picha

Tiba ya awali kwa mwanamke mwenye changamoto ya PID

Posti hii inahusu zaidi tiba ya awali kwa mwanamke mwenye changamoto ya PID, tunaita tiba ya awali kwa sababu baada ya kupima na kugunduliwa kwamba una tatizo au changamoto ya PID ni vizuri kutumia tiba hiii baadae ndipo utumie dawa.

Tiba ya awali kwa mwanamke mwenye changamoto ya PID.

1. Kwanza kabisa napaswa kusisitiza kwamba hii tiba sio kwamba ni dawa ya kuponyesha bali ni maandalizi ya kutumia dawa ya PID kwa hiyo unapopatwa na tatizo la PID unapaswa kutumia tiba hii ndipo baadae unaweza kuendelea na dawa ulizoagizwa kufanya.

 

2. Unapaswa kuandaa tangawizi vipande vitatu na unaviosha vizuri kabisa ili kuondoa uchafu na wadudu wengine pia unazikuna kama hauna kikunio unaweza kuzitwanga na ziwe kama mfano wa unga hivi .

 

3. Baada ya kupata tangawizi zilizotwangwa unaandaa kitunguu swaumu punje kama kumi na tano hivi nazo uzitwange ziwe laini kama ilivyofanya kwa tangawizi .

 

4. Baada ya maandalizi ya vitunguu saumu andaa vitunguu maji vikate Kaye kwa vipande vidogo vidogo na hakikisha vimeoshwa kwa maji na kutakata vizuri.

 

5. Baada ya maandalizi ya tangawizi, kitunguu swaumu na vitunguu maji changanya vyote kwa ujumla weka maji ya moto na pia unaweza kuweka maji ya baridi , weka kiasi cha lita moja funika vizuri acha ikae kwa masaa sita baada ya hapo chuja vizuri unaweza kutunza kwenye jagi au kifaa chochote kile.

 

6. Tumia hayo maji kwenye glasi changanya na asali mbichi vijiko viwili tumia glasi moja asubuhi,moja mchana na nyingine jioni kwa mda wa siku moja baada ya hapo mwili utakuwa tayari umeuandaa vizuri kwa ajili ya kutumia dawa.

 

7. Pia tiba hii isitumiwe mara kwa mara na watu wenye matatizo ya vidonda vya tumbo kwa sababu ya kuwepo kwa kiwango kikubwa cha asidi.

 

8. Na kama nilivyotangulia kusema hii tiba sio kwa sababu ya kutibu PID bali ni kwa sababu ya maandalizi ya kuanza kutumia dawa za PID kwa hiyo ukitumia mchanganyiko huu unakusudia na kukupa maandalizi mazuri ya kutumia dawa za PID

 

 

 

 

 

 

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 2022/07/12/Tuesday - 02:44:25 pm Topic: Uzazi Main: Afya File: Download PDF Views 9925

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Dua za Mitume na Manabii    👉2 Kitau cha Fiqh    👉3 Kitabu cha Afya    👉4 Simulizi za Hadithi Audio    👉5 web hosting    👉6 Bongolite - Game zone - Play free game   

Post zinazofanana:

Je inaweza ukaingia period wakati unaujauzito?

Ukiwa mjamzito unaweza kushuhudia kutokwa na damu. Je damu hii ni ya hedhi?

Soma Zaidi...
Utaratibu wa chakula kwa Mama mjamzito.

Post huu inahusu zaidi utaratibu wa chakula kwa Mama mjamzito, ni chakula anachopaswa kutumia na ambavyo hapaswi kutumia kwa Mama mjamzito mzito, kwa sababu Mama mjamzito anapaswa kuwa makini katika matumizi ya chakula ili kuweza kuongeza vitu muhimu mwil

Soma Zaidi...
Dalili za mimba kuanzia siku 7 Hadi 14

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu dalili za mimba kuanzia siku ya 7 Hadi ya 14

Soma Zaidi...
Je siku sahihi yakufanya tendo la ndoa niipi ukipata siku zake za hatari?

Swali langu ni hili doktaJe siku sahihi yakufanya tendo la ndoa niipi ukipata siku zake za hatari?

Soma Zaidi...
Dalili za hatari kwa mama aliyejifungua.

Posti hii inaelezea kiufupi kabisa kuhusiana na Dalili za hatari kwa mama aliyejifungua.

Soma Zaidi...
Umuhimu wa maji yaliyomo kwenye mfuko wa mtoto akiwa tumboni mwa mama

Post hii inahusu zaidi umuhimu wa maji yaliyomo kwenye mfuko wa mtoto akiwa tumboni. Ni maji ambayo kwa kitaalamu huitwa (Amniotic fluid)

Soma Zaidi...
Sababu za kutoka kwa mimba na dalili zake

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu sababu za kutoka kwa mimba na dalili zake

Soma Zaidi...
Huduma kwa wasioona hedhi

Posti hii inahusu zaidi msaada au namna ya kuwahudumia wale wasioona hedhi na wamefikiwa kwenye umri wa kuweza kuona hedhi.

Soma Zaidi...
Njia za kuzuia Malaria kwa wajawazito

Posti hii inahusu zaidi njia mbalimbali za kuzuia Malaria kwa wajawazito na watoto wao wakiwa bado tumboni, tunajuwa wazi kuwa wajawazito wakipata Malaria inaweza kupelekea mimba kutoka kwa hiyo ili kuzuia tatizo hili zifuatazo ni njia zilizowekwa ili kuz

Soma Zaidi...
Tofauti za ute kwa mwanamke

Posti hii inahusu zaidi tofauti mbalimbali za uke, kwa sababu ya kuwepo kwa matatizo mbalimbali kwenye mwili wa binadamu kuna tofauti mbalimbali za ute kutegemea na hali iliyopo.

Soma Zaidi...