Posti hii inahusu zaidi sababu za kupoteza fahamu, ni sababu ambazo umfanya mtu kupoteza fahamu kwa sababu mbalimbali kama ifuayavyo.
Sababu za kupoteza fahamu.
1. Kupata mshutuko.
Kupata mshutuko ni sababu mojawapo ya kumfanya mtu kupoteza fahamu, vitu kama vile habari mbaya ya kuondokewa na mpendwa yeyote katika jamii, magonjwa mbalimbali nayo usababisha mshutuko,kuona vitu vya kutisha, mawazo nayo usababisha mshutuko na kutoelewana katika familia na mambo mengine kama hayo uweza kumfanya mtu ashutuke na kupoteza fahamu.
2. Kupigwa na kitu kichwani.
Kupigwa na kitu kichwani usababisha kupoteza fahamu kwa sababu kwenye kichwa Kuna ogani ya muhimu ambayo ni ubongo, ubongo ufanya kazi mbalimbali kwenye mwili wa binadamu kwa hiyo ubongo ukishutuliwa tu mtu upoteza fahamu kwa hiyo tunapaswa kumpatia mgonjwa aliyepoteza fahamu mda wa kupumzika Ili ubongo uweze kutulia na kufanya kazi yake kama kawaida.
3. Mshutuko wa Moyo.
Pia mshutuko wa Moyo usababisha mtu kupoteza fahamu kwa sababu tunajua kuwa kazi kuu ya moyo ni kusukuma damu kwenye sehemu mbalimbali za mwili kwa hiyo na kazi ya damu ni kubwa mno kwenye mwili, kwa hiyo basi moyo ukishutuliwa tu mfumo ushindwa kufanya kazi yake kwa Kawaida na mtu upoteza fahamu, hali hii uweza kurudisha kwa kuamsha moyo ulioshutuluwa na mgonjwa urudia hali yake ya kawaida.
4. Kula au kulishwa sumu.
Kula au kulishwa sumu ni mojawapo ya sababu ya kupoteza fahamu kwa sababu sumu inapoingia kwenye mfumo wa damu ufanya damu yote kuwa sumu na kazi yake ya kawaida ushindwa kufanyika vizuri na baadae mtu upoteza fahamu na hali hii inaweza kutibiwa kwa kutumia huduma ya kwanza kwa mtu aliyekunywa sumu na pengine watu utumia Tiba asili kupunguza sumu kwenye mwili kama vile kumpatia mgonjwa mkojo na Tiba mbalimbali za asili na mgonjwa anaweza kupona.
5. Kiwango Cha sukari kushuka.
Kiwango Cha sukari kikishuka usababisha mgonjwa kupoteza fahamu kwa sababu tunajua kabisa kazi ya sukari mwilini ni kuongeza nguvu, kwa hiyo mwili ukiishiwa nguvu kila mfumo kwenye mwili uhishiwa nguvu hatimaye mtu hupoteza fahamu.kwa hiyo tatizo hili linaweza kutibiwa kwa kumpatia mgonjwa vyakula vyenye sukari kama vile soda, chai au kama mgonjwa Yuko hospitalin anaweza kupewa maji yanayoongeza sukari mwilini.
6. Kutumia kiasi kikubwa Cha Pombe au madawa ya kulevya.
Watumiaji wa madawa ya kulevya na Pombe uadhiri kiwango Cha kazi ya Neva system kwa kutumia vitu hivi kwa mda mrefu kwa hiyo na wakati mwingine Pombe umaliza kiwango Cha sukari mwilni na baadae mtu hupoteza fahamu kwa sababu wengine wanatumia Pombe na madawa ya kulevya bila chakula hatimaye wanapoteza fahamu, hao tunaweza kuwasaidia kwa kuwashauri na kubadilisha mtindo wa maisha Ili kuepusha madhara makubwa yanayoweza kujitokeza kwenye maisha yao
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowJe umeipenda post hii ?
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu madhara ya upungufu wa maji mwilini
Soma Zaidi...Posti hii inahusu kazi ya chanjo ya kifua kikuu kwa kitaalamu huitwa BCG. Ni chanjo ambayo uzuia kifua kikuu na ukoma.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi madhara ya kutotibu magonjwa ya vidonda vya tumbo, ni hatari inayotokea kwa mtu ambaye haujatibiwa vidonda vya tumbo.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi athari za kutotibu vidonda, hizi ni athari mbalimbali ambazo zinaweza kutokea ingawa kama vidonge haujatibiwa au vimetibiwa kwa kuchelewa.
Soma Zaidi...Hii ni hali inayotokea ambapo wili unakuwa na joto la juu sana tofauti na kawaida.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi hasara za magonjwa ya ngono, ni magonjwa yanayoambukizwa kwa kujamiiana bila kutumia kinga.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi mabadiliko kwa wavulana wakati wa kubarehe, ni kipindi ambacho ni kutoka utotoni kwendea ujana.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukuletea namna ambavyo mwili unapambana na maradhi
Soma Zaidi...Unyanyasaji wa kimwili. Unyanyasaji wa watoto kimwili hutokea wakati mtoto amejeruhiwa kimwili kimakusudi. Unyanyasaji wa kijinsia. Unyanyasaji wa watoto kingono ni shughuli yoyote ya kingono na mtoto, kama vile kumpapasa, kushikana mdomo na sehemu
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu huduma ya Kwanza kwa mtu aliyepatwa na shambulio la moyo
Soma Zaidi...