Navigation Menu



Kumkafini maiti namna ya kushona sanda ya maiti na utaratibu wa kumvisha sanda maiti

2.

Kumkafini maiti namna ya kushona sanda ya maiti na utaratibu wa kumvisha sanda maiti

Kuandaa sanda na kumvalisha maiti wa kiume na kike

2. Kumkafini (Kumvisha Sanda) Maiti.
Mazingatio juu ya Sanda.
- Ni sunnah kutumia nguo nyeupe.
‘Ibn Abbas amesimulia kuwa Mtume wa Allah (s.a.w) amesema:
“Vaeni nguo nyeupe, kwa sababu hili ni vazi lenu lililo bora kuliko yote, na wakafinini maiti wenu kwa nguo (nyeupe)”
(Abu Daud, Tirmidh na Ibn Majah)



- Pia sanda isiwe nguo ya gharama.
‘Ali (r.a) amesimulia kuwa Mtume wa Allah amesema:
“Msigharamie sana nguo za sanda, kwani inakwenda kuozeana (kaburini)”
(Abu Daud)



- Hajji akifa akiwa katika vazi la Ihram (Hija), vazi hilo ndio litakuwa sanda yake.
‘Abdullah bin Abbas amesimulia kuwa mtu mmoja alikuwa pamoja na Mtume (s.a.w) ngamia wake alimkanyaga, wakati akiwa anahiji mpaka akafa, Mtume wa Allah akasema:
“Muosheni na maji na majani ya mkunazi na mumkafini kwa hayo mashuka yake mawili, msimpake manukato na msimfunike kichwa chake …….”
(Bukhari na Muslim )



- Ukubwa wa sanda unategemeana na ukubwa wa maiti.



Sanda ya Mwanamume na namna ya kumkafini (kumvika).
- Sanda ya mwanamume ina vipande (majavi) vitatu.

1. Utaratibu wa kutayarisha sanda ya mwanamume.
i.Weka kipande cha kwanza juu ya mkeka kisha cha pili na cha tatu na vyote kushikizwa kwa uzi katikati, na kila kipande kipakwe marashi na ubani.



ii.Pasua kamba katika pembe mbili za jamvi la kwanza, moja kwa ajili ya kufungia kichwani na nyingine kwa ajili ya kufungia miguuni.
Kamba moja itachanwa kutoka jamvi la pili, ili kumfunika (kufungia) maiti katikati. Na kamba tatu zitachanwa jamvi la tatu na la pili kwa ajili ya kufungia juu ya mkeka.



iii.Maiti italazwa juu ya majavi yote matatu. Ichukuliwe pamba iwekwe manukato kisha iwekwe juu ya viungo vyote vya sijda; paji la uso, viganja vya mikono, magotini na vidole vya miguu. Pamba itumike pia kuziba tundu zote mwilini; mdomo, masikio, pua na makalio.



iv.Maiti itatizwe (ifunikwe) mwili wote, kwa kuanza kipande cha kwanza, kisha cha pili na cha tatu ukitanguliza kunjo la kushoto kisha la kulia linafuata. Zile kamba zilizochanwa zitatumika kufungia vitanzi maiti kichwani, tumboni na miguuni. Baada ya hapo maiti inaweza kuwekwa kwenye jeneza baada ya kuzungushiwa kwa mkeka tayari kwa kuswaliwa.



Sanda ya mwanamke na namna ya kumvika.
- Sanda ya mwanamke ina vipande vitano;
1. Majamvi 2
2. Shuka (Gagulo) au Underskirt 1
3. Kanzu (Blause) 1
4. Shungi (Ukaya) 1.



- Taratibu za kutayarisha sanda na kukafini:
i.Majamvi mawili yatatandikwa moja baada ya nyingine.
ii.Kikatwe kitambaa cha ukubwa wa shuka ya kujifunga kiunoni (shuka/gagulo) na iwekwe juu ya majamvi mawili ili ije kutumika kumfungia kiunoni.



iii.Kisha ikatwe kanzu (blause) isiyoshonwa vizuri kwa kukunja kitambaa na kukitoboa katikati kwa ajili ya kuingizia kichwa cha maiti (kumvalisha) na kisha kushikiza pembeni kwa uzi mfano wa kanzu kata mikono na kuwekwa juu ya gagulo sehemu ya chini (kiunoni) na itakuwa juu ya majamvi 2 sehemu ya juu (kifuani).



iv. Kitambaa (ukaya/shungi) ya kutosha kuweza kufunika kichwa na uso kitaingizwa ndani ya shingo ya kanzu na kunyooshwa kwa juu.



v.Maiti itaanza kuvalishwa kanzu, kisha kufungwa shuka (gagulo) juu yake. Kisha maiti itawekewa pamba viungo vyote vya sijda na kuziba sehemu za matundu kama ilivyokuwa kuwa kwa maiti mwanamume. Kisha maiti itatizwa (itafungwa) na majamvi mawili, moja baada ya jingine kwa kuanza kunjo la kushoto na kumalizia la kulia juu yake, na kisha kufungwa na kamba tatu juu yake- kichwani, tumboni na miguuni na kuwa tayari kuingizwa kwenye jeneza na kuswaliwa.


Sanda ya mtoto.
- Sanda ya mtoto mdogo, wa kike au kiume wasiofikia baleghe ni majamvi matatu, kama ilivyo sanda ya mwanamume.



                   

Download app yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiw ana App yetu. Bofya liln hapo chini kuweza ku download

Download Now Bongoclass

           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu image Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Fiqh Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Views 2952


Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Kitau cha Fiqh     👉5 Madrasa kiganjani     👉6 Simulizi za Hadithi Audio    

Post zifazofanana:-

Hijja na umrah
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Historia ya adhana na Iqama na jinsi ya kuadhini.
Hadithi hii inakwenda kukufundisha historia fupi ya adhana pia utakwenda kujifunza jinsi ya kuadhini na kuqimu. Soma Zaidi...

Historia ya adhana na nama ya kuadhini
Soma Zaidi...

Umuhimu na nafasi za hijjah katika uislamu
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Eda ya kufiwa na hukumu zake
Soma Zaidi...

Hili ndilo hasa lengo la kuamrishwa kufunga
Soma Zaidi...

Mambo yasiyoharibu Swaumu na Kufunguza mwenye kufunga
Soma Zaidi...

Dua ya kuzuru makaburi, na utaratibu wa kuzuru makaburi
Kuzuru makaburi ni katika matendo ya sunah yaani unapata thawabu kwa kwenda klizuru kaburi. Soma Zaidi...

Kumuandaa Maiti kabla ya kufa ama kukata roho
Soma Zaidi...

Jinsi ya kutwaharisha Aina mbalimbali za Najisi katika uislamu
Katika somo hili utakwedna kujifunza jinsi ya kutwaharisha aina mbalimbali za najisi kwa mujibu wa mafundiso ya Mtume Muhammad (s.a.w) Soma Zaidi...