Jinsi Uislamu Ulivyokomesha Biashara ya Utumwa wakati na baada ya Mtume Muhammad (s.a.w)
- Uislamu ulieneza nadharia kuwa wanaadamu wote ni sawa na wote ni watumwa mbele ya Mwenyezi Mungu (s.
Jinsi Uislamu Ulivyokomesha Biashara ya Utumwa wakati na baada ya Mtume Muhammad (s.a.w)
.Uislamu baada ya kuenea na kuongoza sehemu mbali mbali, ilikuwa ndio mwanzo wa kukomesha biashara ya utumwa na kumkomboa mwanaadamu kiutu, (kiroho), kifikra na kisaikolojia kupitia njia na sera mbali mbali kama ifuatayo:
- Uislamu ulieneza nadharia kuwa wanaadamu wote ni sawa na wote ni watumwa mbele ya Mwenyezi Mungu (s.w).
- Uislamu ulijenga uhusiano wa udugu na upendo baina ya watu bila kujali hadhi, nafasi, rangi, taifa la mtu.
- Uislamu ulisisitiza kuwa ubora wa mtu unatokana na ucha-Mungu wake na pia mtumwa au mtu huru anastahiki kuwa kiongozi na kutiiwa ipasavyo
Rejea Qur’an (49:13) na (4:25).
- Utumwa katika Uislamu ulikuwa jambo la kupita na sio taasisi ya kudumu inayojenga matabaka ndani ya jamii.
- Uislamu uliweka mikakati ya kulinda haki, utu na hadhi ya watumwa kwa kuwafanyia wema na ihsani kama wanaadamu wengine.
Rejea Qur’an (4:36) na (49:13).
- Watumwa walikuwa na haki ya kuamini na kufuata mila au dini waipendayo bila kushurutishwa.
Rejea Qur’an (2:256).
- Watumwa walikuwa wanapata huduma za kijamii kama mavazi na malazi sawa na mabwana au wanaadamu wengine.
- Mtumwa alikuwa akikosea alisamehewa badala ya kuadhibiwa, Mtume (s.a.w) alisema mtumwa asamehewe hata mara sabini kwa siku.
- Mtumwa alistahiki kuwa kiongozi na kutiiwa ipasavyo maadamu ni muislamu na Mcha-Mungu. Mtume (s.a.w) amesema “msikilizeni na mtiini kiongozi hata akiwa ni mtumwa wa kutoka uhabeshi, maadam anafuata njia ya haki”
- Uislamu unalinda hadhi ya mtumwa kwa kutomuita “Ewe mtumwa wangu” badala yake anaitwa “Ewe kijana wangu”.
- Watumwa walikuwa na haki ya kujikomboa na huru kwa njia mbali mbali zikiwemo:
1. Kulipa kiasi fulani cha pesa au mali yeyote inayokubalika.
2. Kubadilishana na mateka Waislamu waliokamatwa na maadui.
3. Kulipa fidia kwa kufanya jambo fulani lenye manufaa kwa jamii ya waislamu.
Rejea Qur’an (47:4).
- Mtume (s.a.w) na Maswahaba waliwaachia watumwa huru na kuwakomboa wengine kisha kuwaacha huru kama ifuatavyo:
1. Mtume (s.a.w) mwenyewe aliwaacha huru watumwa 63.
2. Bi Aisha (r.a) mkewe Mtume (s.a.w) aliwaacha huru watumwa 67.
3. Ibn Abbas aliwaachia huru watumwa 70.
4. Abdallah bin Umar aliwaacha huru watumwa 1,000.
5. Abdul-Rahman bin Auf alinunua watumwa 30,000 na kuwaacha huru.
Mpaka kufikia mwisho wa uongozi wa Makhalifah wa nne Waongofu, suala la Utumwa lilibakia kuwa historia katika ulimwengu wa Kiislamu.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉2 Kitabu cha Afya 👉3 Dua za Mitume na Manabii 👉4 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉5 Simulizi za Hadithi Audio 👉6 Bongolite - Game zone - Play free game
Post zinazofanana:
Milki ya raslimali katika uislamu
Milki ya RasilimaliIli kujipatia maendeleo ya kiuchumi katika zama zote mwanaadamu anahitaji rasilimali za kumwezesha kufikia azma hiyo.
Soma Zaidi...Jinsi ya kiswali swala ya haja
Post hii itakufundisha kuhusu swala ya haja na jisi ya kuiswali.
Soma Zaidi...Faida na umuhimu wa ndoa katika jamii
Hapa utajifunza faida za ndoa katika Jamii na kwa wanadamu kiafya, kiroho, kiuchumi
Soma Zaidi...