Makala hii inakwenda kukuletea somo linalozungumzia maumivu ya tumbo chini ya kitomvu. Ni katika maumivu amaboyo kwa wanaume mara nyingi huhusishwa an ngiri na kwa upande wa wanawake huhusishwa na chango hasa pale wanapokaribia kuingia katika siku zao. Ma
NINI HUSABABISHA MAUMIVU YA TUMBO CHINI YA KITOMVU KWA WANWAKE NA WANAUME?
Watu wengi wamekuwa wakilalamikajuu ya maumivu makali ya tumbo chini ya kitomvu. Tatizo hili linaweza kuwapata wanawake na wanaume pia. Kwa upande wa wanawake tatizo hili limekuwa ni kawaida hasa wakati wa kukaribia kuingia siku zao. Kawaida maumivu haya hayana shida sana kiafya lakini ikzidi uangalizi wa dakatari unahitajika. Je na wewe ni muhusika wa maumivu haya? Makala hii itakuwa ni jibu lako.
Maumivu ya tumbo kitomvuni
Eneo hili la kitomvuni kitaalamu hufahamika kama umblical region. Eneo hili la tumbo linahusisha viungo kama tumbo la chakula, utumbo mdogo, utumbo mkubwa na kongosho. Hivi ni katika viungo muhimu sana katika mmengenyo wa chakula, na afya ya mtu kwa ujumla.
SABABU ZA MAUMIVU YA TUMBO KITOMVUNI
1.Kuwepo na uvimbe kwenye njia ya chakula (digestive track) kitaalamu hufahamika kama gastroenteritis. Hali hii inaweza kusababishwa na virusi, bakteria ama parasite. Mgonjwa anaweza kusikia maumivu na yanaweza kuwa ni makali sana. Mara nyingi maumivu haya yanapoa yenyyewe bila hata kuhitaji matibabau ha huondoka ndani ya siku chache. Ila ni vyema kumuona daktari kwa uchunguzi zaidi.
2.Kuvimba kwa appendix. Maumivu ya tumbo kwenye kitomfu yanaweza kuashiria ugonjwa wa appendix, kitaalamu hufahamika kama appendicitis. Kama utahisi maumivu makali ya tumo kitomvuni kisha ghafla yanahamia upande wa kulia wa tumbo kwa chini, huashiria tatizo hili.
3.Vidonda vya tumbo
Yes maumivu ya tumbo kitomvuni yanaweza kuwa yamesababishwa na vidonda vya tumbo, huwenda vipo kwenye tumbo la chakula ama sehemu ya juu ya utumbo mdogo inayotambulika kama duodenum.
3.Matatizo kwenye kongosho
Huu ni ugonjwa unaosababisha kuvimba kwa kongosho kitaalamu huitwa Pancreatitis. Maradhi haya yanaweza kuja ghafla sana bila ya kuonyesha ishara za awali.
5.Kuwa na ngriri ya henia
Ugonjwa huu huwapata wanaume, na hutokea pale ambapo baadhi ya tishu za tumboni zinapoingia kwenye misuli ya tumboni karibu na kitomvu. Kwa watu wazima upasuaji hufanyika ili kutibu tatizo.
6.Kama kuna kizuizi katika utumbo kinachozuia chakula kutembea. Tatizo hili likichelewa kutibiwalinaweza kuwa hatari zaidi. Tatizo hili huweza kusababishwa na:-
1.Mashambulizi ya bakteria
2.Henia
3.Uvimbe
4.Kama kulitokea shida wakati wa kufanyiwa upasuaji.
7.Matatizo katika mishipa mikuu ya damu kwenye tumbo (aortic aneurysm). hili ni tatizo la kiafya linalosababishwa na kudhoofu na kutanuka kwa kuta za mishipa mikuu ya damu. Hali hii inaweza kuhatarisha maisha ya mtu kama mishipa ya damu itapasuka na kupelekea damu kuingia tumboni, hii inaweza kupelekea maumivu makli. Maumivu haya yanaweza kuathiri na viungo vingine.
8.Kama kutakuwa na shida wakati wa mzunguko wa damu katika tumbo (mesenteric ischemia). hii hutokea endapodamu inayotembea kwenye utumbo mdogo itapata usumbufu, kwa mfano ikiganda. Mgonjwa anaweza kusikia maumivu makali ya tumbo. Maumivu haya huandamana na dalili kama:-
1.Kuongezeka kwa mapigo ya moyo
2.Kuona damu kwenye choo
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowUmeionaje Makala hii.. ?
Jifunze dalili za gonorrhea na namna inavyoambukiza, zipi athari za gonori kwa wanawae na wanaume
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi njia mbalimbali za kuweza kupambana na fangasi za ukeni ili kuweza kujiepusha na madhara mbalimbali kwenye maisha ambayo ni pamoja na ugumba na Maambukizi kwenye via vya uzazi.
Soma Zaidi...Posti hii inazungumzia dalili na namna ya kujikinga tusipate mafua .mafua kwa jina lingine hujulikana Kama baridi ya kawaida (common cold).baridi ya kawaida husababishwa na virusi kwenye pua na hutoa makamasi.
Soma Zaidi...Posti hii inazungumzia zaidi kuhusiana na Homa ya ini yenye sumu ni kuvimba kwa ini lako kutokana na kuguswa na vitu fulani ambavyo umeathiriwa navyo. Homa ya ini yenye sumu inaweza kusababishwa na pombe, kemikali, madawa ya kulevya au virutubisho vya lis
Soma Zaidi...Dr huwa nasikia maumivu makali sana juu ya tumbo yn kama kuna moto hivi na mgongon kama unadungwa sindano hivi je hizo ni dalili za vidonda vya tumbo?
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu njia ambazo VVU huambukizwa
Soma Zaidi...Posti hii inazungumzia kuhusiana na maumivu ya shingo na ndani yake kunasababu zinazopelekea shingo kupata maumivu.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu faida za bamia mwilini
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu athari za kutokutibu fangasi
Soma Zaidi...