SIKU YA KUPATA UJAUZITO Mimba hutokea pindi mbegu ya kiume (sperm) inapokutana na yai la mwanamke (ova) na kuungana kwa pamoja kutengeneza selli moja iitwayo zygote.
SIKU YA KUPATA UJAUZITO
Mimba hutokea pindi mbegu ya kiume (sperm) inapokutana na yai la mwanamke (ova) na kuungana kwa pamoja kutengeneza selli moja iitwayo zygote. Seli hii hukuwa na kujakuwa mtoto kamili. Kawaida kitendo hiki hufanyika ndani ya masaa 12 toka yai kukomaa na kuletwa kwenye mirija ya falopian. Baada ya mimba kutungwa itabakia pale kwa masaa kama matatu, kisha huanza kusafirishwa na kupelekwa kwenye tumbo la mimba ambapo huku litabakia mpaka mtoto kuzaliwa.
Mwanamke hutoa yai moja kila mwezi kutoka katika ovari moja. Kuna wakati mwanamke huenda akatowa mayai zaidi ya moja, hali hii si kawaida. Yai hili linaweza kuwa hai ndani ya masaa 12 mpaka 24. hutokea pia likaweza kuwa hai mpaka masaa 48. ndani ya muda huu yai ni lazima likutane na mbegu ya kiume ili mimba itungwe. Kipindi hiki kitaalamu kinajulikana kama fertile window.
Mbegu ya mwanaume huweza kudumu kuwa hai ndani ya siku 5, ndani ya siku hizi mbegu hizi huwa zipo hai hivyo zinaweza kurutubisha yai. Mwanaume huto zaidi ya mbegu milioni 300 ejaculation moja. Katika mbegi hizi mbegu moja ndio hutakiwa kuungana na yai.
Siku za mwanamke kuweza kuwa kati ya 21 mpaka 35 inategeme na mwanamke. Kikawaida walio wengi siku zao ni 28. katika siku hizi zipo siku 6 tu ambazo mwanamke anaweza kupata ujauzito. Siku hizi huanzia siku ya 11,12,13,14,15 na 16. katika siku hizi siku ya 14 ndio ambayo huaminika zaidi kuwa yai hutolewa ziku hii. Ni vyema kukutana kimwili katika siku hizi kwa wanaotafuta ujauzito. Sio lazima pia kufululiza inawezekana kuruka ila nivyema kutoikosa siku ya 13 na 14.
Pia kuna dalili kadha za kuijua siku hii kama kuzidi kwa joto la mwanamke siku moja kabla na siku ile ya kutolewa kwa yai. Pia kuongezeka kwa utelezi kwenye shingo ya uzazi. Pia mwanamke anapenda sana kukutana kimwili kukaribia siku hii. Vipo vifaa pia vya kuitambua siku hii. Siku hizi huhesabiwa kutoka kupata hedhi na kuendelea. Pia siku hisi kutofautiana kwa wanawake.
Umeionaje Makala hii.. ?
Tendo la ndoa wakati wa siku za hedhi ni halia mbayo jamii nying zinakataza. Katika vitabu vya dini pia haviruhusu, hata ki saikolojia utaona kuwa sio jambo jema. Hata hivyo hapa ninakuletea madhara yake kiafya
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi sababu za mimba ya miezi kuanzia minne mpaka sita kutoka , Kuna kipindi mimba kuanzia miezi mimne mpaka sita utoka kwa sababu mbalimbali.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi madhara ambayo yanaweza kutokea kama mtoto alizaliwa na uzito mkubwa.
Soma Zaidi...Posti hii inazungumzia kuhusiana na maambukizi na uvimbe katika mirija ya uzazi. Mara nyingi hutumiwa sawa na ugonjwa wa uvimbe kwenye fupa nyonga (PID), ingawa PID haina ufafanuzi sahihi na inaweza kurejelea magonjwa kadhaa ya njia ya juu ya uzazi
Soma Zaidi...Miongoni mwa matunda yenye virutubisho vingi ni pamoja na papai, nanasi, tikiti, palachichi, pera, karoti, hindi na boga. Lakini katika matunda haya yapo ambayo kwa mimba changa anatakiwa awe makini, kama papai na nanasi. Sasa vipi kuhusu mimba ya
Soma Zaidi...Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu sababu za maumivu ya uume baada ya tendo la ndoa
Soma Zaidi...Hii ni hali inayowapata sana wanaume huwa wanamaliza hamu ya tendo la ndoa mapema kabla ya mwenza kuridhika.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi sababu za kupasuka kwa mfuko wa uzazi hasa mama anapokalibia kujifungua.
Soma Zaidi...Utajifunza dalili za minyoo, sababu za minyoo na namna ya kujiepusha na minyoo. Dalili kuu 5 za minyoo mwilini
Soma Zaidi...