Namna ugonjwa wa herpes simplex unavyosambaa.

Posti hii inahusu zaidi namna ya ugonjwa wa vipele kwenye midomo na sehemu za siri unavyoweza kuenea kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine.

Namna ugonjwa wa herpes simplex au vipele kwenye midomo na sehemu za siri unavyoweza kuenea kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine.

1.Ugonjwa huu wa herpes simplex unaweza kusambaa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kwa njia ya kujamiiana pasipokutumia kondomu kwa hiyo wakati wa kujamiiana ni lazima kutumia kinga ili kuzuia kuenea kwa ugonjwa huu ambao hauna tiba.

 

2.vile vile ugonjwa huu unaweza kusambaa kwa kupigana busu kwa wapenzi na wale wenye utamaduni wa kufanya hivyo, kwa hiyo tunapaswa kuwa makini katika kupigana busu kwa kuangalia kwanza kama kuna dalili na wagonjwa wanapaswa kuwa wazi kama wana ugonjwa huu.

 

3.Pia Ugonjwa huu unasambaa kwa kutumia vifaa ambavyo vimetumiwa na mtu mwenye Ugonjwa huu ikiwa virus wamebaki kwa hiyo tunapaswa kuosha vizuri vyombo vyetu kama tunafikiria au tunajua kuna mtu ana matatizo hayo na ametumia vyombo hivyo, kwa hiyo hatupaswi kuwatenga wagonjwa wenye matatizo ya aina hii ila tuwahudumie na kuwa makini.

 

4.Ugonjwa huu unasambaa kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto wakati wa kujifungua kwa hiyo mama anapaswa kujifungulia hospitalini ili kuepuka Maambukizi kutoka kwa Mama kwenda kwa mtoto na pia akina Mama wakati wa ujauzito wanapaswa kupima afya zao ili kuepukana kuwaambukiza watoto wao.

 

5.Baada ya kujua njia zinazotumika kuambukiza ugonjwa huu ni lazima kubwa makini na kujikinga ili kuepuka kusambaza ugonjwa huu kwa sababu unasababishwa na virusi kwa hiyo kupona kwake na majaliwa ya Mwenyezi Mungu.Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/02/23/Wednesday - 04:43:00 pm     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 785


Download our Apps
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-