DALILI ZA MIMBA BAADA YA TENDO LA NDOA

Je unahitaji kujuwa kama umepata ujauzito baada ya kufanya tendo la ndoa? hakika sio rahisi ila kama utakuwa makini utaweza.

DALILI ZA UJAUZITO BAADA YA TENDO LA NDOA

Je umeshawahi kujiuliza ni zipi zinaweza kuwa dalili za kwanza za ujauzito baada ya kushiriki tendo la ndoa? Hakika hili ni swali zuri na hapa niyakujuza majibu yake. Ukweli ni kuwa ni vigumu kuona dalili za ujauzito baada ya tendo la ndoa kama hutakuwa makini. Yes inawezekana kuzijuwa ila inahitaji uangalizi wa umakini kabisa. Mwanamke mmoja alishaniambia kuwa yeye ndani ya masaa matano baada ya kufanya tendo la ndoa anaweza kujuwa kama amebeba mimba ama laa. Nilipojaribu kumuuliza alikataa kabisa kunieleza.

 

Je naweza kuziona dalili za ujauzito baada ya tendo la ndoa?

Kabla ya kulijibu swahi hili inapasa kujuwa mabadiliko ya mwili wako kabla ya ujauzito ama kabla ya kushiriki tendo la ndoa. Kwanza zingatia mabo haya kabla ya kushiriki tendo la ndoa:-

  1. Jeoto la mwili wako. Hakikisha unatambuwa vyema kama mwili wako joto lake lipo kiasi gani. Na hakikisha unaweza kutofautisha kati ya joto la homa na joto la kawaida.
  2. Zingatia majimaji ya kwenye uke wako. Zingatia kama uke wako upo katika majimaji ama upo mkavu. Pia angalia rangi za mashavu ya uke.
  3. Zingatia tarehe zako. Kabla ya kushiriki tebdo la ndoa hakikisha tarehe zako unazifahamu vyema, pamoja na siku zako za hatari ni lini.

 

Je nitazijuaje sasa hizo dalili baada ya kuzingatia mambo hayo?

Kujuwa kama umebeba mimba ama laa inaweza kuchukuwa hata wiki moja kuona mabadiliko kwenye mwili wako, mabadiliko haya yataweza kukuambia kwamba huwenda umebebe mimba. Ila pia kuna baadhi ya waanwake wanaweza kuyana mabadiliko hayo mapema kabisa. Ila tambuwa kuwa mabadiliko hayo yote yanaweza kuwa ni vyanzo vya sababu zingine na si ujauzito.

 

Mabadiliko hayo ni kama:-

  1. Kuongezeka kwa joto la mwili. Kama ulizingatia vyema joto la mwili wako wakati ukiwa katika siku za hatari linakuwa kubwa kulinganisha ziku za nyuma. Baada ya kushiriki tendo la ndoa angalia je joto litapunguwa ama kuongezeka. Kama litapunguwa baada ya kupita siku za hatari huwenda bado hujabeba ujauzito. Lakini endapo utaona joto halipungui na huwenda likaongezeka hii huonyesha kuwa una mabadiliko kwenye mwili wako ambayo huwenda ni ujauzito. Jifunze pia kutofautisha kati ya homa na joto la kawaida.

 

  1. Majimaji kwenye uke na njia ya kuelekea kwenye tumbo la mimba. Kikawaida wakati wa siku za hatari kiasi cha majimaji kwenye uke huongezeka, hii ni kwa ajili ya kuandaa mazingira ya kuweza kubeba mimba. Zinapopita siku za hatari majimaji hupunguwa na hatimaye kurudi hali ya kawaida ya ukavu. Sasa endapo majimaji hayatapunguwa na vinginevyo yakawa yanabadilika na kuwa mazito kuliko hapo mwanzo hii huashiria huwenda amebeba ujauzito.

 

  1. Ok sasa zingatia ziku zako za hatari.kama ulishiriki tendo la ndoa katika siku hatari kisha ukaanza kuona mabadiliko kama kutokwa na damu chache iliyo tofauti na hedhi, ama maumivu ya tumbo ya ghafla, ama kichwa kuhisi chepesi mabadiliko kama haya na mengineyo huashiria ujauzito.

 

  1. Mabadiliko ya rangi kwenye chuchu na mashavu ya uke yanaweza kuwa n dalili ya ujauzito. Matiti kuuma ama kuwa magumu hii ni katika dalili wanayoiona wengi katka wanawake. Mashavu ya uke hubadilika kuwa na uweuzi ama uwekundu kutokana na mishipa ya damu kuja juu na kupitisha damu kwa wingi maeneo ya chini ili kuandaa ukuaji wa mimba.

 

NI ZIPI DALILI ZA MWANZO ZA MIMBA KUANZIA SIKU YA KWANZA?

Yes kama tulivyoona hapo juu, mabadiliko hayo sio rahisi kutokea kutoka siku ya kwanza, ila yes mwili huanza kuonyehsa mabadiliko ya ndani punde tu mimba inapoingia, lakini kwa mwanamke kuhusi mabadiliko hayo inaweza kuchukuwa muda. Sasa hapa tutaziona kwa ufupi orodha ya dalili za mimba changa:

  1. Kuingezeka kwa joto la mwili
  2. Kuongezeka kwa maimaji ya ukeni
  3. Kutoka na damu kidogo nyepesi
  4. Maumivu ya matiti na kujaa ama kuwa magmu
  5. Mabadiliko ya rangi kwenye matiti na mashavu ya uke
  6. Kutoziona siku zako
  7. Kichwa kuwa chepesi
  8. Maumivu ya kichwa, tumbo na kizunguzungu
  9. Kichefuchefu na kutapika
  10. Kukojoa mara kwa mara
  11. Maumivu ya tumbo

 

JE KAMA SIO MIMBA NINI KITAKUWA.

Si kila dalili za mimba zinamaanisha ni kweli una ujauzito. Unaweza kuona dalili za mimba lakini ukawa huna. Sababu zinazoweza kupelekea hali hii ni kama:-

  1. Mabadiliko ya homoni
  2. Mashambulizi ya bakteria na virusi kwenye ufumo wa mkojo na mfumo wa uzazi
  3. Vyakula
  4. Mazingira
  5. Maradhi mengineyo yahusuyo mfumo wa uzazi

Soma zaidi kuhusu ujauzito

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: magonjwa Main: Afya File: Download PDF Views 8981

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi    👉2 web hosting    👉3 Simulizi za Hadithi Audio    👉4 Dua za Mitume na Manabii    👉5 Tafasiri ya Riyadh Swalihina    👉6 Kitabu cha Afya   

Post zinazofanana:

Madhara ya kuwepo Kwa usaha kwenye mapafu

Post hii inahusu Zaidi madhara ambayo yanaweza kutokea Kwa mgonjwa mweye usaha kwenye mapafu.

Soma Zaidi...
Homa ya Dengue, dalili za homa ya dengue na Njia ya kujikinga nayo

HOMA YA DENGUEHoma ya dengue ni miongoni mwa maradhi hatari ambayo husambazwa na mbu.

Soma Zaidi...
Fahamu ugonjwa wa kaswende wakati wa ujauzito.

Post hii inahusu zaidi ugonjwa wa kaswende wakati wa ujauzito, kaswende inaweza kukaa kwa mtu zaidi ya miaka mingi bila kuleta madhara ya moja kwa moja lakini kadiri ya siku zinavyokwenda madhara utokea hasa wakati wa ujauzito, madhara hayo umwadhiri mtot

Soma Zaidi...
Dalili za ugonjwa wa vericose veini

Posti hii inahusu zaidi dalili za ugonjwa wa vericose veini

Soma Zaidi...
Dalili za ugonjwa wa kisonono

Kisonono ni ugonjwa unaosababishwa na bakteria wa zinaa ambao wanaweza kuwaambukiza wanaume na wanawake. Kisonono mara nyingi huathiri urethra, puru au koo. Kwa wanawake, ugonjwa wa kisonono unaweza pia kuambukiza kizazi.

Soma Zaidi...
Namna ya kuzuia virusi vya ukimwi

Posti hii inaelezea kuhusiana na kujikinga au kuzuia virusi vya ukimwi.

Soma Zaidi...
Nini chanzo cha malaria

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu chanzo cha ugonjwa wa malaria

Soma Zaidi...
Dalili za ugonjwa wa UTI

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu dalili za ugonjwa wa UTI

Soma Zaidi...
Ugonjwa wa Saratani ya ini.

Saratani ya ini ni Saratani inayoanzia kwenye seli za ini lako.

Soma Zaidi...
Mie ni mwanamke ninamaumivu chini ya kitovu upande wa kushoto, na nikishika tumbo nahisi kitu kigumu upande huo huo wa kushoto... hii itakua ni nini?

Je unasumbuliwa na maumivuvya tumbo chini ya kitovu upande wa kushito. Post hii itakuletea sababu za maukivubhayo na nini ufanye.

Soma Zaidi...