Jinsi ya kupata mtoto wa kiume
Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu nadharia ya kupata mtoto wa kiume.
Habari,
Nashukuru kwa kuelewa jinsi ya kukokotoa siku na kupata siku za kutungwa mimba. Mimi siku zangu hubadilika mara kwa mara, lakini mara nyingi huwa siku 31 au 32. Shida yangu ni kupata mtoto wa kiume, nifanyeje katika hilo?
Jibu
Kwanza kabisa, ni vizuri kujua kuwa kupata mtoto wa kiume au wa kike hakuna njia yenye uhakika wa kitaalamu. Kuna nadharia nyingi ambazo watu huzitumia na wengine hudai zimewasaidia, lakini hakuna uthibitisho wa asilimia 100. Hata hivyo, wacha nikuchagulie baadhi ya nadharia maarufu:
1. Lishe yenye kalori nyingi
Baadhi ya tafiti zimeonyesha kuwa mwanamke anayekula chakula chenye kalori nyingi ana nafasi kubwa ya kupata mtoto wa kiume.
Kalori ni kipimo cha nishati kinachopatikana kwenye chakula. Vyakula vyenye kalori nyingi ni pamoja na vyakula vya wanga (wali, viazi, mikate), vyenye mafuta (karanga, mbegu, parachichi, samli, siagi) na nyama.
Pia inashauriwa kula vyakula vyenye madini ya potasiamu kama ndizi, na kutumia chumvi ya kawaida kwa kiasi.
Sababu: Chumvi na vyakula vya potasiamu husaidia kufanya mazingira ya uke na mji wa mimba yawe na asili ya alkali. Hali hii husaidia mbegu za kiume kuishi muda mrefu zaidi.
2. Kufika kileleni mapema
Tafiti fulani zinasema kuwa mwanamke akiwahi kufika kileleni kabla ya mume, huongeza uwezekano wa kupata mtoto wa kiume. Hii ni kwa sababu mbegu za kiume husafiri kwa kasi zaidi kuliko mbegu za kike.
3. Mkao baada ya tendo
Wengine huamini kuwa baada ya tendo la ndoa, mwanamke akilala ubavu wa kulia husaidia mbegu za kiume kufika kwa haraka zaidi kwenye yai.
4. Mbinu za mikao ya tendo la ndoa
Kuna wanaoamini kuwa mikao fulani, kama ule wa “kifo cha mende” (doggy style), husaidia kwa sababu uume unakaribia zaidi kwenye mlango wa kizazi, na hivyo mbegu za kiume kufika haraka.
Hitimisho
Hizi zote ni nadharia tu, si njia za kitaalamu zenye uhakika. Watu wengine hudai zimewasaidia, lakini mara nyingi inaweza kuwa ni kwa bahati tu.
Kwa ushauri wa kibinafsi, unaweza kujaribu ile ya kwanza (lishe yenye kalori nyingi na vyakula vyenye potasiamu), ila usitumie chumvi nyingi kupita kiasi kwani inaweza kuathiri afya.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 ai web app 👉2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉3 web hosting 👉4 kitabu cha Simulizi 👉5 Dua za Mitume na Manabii 👉6 Bongolite - Game zone - Play free game
Post zinazofanana:
Nna mimba ya miez miezi mitano 5 naruhusiwa kula papai kwa wing
Miongoni mwa matunda yenye virutubisho vingi ni pamoja na papai, nanasi, tikiti, palachichi, pera, karoti, hindi na boga. Lakini katika matunda haya yapo ambayo kwa mimba changa anatakiwa awe makini, kama papai na nanasi. Sasa vipi kuhusu mimba ya
Soma Zaidi...Dalili ya mimba ya wiki moja(1)
Mwanaume na mwanamke wanapo kutana na kujamiina kama mwanamke yupo kwenye ferlile process ni rahisi kupata mbimba. Sparm Zaid ya million moja huingia kwenye mfuko wa lakin sparm moja ndio huweza kuingia kwenye ovum(yai)lakin nyingine hubaki kwenye follopi
Soma Zaidi...dalili za mimba changa na siku ya kupata mimba
Jifunze namna ya kuthibitisha dalili za ujauzito kuwa ni za kweli. Tambuwa namna ya kupima mimba na muda mujarabu wa kupima
Soma Zaidi...Fahamu kuhusu fangasi za ukeni
Posti hii inahusu zaidi fangasi za ukeni, hili ni tatizo kubwa ambalo linawakumba watoto, akina dada na wanawake kwa hiyo na vizuri kujua Dalili zake na kuweza kuchukua hatua mapema.
Soma Zaidi...