image

Namna ya kutoa na kuhesabu zake, masharti ya zaka na nguzo zake, nani inampasa kutoa ama kupewa zaka na sadaka

4.

Namna ya kutoa na kuhesabu zake, masharti ya zaka na nguzo zake, nani inampasa kutoa ama kupewa zaka na sadaka

Namna ya kutoa na kuhesabu zake, masharti ya zaka na nguzo zake, nani inampasa kutoa ama kupewa

4.3 Kutoa Zakat na Sadaqat.

Kilugha: Maana yake ni utakaso (purification).

Rejea Qur’an (91:9), (9:103) na (87:14).Kisheria: Maana yake ni sehemu ya mali (2.5% au 1/40) ya tajiri anayotakiwa kutoa

kuwapa wanaostahiki baada ya kufikia kiwango cha Nisaab.Nisaab: Ni kiwango (kima) akifikia au kuzaidi muislamu, analazimika kutoa zakat.

Kilugha: Neno ‘sadaqat’ linatokana na neno “sidiq” lenye maana ya ukweli.

Kisheria: Sadaqat maana yake ni mali au huduma inayotolewa kwa mtu yeyote

anayohitajia.Na.

Zakat

Sadaqat

1.

Inahusiana na utoaji wa mali tu.

Inahusiana na utoaji wa mali na huduma.

2.

Ni faradhi (amri) tu kwa tajiri muislamu aliyefikia kiwango cha Nisaab.

Ni wajibu kwa kila mtu kadri ya uwezo wake pindi inapohitajika.

3.

Zakat hutolewa kwa kiwango maalumu (2.5% au 1/40) cha mali inayojuzu kutolewa zaka.

Sadaqat haina kiwango maalumu. Kila muislamu atatoa kulingana na uwezo wake.

4.

Zakat hutolewa baada ya mwaka au mavuno.

Sadaqat haina muda maalumu wa kutoa.

5.

Zakat hustahiki kupewa Waislamu tu.

Hupewa mtu yeyote bila kujali dini au uwezo wake, bali kila anayehitajia.  1. Zakat ni nguzo ya tatu ya Uislamu.
  2. Kutoa zakat na Sadaka ni amri ya Mwenyezi Mungu (s.w).

Rejea Qur’an (14:31) na (2:254).Rejea Qur’an (9:11) na (2:2-3).

  1. Kutoa Zakat na sadaka ni sababu ya mtu kufaulu Duniani na Akhera.

Rejea Qur’an (2:2-3), (23:1-4), (22:34-45) na (2:262,274).

  1. Kutotoa Zakat na Sadaka ni sababu ya kuangamia mtu Duniani na Akhera.

Rejea Qur’an (9:34-35), (92:8-10) na (3:180).- Mali ya halali na iliyochumwa kwa njia ya halali ndio inayofaa kutolewa Zakat ua Sadaqat. Mali ya haramu au iliyochumwa kwa njia ya haramu haikubaliki.

Rejea Qur’an (4:10), (23:51) na (2:172).- Ni kutoa kile ukipendacho kwa dhati na ndio zina malipo makubwa kwa Allah.

Rejea Qur’an (2:267) na (3:92).

- Ni kutoa kwa kuzingatia kipimo (kiasi) ambacho hakiwezi kukuathiri katika matumizi ya maisha yako na familia pia.

Rejea Qur’an (2:219) na (17:29).

- Ni kutoa mali au huduma kwa ajili ya Allah pasina kujionyesha na kufuatilia kwa masimbulizi.

Rejea Qur’an (2:264), (2:271) na (2:274).

- Zakat au Sadaqat hutolewa kupewa watu maalumu wanaohitajia, wenye matatizo na zikitolewa kwa asiyestahiki, huwa ni dhuluma.

Rejea Qur’an (9:60).Kwa mujibu wa Qur’an (9:60) na (2:273), wanaostahiki kupewa Zakat ni waislamu tu katika makundi yafuatayo;

- Ni kundi la wale wasiojiweza kwa chochote cha kumudu maisha yao kabisa ya kila siku bila kusaidiwa.- Ni wale wasio na uwezo wa kupata mahitaji yao ya msingi ya kimaisha ila wana uwezo wa kujikimu kwa kiasi fulani tu.

- Ni wale wote wanaozikusanya na kuzigawanya kwa wanaohusika bila kujali uwezo wao.

  1. Wanaotiwa nguvu nyoyo zao juu ya Uislamu.

- Ni wale walioingia katika Uislamu karibuni na wanahitajika kuimarishwa imani zao juu ya Uislamu.

  1. Kuwakomboa Watumwa (Fir-riqaabu).

- Ni kuwakomboa au kuwanunua watumwa au watu wote wanaoishi chini ya miliki ya watu (mabwana) na kuwaachia huru.  1. Kuwasaidia wanaodaiwa kulipa madeni yao.

- Ni kuwalipia waislamu madeni yao waliokopa ili kujikimu kimaisha lakini bila kukusudia wameshindwa kulipa deni zao.

- Ni kutumika katika shughuli zote zinazopelekea kuhuisha na kusimamisha Uislamu katika jamii.

- Msafiri yeyote muislamu aliyeharibikiwa kwa kupoteza, kuibiwa au kuishiwa mali yake hata kama ni tajiri, ni wajibu kupewa zakat.Kwa mujibu wa Qur’an (4:36) na (51:9);

- Sadaqat hupewa wale wale wanaopewa Zakat lakini bila kiwango au muda

maalumu au kufikia nisaab.

- Sadaqat hupewa mwanaadamu yeyote hata wasiokuwa Waislamu ikiwa tu ni

mwenye kuhitajia.- Kila muislamu anao uwezo wa kutoa sadaqat, kwani inahusika na kutoa mali,

huduma, tabia nzuri, n.k.

Rejea Qur’an (2:263).- Pia haifai kurejesha sadaqat baada ya kuitoa.Rejea Hadith ya Umar (r.a); Kitabu cha 2; EDK. Uk. 80.

Rejea Jedwali lifuatalo na pia katika Kitabu cha 2; EDK, uk. 80-87.

Na.

Mali zinazojuzu kutolewa Zakat

Nisaab (Kiwango)

Kiasi (%)

Muda wa Kutoa

1.

Mazao yote ya shambani.

Wasaq 5 au kg 666(Wasaq 1 = 133.5kg)

(a) Kg 66.6 au ½ wasaq kwa mazao ya maji ya mvua.

(b) Kg 33.3 au ¼ wasaq kwa mazao yaliyomwagiliwa.

Baada ya mavuno

2.

Wanyama wafugwao kwa ajili ya chakula:

(a) Ngamia

(b) Ng’ombe

(c) Mbuzi

(d) Kondoo

(e) Kondoo au Mbuzi

Ngamia 5

Ng’ombe 30

Mbuzi 40

Kondoo 40

Kondoo au Mbuzi 40

Mbuzi 1 wa mwaka 1

Ndama 1 wa mwaka 1

Mbuzi 1 wa mwaka 1

Kondoo 1 wa mwaka 1

Kondoo au mbuzi 1 wa mwaka 1

Baada ya mwaka

3.

Dhahabu na Vito

Gram 82.5 au tola 7.5

2.5 % au 1/40 ya thamani ya mali

Baada ya mwaka

4.

Fedha na Vito

Gram 577.5 au tola 52

2.5 % au 1/40 ya thamani ya mali

Baada ya mwaka

5.

Mali ya Biashara

Sawa na thamani ya Nisaab ya Dhahabu au Fedha.

2.5 % au 1/40 ya mali

Baada ya mwaka

6.

Fedha taslimu

Sawa na mali ya Biashara

2.5 % au 1/40 ya fedha

Baada ya mwaka

7.

Mali ya kuokota au kuchimbuliwa ardhini

Haina

20 % au 1/5 ya mali

Baada ya kuokotwa na kukosa mwenyewe au baada ya kuchimbuliwa.                   

           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 795


Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-

Namna ya kutoa na kuhesabu zake, masharti ya zaka na nguzo zake, nani inampasa kutoa ama kupewa zaka na sadaka
4. Soma Zaidi...

Hadithi Ya 36: Atakayemuondoshea Shida Muislamu Mwenzake,Allah Atamuondoshea Shida Zake
Soma Zaidi...