MAUMIVU WAKATI WA TENDO LA NDOA

Maumivu wakati wa tendo la ndoa kitaalamu huitwa dyspareunia. Maumivu haya hutokea kwa namna mbalimbali. Mara nyingi maumivu haya huwapata wanawake. Mara chache wanaume wanapokuwa na maradhi flani kama fangasi kwenye uume ama maradhi mengine ya ngono ndipo hupata maumivu haya.

 

Maumivu haya hutokea pindi:

 1. Pindi uume unapoingia ukeni kwa mara ya kwanza
 2. Kila wakati uume unapoingia ukeni
 3. Maumivu wakati wa kupushi na kutoka kwa uume
 4. Kuhisi kuungua ukeni
 5. Maumivu baada ya kufanya tendo la ndoa

 

Sababu za maumivu haya

 1. Kutokuwepo kwa uteute wa kutosha wa kulainisha uke
 2. Majeraha na makovu ukeni kama waliotahiriwa
 3. Kuvimba kwa uke ama kuwa na mashambulizi ya bakteria
 4. Matatizo ya saikolojia
 5. Kukaza kwa misuli ya uke
 6. Maumbile ya uuke kama kuwepo kwa utando unaozuia njia ya uke kuwa wazi
 7. Kufanyiwa upasuaji kama hysterectomy ama matibabu ya saratani
 8. Kuwa na msongo wa mawazo
 9. Staili iliyotumika wakati wa kufanya tendo


 10.