake ya mwisho yatakuwa; “Laailahaillallaah” ataingia peponi.
(Abu Daud)
- Si lazima anayekufa aitamke kwa sauti, inaweza ikawa kimoyo moyo.



Mambo anayofanyiwa mtu (maiti) mara tu baada ya kufa.
Baada ya mtu kufa inatuwajibikia tuseme: “Innalillah wainnailaihraaji’una”. Qur’an (2:156). Kisha kumfanyia maiti mambo yafuatayo:

i.Kwa taratibu kurudishia mdomo wake usiwe wazi kwa kufunga kwa kitambaa kutoka kidevuni na kuzungushia kichwani.



ii.Kufunga macho ya marehemu na huku ukisema;
“Kwa jina la Allah na kwa kufuata mila ya Mjumbe wa Allah, Ewe Mola wetu mrahisishie mambo yake ya sasa na msahilishie mambo yake ya baadaye. Na jaalia anayokutanayo yawe bora kuliko aliyoyaacha.”



iii.Lainisha viungo vyake (miguu na mikono) kwa kukunja na kukunjua taratibu.
- Kama kuna ugumu maji ya uvuguvugu au mafuta yanaweza kutumika kulaisha na kunyoosha viungo hivyo.
- Baada ya kulainisha viungo, miguu na mikono inyooshwe na kulazwa uso ukielekezwa Qibla kwenye mkeka au kitanda kisicho na godoro.



iv.Maiti avuliwe nguo zote alizokufa nazo na kisha kufunikwa kwa shuka kubwa
- Ni vyema afunwe kitambaa tumboni au kuwekewa kitu kizito ili tumbo lisifutuke.



v.Marashi na ubani vitumike kwa wingi ili kuzima harufu ya uvundo wa maiti.


Baada ya kufanyiwa hatua hizo, sasa ni lazima maiti kufanyiwa yafuatayo:
Mambo haya ni faradh Kifaya, wakifanya wachache wanawakilisha wengine.



                   

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Fiqh Main: Dini File: Download PDF Views 2054

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Simulizi za Hadithi Audio    👉2 kitabu cha Simulizi    👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉4 Madrasa kiganjani    👉5 Bongolite - Game zone - Play free game    👉6 Kitabu cha Afya   

Post zinazofanana:

Msimamo wa Uislamu juu ya Utumwa

- Watumwa walikuwa wakikamatwa na kutezwa nguvu bila kujali utu na ubinaadamu wao.

Soma Zaidi...
maana ya uchumi kiislamu

Maana ya UchumiMfumo wa maisha wa Kiislamu humuelekeza binaadamu kujenga na kudumisha uhusiano wake na Al-lah (s.

Soma Zaidi...
Namna ya kurithisgha hatuwa kwa hatuwa.

Hspa utajifunza sasa jinsi ya kugawa mirathi kutokana na viwango maalumu.

Soma Zaidi...
Faida za kuswali swala za sunnah

Posti hii inakwenda kukufundisha kuhush swala za sunnah.

Soma Zaidi...
MAMBO YANAYOBATILISHA (HARIBU) SWALA YAKO

Lugha ya Swala Lugha ya swala,kuanzia kwenye Takbira ya kuhirimia Swala mpaka kumalizia swala kwa Salaam, ni Kiarabu.

Soma Zaidi...
Mambo ya kuzingatia kabla ya kugawa mirathi

Haya ni mamno muhimu yanayozingatiwa kabla ya kuanza zoezi la kugawa mirathi ya marehemu.

Soma Zaidi...
NI ZIPI NGUZO NA SHARTI KUU ZA SWALA ILI IKUBALIWE

Sharti za SwalaSharti za Swala Sharti za swala ni yale mambo ya lazima anayotakiwa Muislamu ayachunge na kuyatekeleza kabla hajaanza kuswali.

Soma Zaidi...