Maana ya shahada kama nguzo ya kwanza ya uislamu

4.1 Shahada.
Tafsiri na Maana ya Shahada.
- Shahada ya kwanza.
“Nashuhudia kuwa hapana Mola ila Allah”

Sifa (tabia) za mtu aliyetoa Shahada ya Kwanza Kiutendaji:
-Hatamtii yeyote katika maisha yake ya kila siku ila Allah peke yake.
-Hatamuogopa, hatamtegemea na hatamuomba yeyote ila Allah.
-Hatafuata mwongozo wowote ila ule wa Allah pekee.
-Hatamshirikisha Allah (s.w) kwa chochote kile.
-Atajipamba na sifa na tabia njema zilizoainishwa katika Qur’an na Sunnah.

- Shahada ya Pili.
“Nashuhudia kuwa Muhammad ni Mjumbe wa Allah”

Sifa (tabia) za mtu aliyetoa shahada ya Pili Kiutendaji:
- Kumtii Mtume (s.a.w) kwa kufuata aliyoagiza na kuacha aliyokataza.
- Kumuiga Mtume (s.a.w) katika mwenendo na tabia yake.
- Kumfanya Mtume (s.a.w) kuwa hakimu wa mambo yetu yote.
- Kuliendea lengo la kuletwa kwake la kuusimamisha Uislamu katika
jamii.