Navigation Menu



image

Ufafanuzi kuhudu mgogoro wa mwezi ni muda gani mtu aanze kufunga.

Je inapoonekana sehemu moja tufunge duania nzima ama tufunge kwa kuangalia mwandamo katika maenro tunayoishi.

Mwezi ukionekana sehemu moja, Waislamu wote ulimwenguni watalazimika kufunga?

 

Waislamu wote wanakubaliana kutokana na hadithi tulizozinukuu hapo juu, kuwa mtu mmoja au watu wachache wakishuhudia kuandama mwezi wa Ramadhani, Waislamu watalazimika kufunga. Pia waislamu wote wanakubaliana kuwa watu wa wili au zaidi wakishuhudia kuandama kwa mwezi wa Shawwal, Waislamu watalazimika kufuturu na kuswali Id dil-Fitr.

 


Hitilafu kati ya Waislamu juu ya swala la watu wachache kushuhudia kuandama mwezi wa Ramadhani au wa Shawwal ipo kwenye umbali, kwamba ni watu wa wapi wafunge watakaposikia habari za kuandama mwezi kutoka wapi? Juu ya suala hili Waislamu wamegawanyika katika makundi mawili yafu atayo:

 


Kundi la kwanza ni la wale wanaosema kuwa mwezi ukionekana katika mji mmoja au sehemu moja, basi Waislamu wengine popote walipo ulimwenguni watalazimika kufunga au kufungua. Haya pia ni maoni ya Imamu Hambali, Malik na Abu Hanifa. Hawa wamejiegemeza katika hadithi tulizozinukuu hapo juu.

 


Kundi la pili ni la wale wanaojiegemeza katika Hadithi ifuatayo: Kurayb (r.a) ameeleza kuwa Umm Fadhl, binti wa Harith alimtuma (mtoto wake) Fadhl Syria (Sham) kwa Muawiya. Fadhl aliwasili Syria na akatekeleza yale aliyotumwa na mama yake. Alipokuwa pale Syria mwezi wa Ramadhani ulianza. (Amesema Fadhl): Niliuona mwezi wa Ramadhani ulipoandama siku ya Ijumaa. Kisha nilirudi Madina mwishoni mwa mwezi. “Abdullah bin Abbas (r.a) aliniuliza juu ya kuandama kwa mwezi wa Ramadhani na akasema: Mliuona lini? Nikajibu: Tuliuona usiku wa Ijumaa. Akaniuliza; Uliona wewe mwenyewe? Nikajibu; Ndio na watu pia waliuona na walifunga na Muawiya pia alifunga, ndipo akasema; lakini sisi tuliuona usiku wa Jumamosi. Kwa hiyo tutaendelea kufunga mpaka tukamilishe 30 au tuuone mwezi Shawwal baada ya 29 Ramadhani) Nikauliza; (Fadhili): kuonekana kwa Mwezi wa Muawiya hakukutosha? Akajibu; Hapana hivi ndivyo Mtume wa Allah (s.w) alivyotuamrisha ”. (Muslim).

 


Kutokana na hadithi hii kama kuna masafa marefu kati ya mji ulipoonekana mwezi na mji watu walipopata taarifa juu ya kuonekana kwake haitajuzu kwao kufuata mwandamo huo, lakini endapo mji huo utakuwa umekaribiana basi watu waliopata taarifa ya kuandama mwezi kutoka mji wa karibu watawajibika kufunga au kufungua, mwanachuoni mashuhuri anayeshikilia rai hii ni Imamu Shafii.

 


Kutokana na hitilafu hizi, imetokea kuwa waislamu wote ulimwenguni hawaanzi kufunga Ramadhani siku moja na kuswali Iddil-Fitr na Iddil Hajj siku moja. Wale wanaoshikilia raia ya kwanza, wanaona kuwa si vyema umma mmoja wa Kiislamu kutofautiana katika matukio haya muhimu ambayo ni alama ya dini. Isitoshe kutokana na maendeleo ya sayansi, mawasiliano ulimwenguni hivi leo yamerahisika mno. Ulimwengu mzima unaweza kupata habari kwa muda wa dakika chache juu ya mwandamo wa mwezi katika mji mmoja.

 


Wale wanaoshikilia rai ya pili wanaoona kuwa si vyema kufunga au kufungua Ramadhani kwa kufuata habari ya kuandama kwa mwezi kutoka popote pale bila ya kujali masafa au machweo (matlai) kati ya mji huo na pale habari ya kuandamana mwezi ilipopokelewa. Kwani kijiografia sehemu mbali mbali za ulimwengu zinatofautiana sana. Kutokana na uchunguzi wa anga umepatikana ushahidi kuwa kuna kutofautiana katika kuona mwezi ambako katika mji mmoja kuna uwezekano mkubwa kabisa wa kuona mwezi endapo hapatakuwa na mawingu, katika mji mwingine ulio masafa ya mbali na matlai mengine, mwezi hauandami kabisa siku hiyo hata kama hapata kuwa na mawingu. Kwa hiyo hawa wenye mtazamo wa pili, pia kutokana na maendeleo hayo hayo ya kisayansi, wanaona kuwa hadithi zilizowaamrisha watu kufunga au kufungua kwa kupata habari ya kuandama mwezi kutoka kwa mtu mmoja au watu wachache, hazionyeshi kuwa wale walioleta habari za kuandama mwezi walitoka masafa marefu na pale alipokuwa Mtume (s.a.w).

 


Kutokana na rai hizi mbili, ni vema Waislamu wasigombane kwa jambo hili. Kila mtu ana uhuru wa kufuata hoja iliyomtua zaidi. Hata hivyo, lingelikuwa jambo zuri kama wanachuoni wa kila jimbo lenye uhusiano mwema kama vile Afrika ya Mashariki, wangelijadiliana na kukubaliana juu ya msimamo mmoja.

 






           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Fiqh Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1135


Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Simulizi za Hadithi Audio     👉5 Madrasa kiganjani     👉6 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

Mambo yanayoweza kutoa udhu wako
Post hii itakufundisha mambo ambayo yanabatilisha udhu. Soma Zaidi...

Aina za talaka, sharti zake na taratibu za kutaliki katika uislamu
Maana: ni utaratibu wa kuvunja mkataba wa ndoa baina ya mume na mke mbele ya mashahidi wawili kwa kuzingatia sheria ya Kiislamu. Soma Zaidi...

Tofauti ya uchumi wa kiislamu na uchumi wa kikafiri
Uchumi wa kiislamu unatofautiana sana na uchumi wa kikafiri. Hapa utajifunza tofauti hizo. Soma Zaidi...

Je inafaha kuingizwa eda na kutolewa?
Kuingizwa au Kutolewa EdaKatika sheria ya Kiislamu hapana suala Ia kuingizwa au kutolewa eda na Sheikh. Soma Zaidi...

Jinsi ya kukaa itiqaf na taratibu zake
Hapa utajifunza kuhusu taratibu za ibada ya itiqaf yaani kukaa msikitini kwa ajili ya ibada. Soma Zaidi...

Nguzo za swala.
Kipengele hiki kinaelezea nguzo mbalimbali za kuswali. Soma Zaidi...

JIFUNZE FIQH
Fahamu darsa mbalimbali za fiqh kama swala, twahara, zaka pamoja na funga. Zijuwe sharti za swala, funga na zaka. Soma Zaidi...

Hukumu na taratibu za mirathi na kurithi katika uislamu
Soma Zaidi...

Sifa za imamu wa swala ya jamaa
Post hii inakwenda kukupa sifa za imamu wa msikitini anayepasa kuswalisha swala ya jamii. Soma Zaidi...

Kuandama kwa Mwezi na Kufunga ama kufungua ramadhani, sheria na hukumu za kuangalia mwezi
Soma Zaidi...

Mambo yenye kufunguza swaumu (funga)
Soma Zaidi...

Jinsi ya kushona sanda ya maiti na kumvisha yaani kumkafini
Hapa utajifunza taratibu za kumkafini maiti wa kiislamu. Yaani kushona sanda yake na kumvisha. Soma Zaidi...