Posti hii inahusu zaidi sababu za mama kutokwa na damu nyingi baada ya kujifungua, hili ni tatizo ambalo uwapata akina Mama wengi wanapomaliza kujifungua kwa hiyo tutaweza kuziona sababu zinazosababishwa na tatizo hili.
1. Kwanza kabisa tunapaswa kujua kuwa Mama akimaliza kujifungua utokwa na damu kidogo tu na ya kawaida ila Kuna kipindi Mama anatokwa na damu nyingi sana hali inayosababisha matatizo makubwa kwa Mama kama huduma haijatolewa.kuna aina mbili za kutokwa na damu aina ya kwanza ni Ile Mama anatokwa na damu pindi tu anapomaliza kujifungua na mara nyingine Mama anatokwa na damu baada ya Masaa ishilini na manne Hadi wiki sita.
2. Sababu ya kwanza ya Mama kutokwa na damu ni pale mfuko wa kizazi unaposhindwa kisinyaa,kwa asilimia sabini wanawake wanaopatwa na tatizo hili ni kwa sababu ya mfuko wa kizazi kushindwa kisinyaa kwa sababu Ile sehemu inayokuwa imeshikikia plasenta kwa kawaida uwa na mirija inayokuwa inasafirisha chakula kwa mtoto, kwa hiyo baada ya kujifungua mfuko wa kizazi unapaswa kusinyaa Ili kuweza kufunika Ile sehemu ya mishipa ya damu isiendelee kutoa damu, kwa hiyo mfuko wa uzazi usipofunga Ile mishipa uendelea kutoa damu hali inayosababisha kuendelea kuvuja kwa damu nyingi baada ya kujifungua.
3. Kubakizwa baadhi ya vipande vya plasenta au kondo la nyuma kwenye mfuko wa kizazi.
Kwa kawaida tunafahamu kuwa baada ya mtoto kutoka kifuatacho ni kondo la nyuma, na kondo hilo huwa Lina visehemu vyake ambavyo kwa lugha ya kitaalamu huitwa lobe, kwa kawaida hizo lobe uanzia kumi na Saba mpaka ishilini na ikitokea wakati mama anajifungua akabaki sehemu yoyote ya lobe usababisha Mama kutoa damu nyingi baada ya kujifungua. Kwa hiyo ni vizuri kabisa kuziangalia hizo lobe na kuzitoa vizuri Ili kuepukana kuvuja kwa damu.
4. Pengine Mama anakuwa na kovu kwenye sehemu yoyote ya mfuko wa kizazi, au pengine anakuwa amepasuka kwa ndani, hasa hasa akina Mama wanapojifungua kwa mara ya kwanza wanakuwa wamepasuka kwa sababu njia bado ni ndogo, kwa hiyo ni vizuri kabisa kuangalia sehemu iliyochanika na kuishona Ili kuweza kuepuka tatizo la kuvuja kwa damu baada ya kujifungua. Au pengine akina Mama wanakunywa dawa za kuongeza uchungu hali inayosababisha kuwepo kwa uchungu mwingi na njia bado inakuwa imefungwa kwa hiyo Mama ulazimisha kusukuma na kusababisha kuchanika sana sehemu za Siri na kusababisha damu kuvuja sana
5. Tatizo la damu kushindwa kuganda.
Kama tulivyotangulia kusema kwamba, mtoto anapokuwa tumboni upata chakula chake kupitia kondo la nyuma na kondo hilo huwa Lina mirija ya damu na pindi mtoto akizaliwa kondo la nyuma nalo utoka, lakini sehemu ya kondo la nyuma lilipotoka Kuna mishipa ya damu uendelea kutoa damu, Ili mishipa hiyo iache kutoa damu ni lazima mfuko wa kizazi kusinyaa na kufunika sehemu hiyo na pengine kunapaswa kuwepo na vitu vinavyosababisha damu kuganda kwa hiyo Kuna wanawake wengine hawana madini ya kusababisha damu kuganda hali inayosababisha damu kuendelea kutoka kwa wingi.
6. Kwa hiyo akina Mama wanapaswa kujua kwamba tatizo hili la kutokwa na damu nyingi baada ya kujifungua ni hatari na kama hakuna uangalizi mzuri Mama anaweza kupoteza maisha, kwa hiyo ni wito wangu kwamba akina Mama wote wanapaswa kujifungua hospital Ili kama Kuna matatizo kama haya ni vizuri kudili nayo hospital kuliko vijijini, kwa hiyo jamii inapaswa kutoa elimu kuhusu jambo hili Ili wote kwa ujumla tuweze kutokomeza vifo vya akina Mama pindi wanapojifungua.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Posti hii inahusu zaidi njia mbalimbali za kuzuia Malaria kwa wajawazito na watoto wao wakiwa bado tumboni, tunajuwa wazi kuwa wajawazito wakipata Malaria inaweza kupelekea mimba kutoka kwa hiyo ili kuzuia tatizo hili zifuatazo ni njia zilizowekwa ili kuz
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi madhara ya kutumia madawa ya kupunguza maumivu,ni madhara ambayo utokea kwa mtu anayetumia madawa ya kupunguza maumivu.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi msaada au namna ya kuwahudumia wale wasioona hedhi na wamefikiwa kwenye umri wa kuweza kuona hedhi.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi mabadiliko kwenye uke wa Mama pale anapobeba tu mimba, Mama anapobeba mimba Kuna mabadiliko Katika uke wa Mama kama ifuayavyo.
Soma Zaidi...Zijuwe dalili 17 za mimba na mimba changa, kuanzia siku ya kwanza mpaka mwezi mmoja
Soma Zaidi...inaweza kutokea kuwa mtoto aliye tumboni akaishiwa maji hata kabla ya kuzaliwa. yes hali hii huweza kuwapata baadhiya watoto.
Soma Zaidi...Mwanaume na mwanamke wanapo kutana na kujamiina kama mwanamke yupo kwenye ferlile process ni rahisi kupata mbimba. Sparm Zaid ya million moja huingia kwenye mfuko wa lakin sparm moja ndio huweza kuingia kwenye ovum(yai)lakin nyingine hubaki kwenye follopi
Soma Zaidi...Matatizo yahusianayo na nguvu za kume na kukosa hamu ya tendo la ndoa kwahuweza kuchangiwa sana na mpangilio mbovu wa vyakula pamoja na saikolojia ya mtu.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi mambo ya kuzingatia kwa Mama mwenye mimba, ni kipindi ambacho Mama uhitahi uangalizi wa karibu zaidi.
Soma Zaidi...