Posti hii inahusu zaidi madhara ya kushindwa kupitisha mkojo, ni madhara makubwa yanayotokea kwa mtu iwapo akishindwa kupitisha mkojo.
Madhara yanayoweza kutokea iwapo mtu hakutibiwa tatizo la kushindwa kupitisha mkojo.
1.Maambukizi kwenye kibofu Cha mkojo.
Tukumbuke kuwa mkojo unachujwa kutoka sehemu mbalimbali za mwili kwa hiyo mara nyingi mkojo huwa na wadudu na wadudu hao inabidi watolewe nje na wakibaki ndani wanaanza kushambulia sehemu mbalimbali za kibofu Cha mkojo na hatimaye kuleta maambukizi, kwa hiyo hali hii ya kushindwa kupitisha mkojo inabidi ishughulikiwe mara Moja kwa sababu inaweza kuleta maambukizi makubwa kwenye kibofu Cha mkojo na hatimaye kuleta maambukizi ambayo ni makubwa zaidi na hayakutarajiwa.
2. Kuharibika kwa figo.
Tunajua kazi za figo kwenye mwili wa binadamu ni kubwa mno kwa hiyo figo likiharibika matatizo mengi utokea kwenye sehemu mbalimbali za mwili wa binadamu, kwa hiyo figo likiharibika mkojo utashindwa kutengenezwa na damu utashindwa kuchuja na mwisho wake mtu asipotibiwa haraka anaweza kupoteza maisha, kwa hiyo tunapaswa kutibu tatizo hili mapema iwezekanavyo Ili kuweza kuepuka madhara makubwa zaidi ambayo yanaweza kujitokeza na tukashindwa kuyatibu kwa hiyo tutibu tatizo dogo Ili tuepuke kuwepo kwa tatizo kubwa baadae.
3. Kupungua kwa nguvu ya misuli ya kwenye kibofu Cha mkojo.
Hali hii utokea pale ambapo kibofu Cha mkojo kikijaa kinatuna na kusababisha madhara makubwa kwenye misuli ambayo nayo ulegea iwapo tatizo hili kama halijatibiwa mapema linawza kufanya kibofu Cha mkojo kulegea na hatimaye kufanya mkojo ukawa unapita bila taarifa kwa hiyo Tunapaswa kuwa makini katika kutibu ugonjwa huu maana usipotibiwa unaweza kuleta kitu kingine tofauti.
4. Kuwepo kwa UTI.
Ugonjwa wa kushindwa kupitisha mkojo kutoka kwenye kibofu unaweza kusababisha UTI kwa mgonjwa hii ni kwa sababu ya maambukizi kwenye kibofu Cha mkojo na wadudu ambao wapo ndani ya mkojo kwa hiyo tunapaswa kutibu tatizo hili iwezekanavyo Ili tuweze kuepuka na janga hili la Ugonjwa wa UTI ambao ni hatari katika maisha ya watu walio wengi.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu dalili za presha ya kushuka
Soma Zaidi...Ugonjwa wa bakteria unaoambukizwa na kupe ambao husababisha dalili kama za mafua. Dalili na ishara za Ugonjwa huu ni kati ya kuumwa na mwili kidogo hadi homa kali na kwa kawaida huonekana ndani ya wiki moja au mbili baada ya kuumwa na kupe. Njia bora ya
Soma Zaidi...Malaria husababishwa na vijidudu vidogo parasite wanaojulikana kama plasmodium. Vijidudu hivi hubebwa na mbu aina ya anophelesi. Kuna ina nyingi za plasmodium lakini aina 5 tu ndizo husababisha malaria
Soma Zaidi...Pindi malaria isipotibiwa inaweza kufanya dalili ziendelee na hatimaye kusababisha kifo.
Soma Zaidi...Kaswende ni maambukizi ya bakteria kawaida huenezwa kwa kujamiiana pia ugonjwa huu hujulikana kama syphilis. Ugonjwa huu huanza kama kidonda kisicho na maumivu kwa kawaida kwenye sehemu zako za siri, rektamu au mdomo
Soma Zaidi...Posti inahusu zaidi madhara ya kaswende kwa mama mjamzito na mtoto, Ni ugonjwa unaopatikana hasa kwa njia ya kujamiiana na utoka kwa mwenye Ugonjwa kwenda kwa mtu ambaye hana ugonjwa, kwa hiyo tunapaswa kujua madhara ya ugonjwa huu kwa mama mjamzito na mt
Soma Zaidi...Dr huwa nasikia maumivu makali sana juu ya tumbo yn kama kuna moto hivi na mgongon kama unadungwa sindano hivi je hizo ni dalili za vidonda vya tumbo?
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi ugonjwa wa Dengue, ni ugonjwa unaosababishwa na virusi ila unasambazwa na mbu kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine mbu anayasambaza Ugonjwa huu kwa kitaalamu huitwa Aedes mosquito .
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi ugonjwa wa macho, ni ugonjwa ambao ushambulia zaidi sehemu za nje za macho ambazo kwa kawaida uitwa conjunctiva na cornea hizi sehemu zikipata maambukizi zisipotibiwa mapema uweza kusababisha upofu kwa mgonjwa.
Soma Zaidi...