Namna ya kutunza nywele za mgonjwa

Namna ya kutunza nywele za mgonjwa

Posti hii inahusu zaidi namna ya kutunza nywele za mgonjwa hasa kwa wagonjwa mahututi na wale wasiojiweza tunafanya hivyo ili tuweze kuwatoa kwenye hali ya usafi.

Namna ya kutunza nywele za mgonjwa ambaye hajiwezi.

1.Kwanza kabisa tunapaswa kujua kuwa mara nyingi tunakuwa na wagonjwa majumbani kwetu na tunashindwa kuwahudumia kwa sababu ya kutojua au pengine tunashindwa tuwahudumie namna gani kwa hiyo na nywele za mgonjwa zinapaswa kusafishwa kwa njia zifuatazo.

 

2.Kwanza kabisa unapaswa kumwambia mgonjwa nia na lengo la kumfanyia usafi kama mgonjwa anaweza kusikia na pia hakikisha kuwa hakuna Watu ambao hawahusiki ili mgonjwa aweze kujisikia huru  unaweza kuwa na msaidizi wako.

 

3.Ondoa nguo kwenye sehemu ya kichwa na weka nguo za kumwoshea Mgonjwa inaweza kuwa kanga au kitambaa chochote ambacho ukitoa unaweza kukiosha tena na weka mpira ili maji yasidondoke kwenye godoro na Mashuka mengine.

 

4.Msaidie mgonjwa aweze kusogeza kichwa chake juu ya kitanda ili kuweza kuwa karibu na beseni na hakikisha kichwa kipo kwenye beseni na wakati wa kumwosha nywele tumia maji ya moto .

 

5 Chukua maji kutoka kwenye beseni na mwekee mgonjwa na mwekee kwenye kichwa cha Mgonjwa na weka sabuni safisha nywele za mgonjwa na hakikisha kuwa zimetakata na pia chukua taulo safi upanguse nywele za mgonjwa na safisha sehemu ambapo mgonjwa alikuwepo na hakikisha mgonjwa nywele zake zimekuwa safi.

 

6.Mpake mafuta mgonjwa kwenye nywele zake na kama kuna mba unaweza kuweka dawa ili kuepuka hali ya kujikuna kama inawezekana unaweza kumsuka kama ni mwanamke.

 

7.Kwa hiyo baada ya kujua haya tuwafanyie usafi wa nywele wagonjwa na mtaweza kuona mabadiliko kwa sababu pengine hali ya mgonjwa uendelea kubwa mbaya kwa sababu ya kuwepo kwa uchafu kwa kumfanyia mgonjwa usafi anaweza kupata nafuu.

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu Rajabu
Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Huduma Main: Post File: Download PDF Views: 2023

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉2 web hosting     👉3 ai web app     👉4 Kitau cha Fiqh     👉5 Madrasa kiganjani     👉6 Dua za Mitume na Manabii    

Post zinazofanana:

Namna ya kusaidia vijana wakati wa kubarehe

Post hii inahusu zaidi namna ya kuwasaidia vijana wakati wa kubarehe, ni njia za kuhakikisha kuwa vijana wanakuwa na mwelekeo ,

Soma Zaidi...
Zijue kazi za ovari

Posti hii inahusu zaidi umuhimu wa ovari kwenye mwili wa mwanamke. ovari ni sehemu ambapo mayai ya mwanamke hutunza, kwa hiyo kila mwanamke huwa na ovari ambayo husaidia kutunza mayai.

Soma Zaidi...
Je, utamsaidia vipi mtu aliyeumwa na nyuki?

Posti hii inazungumzia kuhusiana na kumsaidia mwenye aliyeumwa na nyuki.nyuki na wadudu ambao wakikushambulia Sana na ukikosa msaada unaweza kufa au kuwa katika Hali mbaya.

Soma Zaidi...
Njia za kushusha presha

Post hii inakwenda kukujulisha njia za kushusha presha iliyopanda.

Soma Zaidi...
Fahamu kuhsu vitamini E na kazi zake mwilini

Je unazijuwa faida za kuwa na vitamini E mwilini mwako.Unahani utapata matatizo yapi ya kiafya endapo utakuwa na upungufu wa vitamini E mwilini? Makala hii ni kwa ajili yako.

Soma Zaidi...
Zijue sababu za kupoteza fahamu.

Posti hii inahusu zaidi sababu za kupoteza fahamu, ni sababu ambazo umfanya mtu kupoteza fahamu kwa sababu mbalimbali kama ifuayavyo.

Soma Zaidi...