image

Dalili za UKIMWI na VVU kutoka mwanzoni mwa siku za mwanzo

Je na wewe ni katika wanaosumbuka sana kujuwa dalili za kwanza za ukimwi toka siku ya kwanza, ama dalili za ukimwi kwenye ulimi, ama unatakakujuwa ni muda gani ukimwi huonekana, na je ukishiriki ngono zembe ndio utapata ukimwi? Basi makala hii ni kwa ajil

ELIMU JUU YA VVU NA UKIMWI

Ukimwi ni katika moja ya maradhi ambayo yanaweza kumuathiri mtu kimwili na kiakili. Pia inaweza kumuathiri mtu kijamii, na hii ndio maana watu wengi wamekuwa wakiogopa kupata ukimwi zaidi kuliko maradhi mengine yaliyo hatari. Ukweli ni kuwa ukimwi ni hatari kwa sababu unamuuwa mtu kidogokidogo kwa muda wa miaka mingi, lakini yapo maradhi hatari zaidi kuliko UKIMW. Makala hii itakwenda kukupa elimu juu ya maradhi haya ya ukimwi, dalili zake, tiba na kinga zake na mengineyo zaidi.

Ni nini maana ya Ukimwi?
UKIMWI ni ufupisho wa maneno “upungufu wa kinga mwilini” ni hali sugu, inayoweza kutishia maisha inayosababishwa na virusi vya Ukimwi (VVU). Kwa kuharibu mfumo wako wa kinga, VVU huingilia uwezo wa mwili wako kupambana na viumbe vinavyosababisha magonjwa. Viumbe hivyo ni kama bakteria, virusi, protozoa, fangasi na vinginevyo.


Nini maana ya Virusi Vya Ukimwi (VVU)?
VVU ni ufupisho wa maneno Virusi Vya Ukimwi, ni virusi vinavyosababisha upungufu wa kinga mwilini. Hudhoofisha mwili uwezo wake kujilinda dhidi ya vijidudu vya maradhi. Neon hili kwa lugha ya kiingereza hufupishwa kama HIV.


VVU ni maambukizo ya zinaa. Yanayoweza pia kuenezwa kwa kuongezewa damu iliyoambukizwa au kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto wakati wa ujauzito, wakati wa kujifungua au kunyonyesha. Inaweza kuchukua miaka mimngi huwenda 5 mpaka 10 kabla ya VVU kudhoofisha kinga yako ya mwili hadi kufikia ukimwi.

HATUWA ZA MAAMBUKIZO YA VVU
Hatua ya kwanza ya maambukizi (Primary infection)

Watu wengi walioambukizwa na VVU hupata ugonjwa unaofanana na Homa ndani ya mwezi mmoja au miwili baada ya virusi kuingia mwilini. Hivyo kutengeneza dalili za awali za VVU na UKIMWI. Dalili hizi si lazima zimpate kila mtu, wapp wengine hawazipati kabisa. Sana dalili hizi hutokea wiki mbili toka kupata maambukizi mpaka wiki nne kisha hupotea. Kwa baadhi ya watu zinaweza kuanzia wiki ya kwanza, na wengine kuishia wiki ya sita. Dalili hizo ni:-


1.Kupatwa na homa.
2.Maumivu ya kichwa yasiyo na sababu
3.Maumivu ya misuli
4.Kuota upele
5.Kupatwa na baridi ama kuhisi baridi.
6.Kukauka na koo ama kupatwa na vidonda kooni.
7.Kupatwa na Vidonda vya kinywa au sehemu za siri
8.Kuvimba kwa Tezi za limfu kwenye mapaja, makwapa na haswa kwenye shingo
9.Mwili kuwa na Maumivu bila ya sababu maalumu.
10.Kutokwa na Jasho la usiku
11.Kuharisha

Hatuwa ya pili Toka kuambukizwa.
Kama tulivyoona dalili za VVU katika hatuwa ya kwanza. Sasa hutokea kwa baadhi ya watu kuwa tezi za limfu zisivimbe wakati wa hatuwa ya kwanza, ila zikavimba katika hatuwa hii ya pili. Tofauti na hili hakuna dalili nyingine maalumu ya VVU katika hatuwa hii ya pili. Hatuwa hii inaweza kuchukuwa mpaka miaka 10. Kwa watu wengi ni kati ya miaka 4 mpaka 10 ila wengine mara chache hutokea ikawa chini ya hapo.

Kuendelea kwa UKIMWI
Ikiwa hautapata matibabu maalumu ya ART na kutumia ARV mapema iwezekanavyo kwa ajili ya kuthibiti maambukizo yako ya VVU, ugonjwa huendelea hadi kufikia kuwa UKIMWI kwa takriban miaka 10. Wakati huu ukiwa na UKIMWI unakua, mfumo wako wa kinga umeharibiwa sana, na hivyo kukufanya uweze kuambukizwa na magonjwa nyemelezi – Mgonjwa nyemelezi ni magonjwa ambayo hayangemsumbua mtu aliye na kinga nzuri.

SASA UKIMWI UNATOKEAJE?
Seli ndio matofali yaliyojengea miili yetu. Ndani ya miili yetu kuna aina nyingi za seli, na seli za damu. Ndani ya damu pekee kuna aina zisizopunguwa tatu za seli. Kuna seli hai nyekundu, nyeupe na seli sahani. Kila seli kati ya hizi ina kazi zake. Sasa hii seli hai nyeupe yenyewe ndio inakazi ya kupigana na vijidudu vya maradhi vinapoingia katika miili yetu. Vijidudu hivyo vinaweza kuwa bakteria, virusi ama fangasi. Seli hizi ndizo ambazo ambazo huitwa CD4.

Sasa virusi vya VVU vinapoingia mwilini vinaanza kuharibi hizi seli ambazo zinalinda mwili. Kawaida mtu anaweza kuwa na seli hizi 500 mapa 1500 katika kipimo kimoja. Sasa VVU vinaanza kuziharibu hizi na kupunguza idadi yake. Na kila seli hizi zikipunguwa ndipo mfumo wa kinga unavyoendelea kuharibika na ndivyo maradhi yanapozidi kupata nafasi ya kuingia mwilini.

Sasa endapo zimeharibiwa na kufika idadi ya 200 katika kipimo kimoja hapa mtu huyu ataambiwa ana Upungufu wa Kinga Mwilini yaani UKIMWI. Katika hatuwa hii mtu atakuwa akinyemelewa na maradhi nyemelezi kama fangasi, kifuwa kikuu, na mengineyo.

NINI CHANZO CHA VV NA UKIMWI?
Mpaka sasa chanzo halisi cha VVU bado ni mada tatizi. Ijap[okuwa wengi wanakubaliana na nadharia kuwa VVU asili yake ni masokwe, na ni huko Afrika huhusani maeneo ya Misitu ya Kongo. Yaani eti hapo zamani Waafrika wa maeneo hayo walikuwa wakiwinda masokwe kwa ajili ya kula nyama. Kumbe masokwe hayo yalikuwa na VVU. Hivyo kuingiliano huu ukapelekea watu kupata VVU. Kisha vikaanza kusafiri kutoka hapo, utandawazi na ukoloni, ukimbizi na miingiliano ya kibiahsara ilipelekea kuenea kwa kasi virusi hivi.

Dalili za VVU katika hatuwa ya kwanza
1.Homa
2.Kuhisi baridi ama kutetemeka
3.Uota upele
4.Kutokwa na jasho wakatio wa usiku
5.Maumivu ya misuli
6.Kupata vidonda vya koo, ama kuwasha kwa koo.
7.Uchovu mkali usio elezeka
8.Kuvimba kwa tezi node za lymph yaani kuvimba tezi za mtoki mapajani, kwapa na shingoni.
9.Kupata vidonda kwenye mdomo

Dalili za Ukiwmi:-
1.Kupunguwa uzito kwa haraka bila ya sababu maalumu ijulikanayo
2.Kupata homa kali za mara kwa mara na kutokwa na jasho jingi wakati wa usiku.
3.Kuchovu mkali sana usiojulikana sababu.
4.Kuendelea kuvimba kwa tezi za mtoki, kwapa na shingo
5.Kuharisha kunakoendelea zaidi ya wiki moja
6.Kutokwa na vidonda kwenye mdomo, ulimi, mkundu na sehemu za siri.
7.Kubana kwa pumzi
8.Kupoteza kumbukumbu, kukasirika mara kwa mara, ama kupoteza uwezo wa kuthibiti akili (kuchanganyikiwa)
9.Kuota mapele, majipu, mabumbuza kwenye ngozi, kope, pua na mdomoni

VIPIMO VYA VVU:
VVU vinaweza kuonekana mapema sana kulingana na aina ya vipimo. Vipo vipimo ambavyo vinaweza kugunduwa virusi mapema sana hata ndani ya wiki. Hivi hutumiaka sana maabara na si rahisi kuvipata. Hapo chini nitataja baadhi ya vipimo ambavyo hupatikana karibia maeneo mengi

Kuna aina nyingi za vipimo vya VVU. Hapa nitataja baadhi tu ya aina za vipimo hivyo:-
1. Kipimo kinachohuisisha Muunganiko wa HIV antibody na antigen. Chenyewe kinaweza tu kupima damu ya mtu. Hivi vinatumika kugunduwa antigeni ijulikanayo kama p24. antigeni p24 ni chembechembe inayozalishwa mwilini baada ya kupata maambukizi, hivyo kama itakuwepo kwenye damu inamaana mtu atakuwa ameathirika. Kipimo hiki kinaweza kugunduwa virusi mwilini kuanzia wiki 2 mpaka 6 toka kuambukizwa. Yaani kuanzia wiki 2 mpaka mweni mmoja na nusu.

2.kipimo cha HIV antibody testing. Kipimo hiki kinaweza kupimwa kwa kuchukuwa damu ya mtu ama majimajinya wili wake. Chenyewe kinapima VVU mwilini kuanzia wiki ya 3 mpaka wiki ya 12 yaani wiki tatu mapaka miezi mitatu.

3.Kipimo kuangalia viral load; huu ni upimaji wa kiasi cha virusi kwenye kipimo cha damu. Ni kuwa kama kiasi cha virusi kwenye damu yako ni kikubwa sana unaweza kuwa dhaifu kuliko ambaye kiasi chake ni kidogo.

4.Kipimo cha kuangalia drugs resistance. Hapa ni kuangalia uwezo wa mwili kama utakuwa msugu kutumia aina flani ya ART.

MATIBABU YA VVU NA UKIMWI
Kama ijulikanavyo kuwa hakuna dawa ya kutibu kabisa IKIMWI ila zipo dawa za kusaidia kuishi nyema kama kawaida bila ya kupata usumbufu wowote. Dawa hizi husuia yharibifu wa mfumo wa kinga usiendelee. Kwa ufupi matibabu haya kuzuia ukuaji na uongezekaji wa VVU mwilini. Matibabu haya hujulikana kama ART. Yaani Anti Retroviral Theraphy, na dawa zake hujulikana kama ARV yaani Anti Retroviral Virus. Dawa hizi zimegawanyika katika makundi kama:-

1.Reverse transcriptase (RT) inhibitor. Hizi huzuia virusi kujizalisha na kuongezeka.
2.Protease inhibitors. Hufanya virusi vishindwe kufanya kazi vyema.
3.Fusion inhibitors. Hivi huzuia virusi kuingia mwilini
4.Integrase inhibitors. Hizi huzuia HIV kujizalisha
5.Multidrug combination. Huu ni muunganiko wa dawa hizi zaidi ya moja.

Kushiriki ngono na mtu aliye na VVU na UKIMWI
Yes inawezekana, na hili ni swali watu wengi wamekuwa wakijiuliza. Itambulike kuwa kushiriki tendo la ndoa na aliyeathirika si lazima kuwa nawe utaathirika, ila kauli hii isieleweke vibaya. Kwani njia ambayo inaongoza leo katika kueneza maambukizi ya HIV ni kushiriki tendo la ndio. Mtu anaweza kushiriki tendo la ndoa na aliyeathirika bila ya kuathirika endapo:-

A.Endapo hakutatokea michubuko wakati wa tendo
B.Endapo muathirika ametumia dawa za ART kwa muda mrefu kwa kufuata masharti hata viral load yake ikawa haionekani (undetected) na akadumu kwa hali hii walau miezi 6
C.Endapo walitumia kinga wakati wa kushiriki tendo.

Kwa nini ni muhimu kutumia ARV?
Kwa kuwa sasa umeshajuwa kuwa usipotumia dawa unaweza kuishi zaidi ya miaka 10.sasa nikujuze faida za kutumia dawa hizi:-
1.Kuzuia uzalishaji wa virusi vya UKIMWi
2.Kuongeza umathubuti wa kinga ya mwili na kurefusha muda wa kuishi
3.Kupunguza uwezekano wa kuambukiza watu wengine.

Je naweza kufanya ngono na aliyeathirika na nisiathirike?
Ndio inawezekana kabisa kwa sababu zifuatazo:-
1.Kama umetumia kinga (kondomu)
2.Kama hakukutokea muchubuko wakati wa tendo la ndoa
3.Kama mgonjwa ametumia ARV kwa muda mrefu angalau kwa miezi 6 na kutumi na hali hiyo kwa muda zaidi hata akafikia kiasi idadi ya virusi haionekani kwenye kipimo.


Dawa ya kuzuia kuathirika kwa walio hatarini zaidi.
Kuna watu wapo hatarini sana kuathirika. Kwa mfano madaktari na wakunga, muda wowote wanaweza kuathirika. Shuikrani ziwaendee wataalamu wa dawa, wametuletea dawa inayotambulikwa kwa PrEP au kwa kirefu pre-exposure prophylaxis. Hii ji dawa inayotumika kwa dharura endapo umepatwa na mazingira hatarishi ambayo yanaweza kukupelekea kuathirika. Dawa hii inafanya kazi ndani ya masaa 72 baada ya kupata virusi. Tafiti zinaonyesha kuwa dawa hii ni bora kwa asilimia 80 inaweza kuzuia kmaambukizi ya muda mfupi.

Utaratibu wa maisha kwa aliyeathirika
1.Jilinde na maambukizi
2.Punguza misongo ya mawazo
3.Tumia kondomu wakati wa kushiriki ngono
4.Fanya mazoezi ya mara kwa mara
5.Kula mlo kamili
6.Wacha kuvuta sigara
7.Wacha ama punguza kutumia vilevi





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 34837


Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

Fangasi wa sehemu za Siri
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu fangasi wa sehemu za Siri Soma Zaidi...

Dalili za UKIMWI huonekana baada ya muda gani
Hapa utajifunza muda mabao dalili za VVU na UKIMWI huonekana, na kwa muda gani mgonjwa ataishi na UKIMWI bila ya kutumia ARV Soma Zaidi...

Dalili za kwanza za HIV na UKIMWI kuanzia wiki ya kwanza toka kuathirika
DALILI ZA HIV ZA MWANZO NA DALILI ZA UKIMWI ZA MWANZO Kama ilivyo magonjwa mengi hupitia hatua kadha kadha na kuonyesha dalili kadha katika hatua hizo. Soma Zaidi...

Madhara ya kuwepo Kwa usaha kwenye mapafu
Post hii inahusu Zaidi madhara ambayo yanaweza kutokea Kwa mgonjwa mweye usaha kwenye mapafu. Soma Zaidi...

Je utaweza kuambukiza HIV ukiwa unatumia PrEP?
Swali hili limeulizwa na mdau mmoja. Kuwa endapo mtu atafanya ngono zembe na akapata virusi je ataweza kuambukiza. Soma Zaidi...

Dalili za saratani ya kwenye Njia ya haja kubwa.
Saratani ya kwenye Njia ya haja kubwa ni aina isiyo ya kawaida ambayo kitaalamu hujulikana Kama saratani ya mkundu.Mfereji wa mkundu ni mirija fupi iliyo mwisho wa puru yako ambayo kinyesi hutoka mwilini mwako. Saratani ya kwenye Njia ya  ha Soma Zaidi...

Dalili za Dengue.
Posti hii inahusu zaidi dalili za Dengue,ni Dalili ambazo huwa kwenye makundi matatu na kuwepo kwa makundi hayautegemea kuongezeka kwa tatizo kwa sababu tatizo likiongezeka bila kutibiwa na dalili uongezeka na kufikia kwenye sehemu isiyo ya kawaida kwa mg Soma Zaidi...

SABABU ZA KUTOKEA KWA VIDONDA VYA TUMBO
SABABU ZA KUTOKEA KWA VIDONDA VYA TUMBO Sababu za kawaida za vidonda vya tumbo ni maambukizo na bakteria Helicobacter pylori (H. Soma Zaidi...

Matibabu ya vidonda vya tumbo nyumbani
Post hii inahusu zaidi matibabu ya vidonda vya tumbo nyumbani, ni njia ya kawaida ya kujitibu vidonda vya tumbo kama tulivyoona. Soma Zaidi...

Dalili za UTI kwa wanaume
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu dalili za UTI upande wa wanaume Soma Zaidi...

Fahamu Ugonjwa unaohusiana na kuzidi kwa joto mwilini (anhidrosis) ama heatshock
posti hii inazungumzia kuhusiana na Ugonjwa na Ugonjwa unaohusiana na joto ambao hujulikana Kama Anhidrosis ni kutoweza jasho kawaida. Usipotoa jasho mwili wako hauwezi kujipoza, jambo ambalo linaweza kusababisha joto kupita. wakati mwingine inaweza k Soma Zaidi...

Mtu mwenye maumivu ya tumbo upande wa kushoto anaweza kutumia tiba gani ya asili ambayo inaweza kumsaidia kupunguza maumivu?
je na wewe ni mmoja katika wenye maumivu ya tumbo upande mmoja?. Basi post hii ni kwa ajili yako. Soma Zaidi...