Choo kisichokuwa cha kawaida
Posti hii inahusu zaidi Aina ya choo kisichokuwa cha kawaida, ni dalili za choo ambacho siyo Cha kawaida, Ina maana ukiona dalili za choo Cha Aina hii ni vizuri kwenda hospitalini Ili kupata matibabu.
Choo kisichokuwa cha kawaida.
1. Choo kuwa kigumu.
Choo kisichokuwa huwa ni kigumu na Kuna shida wakati wa kutoa choo hicho kwa kitaalamu huitwa constipation, hali hii uwatokea hasa watu wale ambao huwa hawanywi maji ambapo maji ufyonzwa kwenye choo na kwenda kufanya kazi mbalimbali kwenye sehemu za mwili , choo hiki kwa kawaida huwa na kikavu kabisa, wakati mwingine mtu ufikishwa hospitalini na kupata matibabu zaidi kwa sababu ya choo kuwa kigumu, kwa hiyo watu wanashauliwa kunywa maji kwa wingi Ili kufanya choo kuwa laini.
2. Kinyesi kuwa kilaini au kuharisha.
Ni kitendo Cha kupitisha kinyesi kama maji , kinyesi hiki huwa ni maji hali hii utokea kwa sababu ya maambukizi kwenye tumbo ambapo pengine mtu anakuwa amekula chakula kichafu au pengine ni kwa sababu ya magonjwa ambayo yapo mwilini, kwa hali ya kawaida kinyesi hakipaswa kuwa hivi kinapaswa kuwa Cha kawaida bila kuwa kwenye mfumo wa maji, kwa hiyo kuharisha ni kitendo mibaya ambacho upelekea kuishiwa na maji mwilini na kusababisha madhara mengine makubwa zaidi ambayo huwezi kutengeneza, kwa hiyo tunapaswa kuhakikisha kuwa kinyesi kinakuwa Cha kawaida.
3. Kinyesi kuwa na damu.
Hali ya kinyesi hiki siyo ya kawaida kwa sababu kinyesi hakipaswa kuwa na damu, hali ya kinyesi kuwa na damu ni kwa sababu ya kuwepo kwa maambukizi kwenye sehemu mbalimbali kama vile kwenye coloni na sehemu nyingine ambapo kinyesi upitia na kutoka nje kwa hiyo ikiwa mtu anaona damu kwenye kinyesi anapaswa kwenda hospitalini kupima.
4. Kinyesi kuwa na rangi ya kijani.
Hii ni Aina ya kinyesi ambapo kinyesi kinakuwa na rangi ya kijani kwa sababu mbalimbali kama vile kuwepo kwa matatizo kwenye mmengenyo wa chakula na mara nyingine kula sana mboga za majani ufanya kinyesi kuwa na rangi ya kijani. Kwa hiyo kinyesi kikiwa na rangi ya kijani tunapaswa kwenda hospitalini Ili kuangalia shida ni nini?. Itambulik kuwa kama ulikula mboga za majani huwenda ikasababisha kinyesi kuwa cha kijani, hivyo hakuna haja ya kuogopa.
5. Kuwepo kwa Ute mwingi kwenye kinyesi na pia kuwepo kwa usaha kwenye kinyesi.
Hali hii ya kuwepo kwa usaha na Ute kwenye kinyesi sio hali ya amani labda Kuna maambukizi yoyote kwenye sehemu ambapo kinyesi upitia na Aina ya chakula ambacho mtu utumia Mara kwa mara na ufanya kuwepo kwa Ute mwingi kwenye kinyesi, kwa hiyo hali hii sio nzuri inabidi kuchukua vipimo maana Pana uwezekano wa kuwepo kwa maambukizi.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉2 Simulizi za Hadithi Audio 👉3 Kitau cha Fiqh 👉4 Kitabu cha Afya 👉5 Dua za Mitume na Manabii 👉6 Bongolite - Game zone - Play free game
Post zinazofanana:
Zijue faida za mate mdomoni
Post hii inahusu zaidi umuhimu wa mate mdomoni, mate ni majimaji ambayo hukaa mdomoni na husaidia katika kazi mbalimbali mdomoni.
Soma Zaidi...fahamu vitamini A na kazi zake
Je na wewe i katika wale ambaowanahitaji kujuwa kuhusu Vitamini A, kazi zake na vyakula vya vitamini A. post hii inakwenda kukujuza zaidi pamoja na historia ya vitamini A.
Soma Zaidi...Utaratibu wa lishe kwa wagonjwa
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu utaratibu wa lishe kwa wagonjwa
Soma Zaidi...Haya hayawezi kuambukiza UKIMWI
Somo hili linakwenda kukuletea Mambo ambayo hayawezi kuambukiza UKIMWI
Soma Zaidi...Upungufu wa vyakula na madhara yake
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu madhara ya upungufu wa vyakula
Soma Zaidi...Yajue malengo ya kusafisha vidonda.
Posti hii inahusu zaidi malengo ya kusafisha vidonda, kwa sababu Kuna watu wengine huwa wanajiuliza kwa nini nisafishe kidonda hospitalini au kwenye kituo chochote Cha afya, yafuatayo ni majibu ya kwa Nini nisafishe kidonda.
Soma Zaidi...