image

Aina mbili za talaka zisizo na rejea katika uislamu

Huwezi kuruhusiwa kumrejea mke endapo utamuacha kwa talaka hizi mbili.

2.Talaka Isiyorejewa
Talaka isiyorejewa ni ile ambayo mtu hawezi tena kumrejea mkewe hata kama watasuluhishana kabla ya eda au baada ya eda. Kuna ama kuu mbili za talaka zisizorejewa:
(a)Talaka Tatu.
(b)Talaka ya Li'aan.

 


(a)Talaka tatu
Talaka tatu zinapatikana kwa kutamka dhamira ya kumuacha mke mara tatu katika kila twahara ndani ya twahara tatu za eda. Vile vile zitahesabika talaka tatu kama mume katika muda wa ndoa yao amewahi kutoa talaka rejea mbili kwa kipindi kimoja cha eda au vipindi tofauti ambapo walipatana na kurejeana. Pia kama mtu na mkewe waliwahi kuvunja ndoa mara moja kwa talaka mbili kisha mara zote hizo mbili walipatana kufunga ndoa tena watakapopeana talaka katika ndoa yao hii ya mwisho, talaka hiyo itahesabika kuwa ni talaka ya tatu.

 

Ni kinyume kabisa na sheria ya Kiislamu kutoa talaka tatu mfululizo katika kikao kimoja au katika twahara moja kwa matamshi. Wanachuoni wengi wamekubaliana kuwa talaka ya namna hiyo itahesabiwa kuwa ni talaka moja. Waislamu wanaofanya hivyo, wajue kuwa huko ni kuzifanyia mzaha aya za Mwenyezi Mungu na kuvuka mipaka ya Mwenyezi Mungu. "Na anayeruka mipaka ya Mwenyezi Mungu basi amejidhulumu nafsi yake " (65:1).

 


Uislamu umekataza vikali mchezo wa kutoa talaka tatu kwa mpigo kama tunavyojifunza katika hadithi: Mahmuud bin Labiid (r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu alieelezwa juu ya mtu aliyetoa talaka tatu mfululizo kwa mkewe. Kisha Mtume alisimama akiwa amechukizwa sana na akasema: "Unacheza na Kitabu cha Mwenyezi Mungu (s.w) nikiwa bado tupo pamoja (nikiwa bado s/afa)?" (Mtume alikasirika) kwa kiasi ambacho mtu mmoja alisimama akauliza: Je, siwezi kumuua? (Nisai)

 


Hukumu ya talaka tatu ni kwamba baada ya mume kutamka talaka ya tatu hawezi tena kumrejea mkewe katika kipindi cha eda hata kama watapatana vipi. Baada ya kipindi cha eda kwisha, mkewe atakuwa ameachika kwa talaka tatu na atakuwa huru kuolewa na mume mwingine yeyote aliyehalalishwa kwake katika sheria ya Kiislamu. Lakini ni haramu mwanamke huyo kuolewa na mumewe wa kwanza mpaka aolewe na mume mwingine. Kisha akiachika kwa mume wa pili kwa sababu za msingi au akiachwa mjane, ndipo itakuwa halali kwake kuolewa na mume wake wa kwanza. Ndoa ya namna hii inajulikana kwa jina Ia "Tahliil". Qur-an inabainisha hukumu hii katika aya ifuatayo:

 


Na kama amempa talaka (ya tatu) basi (mwanamume huyo) si halali kwake baada ya hapo mpaka aolewe na mume mwingine. Na (mwanamume huyo mwingine) akimwacha, basi hapana dhambi kwao kurejeana (kwa kuoana tena) wakiona kuwa watasimamisha mipaka ya Mwenyezi Mungu. Na hii ni mipaka ya Mwenyezi Mungu anayoibainisha kwa watu wajuao. (2:230)

 


Hukumu hii kali imetolewa iii Waislamu wasifanye mas-khara na talaka. Kuna baadhi ya Waislamu, wakikwaruzana tu kidogo na wake zao hutishia talaka au anatoa talaka kabisa. Mtu akiendelea na mchezo huu atajistukia ameshamuacha mkewe kwa talaka tatu na hana namna tena ya kumrejea. Ni katika mchezo huu wa kutoa talaka tatu bila kufikiri na kumuogopa Mwenyezi Mungu, baadhi ya Waislamu wameishia katika majuto. Baadhi ya Waislamu wanadiriki kumdanganya Mwenyezi Mungu kwa mtu kumuhonga mume mwingine amuoe mtalaka wake kwa lengo Ia kumuacha baada ya muda mfupi (na ikiwezekana asimguse) iii awe halali kuolewa na mume wake wa mwanzo. Huku ni kuzifanyia mzaha sheria za Mwenyezi Mungu na ni Haramu ya uwazi. Ndoa za namna hiyo hazisihi mbele ya Mwenyezi Mungu (s.w).

 


(b)Talaka ya Li'aan
Talaka hii hupatikana kwa viapo viwili cha mume na mke. Ikitokea kwamba mume au mke amemkamata mwenzie ugoni lakini hapana mashahidi wanne walioshuhudia kitendo hicho ila yeye mwenyewe itabidi, kama mume ndiye aliyemkamata mkewe ugoni, aape kwa kurudia mara nne kuwa anashuhudia kuwa mkewe mzinifu, kisha mara ya tano aape kwamba Iaana ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake ikiwa yeye ni miongoni mwa waongo. Mke naye ataapa mara nne kujitetea kuwa yeye hakufanya kitendo hicho kisha mara ya tano aape kuwa Iaana ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake kama mumewe ni miongoni mwa wasemao kweli. Viapo hivi vinabainishwa katika aya zifuatazo:

 

Na wale wanaowasingizia wake zao (kuwa wamezini) na hawana mashahidi ila nafsi zao, basi ushahidi wa mmoja wao utakuwa kushuhudilia mara nne kwa kiapo cha Mwenyezi Mungu ya kwamba: bila shaka yeye ni mmoja wa wanaosema kweli.

 


Na mara ya tano (aape) kwamba laana ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake ikiwa ni miongoni mwa waongo. Na (mke) itamuondokea adhabu kwa kutoa shahada mara nne kwa kiapo cha Mwenyezi Mungu ya kwamba (mume) ni miongoni mwa waongo.

 


Na mara ya tano (aape) ya kwamba hasira ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake kama (mumewe) yu miongoni mwa wanaosema kweli, (na yeye mke ndiye mwongo). (24:6-9)
Baada ya kuapizana hivi, hapo hapo ndoa itakuwa imevunjika moja kwa moja kwani wawili hawa hawategemewi tena kurejeana na kukaa kwa furaha na amani.

 





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 968


Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Madrasa kiganjani     👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    

Post zifazofanana:-

Ni yapi masharti ya Udhu na kujitwaharisha
Soma Zaidi...

Jinsi ya kutawadha hatuwa kwa hatuwa
Kutawadha ni katika ibada muhimu za mwanzo kutakiwa kuzijuwa na ni lazima. Swala yako haitaweza kutimia bila ya kujuwa udhu. Inakupasa kujuwa nguzo za udhu, yanayoharibu udhu na namna ya kutawadha kifasaha. Hapa utajifunza hatuwa za kutawadha Soma Zaidi...

Maana ya mirathi katika uislamu
Post hii itakufundishabkuhusu mirathi ya kiislamu, maana yake. Soma Zaidi...

Sifa nyingine za kuchaguwa mchumba ambazo watu wengi hawazijui
Hizi ni sifa za ziada za mchumba katika uislamu. Sifa hizi wengi hawazijui ama hawazingatii. Soma Zaidi...

sadaka
Soma Zaidi...

Fadhila za kufunga mwezi wa ramadhani
Soma Zaidi...

Nadharia ya uchumi kiislamu
1. Soma Zaidi...

TAKBIRA YA KWANZA, DUA BAADA YA TAKBIRA YA KUHIRIMIA SWALA NA KUSOMA ALHAMDU (SURAT AL-FATIHA KWENYE SWALA
2. Soma Zaidi...

Nguzo za swala.
Kipengele hiki kinaelezea nguzo mbalimbali za kuswali. Soma Zaidi...

Hii ndio hutuba ya ndoa ya kiislamu
Hapa utajifunza utaratibu wa hutuba ya ndoa ya kiislamu. Sharti za jutuba ya ndoa na jinsibya kuozesha Soma Zaidi...

Vipi utapata uchamungu kupitia funga
Vipi lengo la funga litafikiwa na kumfanya mfungaji awe mchamungu. Soma Zaidi...

Muundo wa Dola ya Kiislamu
Soma Zaidi...