dalili za mimba changa ndani ya wiki moja

dalili za mimba changa ndani ya wiki moja

Nataka kujuwa kuhusu dalili za mimba changa ndani ya wiki moja



Namba ya swali 064

Dalili za mimba ndani ya wiki moja zipo nyingi Ila utambuwe kuwa sio rahisi kuziona dalili za mimba changa ndani ya wiki moja. Kwa sababu mwili haujapata mabadiliko ya kutosha kuonyesha dalili.

Hapa nitakutajia Baadhi tu ya dalili ambazo huwenda zikaonekana mwanzoni mwa ujauzito. Huwenda zikaonekana ndani ya wiki moja ama zaidi.



Namba ya swali 064

Tafadhali nitajie dalili hizo, maana ninapata maumivu ya Tumbo toka nilipofanya tendo la ndoa.



Namba ya swali 064

Dalili za mimba changa ndani ya wiki moja ni kama zifuatazo

  1. Kutokwa na matone ya damu machache ukeni
  2. Kichwa kuuma ama kuwa chepesi siku chache toka uliposhiriki tendo la ndoa
  3. Kupatwa na kizunguzungu cha ghafla
  4. Maumivu ya tumbo kwa chini
  5. Joto la mwili kuongezeka
  6. Kuongezeka kwamajimaji ukeni
  7. Kuuma kwa matiti


Dalili nyingine za mimba changa
  1. Kukosa hedhi
  2. Kichefuchefu
  3. Kuwa na mabadiliko badiliko kwenye hisia mara unachukia hiki mara unapenda hiki
  4. Kukojoa mara kwa mara
  5. Mabadiliko ya rangi za chuchu



Namba ya swali 064

Ahsante kwa maelezo



Namba ya swali 064

karibu tena



Namba ya swali 064

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Uzazi Main: Afya File: Download PDF Views 3392

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani    👉2 Kitabu cha Afya    👉3 kitabu cha Simulizi    👉4 Tafasiri ya Riyadh Swalihina    👉5 Bongolite - Game zone - Play free game    👉6 Simulizi za Hadithi Audio   

Post zinazofanana:

Fahamu Mambo ya hatari yanayosababisha kuzaliwa kabla ya wakati (premature)

Kuzaliwa kabla ya wakati humpa mtoto muda mdogo wa kukua tumboni. Watoto waliozaliwa kabla ya wakati, hasa wale waliozaliwa mapema, mara nyingi huwa na matatizo magumu ya matibabu.

Soma Zaidi...
Sababu za Mayai kushindwa kuzalishwa kwa mwanamke

Posti hii inahusu zaidi sababu za kushindwa kuzalishwa mayai kwa mwanamke, ni tatizo ambalo utokea kwa mwanamke ambapo mwanamke anashindwa kuzalisha mayai.

Soma Zaidi...
Yajue mazoezi ya kegel

Posti inahusu zaidi mazoezi ya kegel, ni mazoezi ambayo ufanywa na watu wengi na sehemu yoyote yanaweza kufanywa kama vile chumbani, sebuleni, uwanjani na sehemu yoyote ile na kwa watu tofauti.

Soma Zaidi...
Dalili za kujifunguwa, na dalili za uchungu wa kujifunguwa

Nitajuwaje kama mjamzito amekaribia kujifunguwa, ni dalili gani anaonyesha, dalili za uchungu wa kujifunguwa

Soma Zaidi...
Kiwango cha juu cha Androgen

Posti hii inahusu zaidi homoni ya androgen, ni homoni ambayo imo kwa wanaume na ikizidi kwa kiwango chake inaweza kuleta shida kwenye mwili wa binadamu kwa hiyo homoni hii inaweza kuleta shida iwapo ikiongezeka kwa kiasi kikubwa.

Soma Zaidi...
Tabia za Ute wa siku za hatari kupata mimba au ovulation

Posti hii inahusu zaidi tabia mbalimbali za Ute wa ovulation kwa sababu Ute huu huwa tofauti na Ute mwingine kwa sababu ya kuwepo kwa tabia zake za kipekee kama tutakavyoona.

Soma Zaidi...
Madhara ya kutotoa huduma kwa Mama anayevuja damu baada ya kujifungua

Posti hii inahusu zaidi Madara ya kutomsaidia mama anayetokwa na damu nyingi baada ya kujifungua.

Soma Zaidi...
Vipimo muhimu wakati wa ujauzito

Post hii inahusu zaidi vipimo muhimu wakati wa ujauzito ni vipimo ambavyo vinapaswa kupimwa na Mama ili kuangalia mambo mbalimbali katika damu au sehemu yoyote, pia vipimo hivi umsaidia sana Mama kujua afya yake.

Soma Zaidi...
Mabadiliko kwenye tumbo la uzazi wa Mama anapobeba Mimba.

Posti hii inahusu zaidi mabadiliko kwenye tumbo la uzazi la Mama pindi anapobeba mimba, ni mabadiliko yanayotokea kwa mwanamke anapobeba mimba kama ifuatavyo.

Soma Zaidi...
Endapo nina dalili za mimba na nikipima sina mimba, je, tatizo ni nini?

dalili za mimba zinaweza kuwa na mkanganyiko kwani zinafanana na shida nyingine za kiafya. Hali hii utaigunduwa endapo utakuwa na dalili za mimba lakini kila ukipima hakuna mimba.

Soma Zaidi...