Posti hii inazungumzia kuhusiana na huduma kwa mama wajawazito na waliojifungua.
Mama mjamzito akiona Dalili zifuatazo awahi kituo Cha afya
1.kutokwa na Damu ukweni.
2.mtoto Kupunguza au kuacha kucheza tumboni.
3.maumivu makali ya tumbo.
4.maumivu makali ya kichwa.
5.kushindwa kuona vizuri.
6.kutokwa na majimaji ukweni.
7.Homa Kali.
Mambo ya kuzingatia kwa mama ili apate huduma endelevu.
1.Aanze kliniki ya ujauzito pale tu atakapojihisi ana mimba.
2.Ahudhurie mahudhurio ya kliniki yote nane.
3.ajifungulie katika kituo Cha huduma ya afya.
4.ahudhurie kliniki baada ya kujifungua Ndani ya siku tatu, baada ya siku ishirini na nane na baada ya siku Arobaini na mbili 42.
5.mama mjamzito anahitaji kula vyakula vyenye virutubisho vya kutosha ili aweze kukidhi mahitaji yake ya kilishe ya kila siku pamoja na Mtoto aliye tumboni.
6.anahitaji kula mlo kamili wenye mchanganyiko kutoka katika makundi matano vinavyopatikana katika jamii ya maziwa, matunda na mbogamboga, nyama,mayai,nafaka na jamii ya kunde.
7.mama anaye nyonyesha ana uhitaji mkubwa wa virutubisho kwaajili yake mwenyewe na kutengeneza maziwa kwa ajili ya mtoto, hivyo anapaswa kula Milo mingi kuliko Kawaida ili kukidhi ongezeko la mahitaji kwa ukuaji wa Mtoto.
8.mama mjamzito anapaswa kula Milo mitatu ya vyakula mchanganyiko na Milo miwili ya ziada kila siku ili kuimarisha Hali yake ya lishe na kuimarisha lishe ya mtoto anaye nyonya.
9.mama amnyonyeshe Mtoto Mara tu anapojifungua (Ndani ya saa moja)
10.mama asimpatie Mtoto chakula au kinywaji kingine chochote au maji mpaka atimize miezi sita
11.mama amwanzishie Mtoto vyakula vya nyongeza Mara anapotimiza miezi sita huku akiendelea kunyonya.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Posti hii inahusu zaidi madhara ya fangasi ukeni, madhara mbalimbali yanayoweza kutokea iwapo mtu hakutibiwa fangasi mapema.
Soma Zaidi...Kuunda na kujaa kwa matiti ni miongoni mwa dalili za ujauzito lakini pia ni dalili za kukaribia hedhi kwa baadhi ya wanawake. Posti hii itakwenda kufafanuabutofauti wa dalili hizi na kipi ni sahihibkatibya hedhi ama ujauzito.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi vyanzo vya kuharibika kwa mimba kuanzia miezi zero mpaka miezi mitatu, kwa sababu hii ni miezi ya kwanza kabisa Kuna sababu au vyanzo vya kuharibika kwa mimba katika kipindi hiki.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukuletea hatua za ukuaji mimba na dalili zake
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi namna ya kutibu tatizo la ugumba kwa Mwanaume, ni njia ambazo utumiwa na wataalam mbalimbali Ili kuweza kutibu tatizo la ugumba kwa wanaume.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza njia za kuongeza nguvu za kiume
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukuletea tiba mbadala ya fangasi wa uumeni
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi kuwepo kwa maziwa kwa akina Mama wakati wa ujauzito ni kawaida kwa sababu ya kuzaliwa kwa homoni ambayo usaidia kutoa maziwa.
Soma Zaidi...Post hii itakujulishs kwa namna gani mwanaune anaweza kupata fangasi kwenye uume wake
Soma Zaidi...