KUHARIBIKA KWA UJAUZITOKitendo cha kuharibika kwa ujauzito kitaalamu hutambulika kama spontaneous abortion. Ni kutoka kwa ujauzito ndani ya wiki 20 za mwanzo. Tafiti zinaonesha kuwa yapata asilimilia 50 ya mimba hutoka yaani nusu ya mimba zinazotugwa hutoka. Wengiwao hupatwa tu na ha;I ya kukosa siku zao bila ya kujuwa kama walikuwa na ujauzito na wengine wanajigundua. Pia tafiti zinaonyesha kuwa yapata asilimia 15 mpaka 25 ya mimba ambazo zimejulikana hutoka. Hata hivyo mimba nyingine hutoka siki chache tu baada ya kuingia. Sasa ni kwa nini mimba hutoka? Makala hii inakwenda kukupa elimu juu ya kutoka kwa mimba, dalili zake na sababu zake.


Dalili za kutoka kwa ujauzito
1.Kutokwa na damu ambayo inawza kuongezeka kadiri muda unavyoenda.
2.Maumivu ya tumbo
3.Kupata uchovu
4.Maumivu makali ya mgongo
5.Kupatwa na homa iliyochanganyikana na moja ya dalili zilizotajwa hapo juu.


6.Sababu za kutoka ujauzitoMaumivu ya chango kupitiliza

Mimba nyingi hutoka kwa sababu kuna matatizo kwenye genetics za mtoto na si kosa la mama ama la baba. Hii ni kutokana na maumbile ya mtoto kuwa na shida katika ufanyikaji. Sababu nyingine za kutokwa na ujauzito ni:-
1.Maambukizi, watu waishio na baadhi ya maambukizi kama PID ama HIV wanaweza kuwa hatarini.
2.Kuwa na maradhi kama kisukari ama maradhi katika tezi ya thyroid
3.Matatizo katika homoni
4.Mfumo wa kinga kuondoa mimba
5.Shughuli na maumbile ya mama
6.Mfuko wa mimba kuwa na matatizo


Pia mwanamke anaweza kuwa na nafasi kubwa ya kutokwa na ujauzito kama:-
1-Atakuwa na umri wa zaidi ya miaka 35
2-Ana maradhi kama kisukari au maradhi ya tezi ya thyroid
3-Kama ana kawaida ya kutokwa na ujauzito zaidi ya mara tatu.