image

Kazi za chanjo ya polio

Posti hii inahusu zaidi kazi ya chanjo za polio na kazi zake,hii ni chanjo ambayo unazuia maambukizi ya Virusi vinavyosababisha polio.

Kazi za chanjo ya polio.

1. Chanjo ya polio ni Aina mojawapo ya chanjo ambayo utolewa kwa watoto wadogo Ili kuwakinga na virusi vinavyosababisha polio, polio ni ugonjwa mbaya ambapo ukimshambulia mtoto unaweza kuleta madhara makubwa kwa mtoto maisha yake yote kwa hiyo ndio maana selikali na ulimwengu mzima ujitahidi kuwapatia watoto wadogo chanjo hii mara tu baada ya kuzaliwa.

 

2. Chanjo hii mtoto anapewa pindi tu anapozaliwa, tena anapewa baada ya wiki sita tena anapewa baada ya wiki nne mpaka pale anapofikisha  miezi miwili na nusu anakuwa bado anapewa chanjo hii ya polio, kwa hiyo mama na walezi wa mtoto wanapaswa kujua kabisa mda na wakati wa kumpeleka mtoto kwa ajili ya kupata chanjo Ili kumwepushia madhara mbalimbali ambayo yanaweza kujitokeza kwa sababu ya kutopata hii chanjo.

 

3. Chanjo ya polio isipotolewa mtoto anaweza kupata ugonjwa wa polio ambapo kwa kuangalia dalili mbalimbali kama vile utepe kwenye mguu au mkojo, ulemavu wa maisha na pengine mtoto anaweza kupooza kwa Saba ya Virusi vinavyosababishwa na ugonjwa wa polio, kwa hiyo akina Mama na walezi wote wanapaswa kupewa elimu kuhusu matatizo ambayo utokea kwa watoto wadogo wasipopata chanjo ya polio na wataweza kuona umuhimu wa kuwapatia watoto chanjo.

 

4. Pamoja na kuwepo kwa chanjo ya ugonjwa wa polio Kuna matokea ambayo yanaweza kutokea kwa mtoto baada ya kupata chanjo hii, ni kama vile  Alama kwenye sehemu ambapo chanjo imetolewA na maumivu kidogo ambayo udumu kwa mda kidogo. Kwa hiyo mama au mlezi wakiona dalili ya mtoto kukosa raha na kulia wasishangae kwa sababu ni maumivu kidogo  ya chanjo na uisha kwa mda mfupi tu.





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 997


Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

Fahamu kuhusu vitamini C na kazi zake
Makala hii itakujulisha kazi kuu za vitamini C mwilini. Hapa pia utatambuwa ni kwa nini tunahitaji vitamini C na wapi tutavipata Soma Zaidi...

HUDUMA YA KWANZA KWA ALIKAZWA NA MISULI
Kukaza kwa misuli lunaweza kutokea muda wowote ila mara nyingi hutokea pindi mtu anapofanya mazoezi, amnapoogelea ama anapofanya kazi. Soma Zaidi...

Njia za kufuata unapohudumia watu waliopata ajali
Post hii inahusu zaidi namna ya kutoa huduma ya kwanza kwa watu waliopata ajali. Ajali ni tukio lisilotarajiwa ambalo kinaweza kumkuta mtu yeyote, tunapotoa huduma ya kwanza tnazingatia rangi ambazo huwakilisha jinsi watu walivyoumia. Soma Zaidi...

HUDUMA YA KWANZA KWA ALIYEANGUKA KIFAFA
Kifafa kinaweza kumpata mtu muda wowte. Soma Zaidi...

Uvimbe kwenye utandu laini uliopo tumboni (peritonitis)
Posti hii inazungumzia kuhusiana na Uvimbe au mashambulizi ya bacteria kwenye utando laini uliopo tumboni ambao kitaalamu hujulikana Kama peritonitis. Soma Zaidi...

Imani potofu juu ya chanjo.
Post hii inahusu zaidi Imani potofu juu ya chanjo kwa watoto na akina Mama, ni baadhi ya Imani waliyonayo watu juu ya chanjo. Soma Zaidi...

Namna ya kumwosha Mgonjwa vidonda
Posti hii inahusu zaidi njia za kutumia unapotaka kumwosha Mgonjwa vidonda, ni njia muhimu ambazo ni lazima kuzipitia unapotaka kumwosha Mgonjwa vidonda. Soma Zaidi...

Aina za mishipa inayosafilisha damu mwilni
Post hii inahusu zaidi mishipa inayosafilisha damu mwilni, ni Aina tatu za mishipa ambazo usafilisha damu kutoka sehemu Moja kwenda nyingine Soma Zaidi...

Huduma ya Kwanza kwa mtu aliyeng'atwa na nyoka
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu huduma ya Kwanza kwa mtu aliyeng'atwa na nyoka Soma Zaidi...

Roghage/ vyakula vya kambakamba
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za vyakula vya roghage Soma Zaidi...

Malengo ya kutibu ukoma
Posti hii inahusu zaidi malengo ya kutibu ukoma, ni malengo ambayo yamewekwa na wizara ya afya ili kuweza kutokomeza ukoma kwenye jamii Soma Zaidi...

Ratiba ya chanjo ya kuzuia Nimonia
Posti hii inahusu zaidi ratiba ya chanjo ya kuzuia Nimonia, hii ni chanjo inayozuia hasa hasa Magonjwa ya mfumo wa hewa kwa hiyo nayo upewa watoto wenye umri chini ya miaka mitano. Soma Zaidi...