Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu changamoto za ujauzito na dalili zake endelevu
CHANGAMOTO ZA UAJAUZITO NA DALILI ZENYE KUENDELEA:
Ni vyema sana kutambuwa hili, kwani itakusaidia katika klujuwa changamioto za ujauzito. Katika dalili hizi za ujauzito zipo ambazo nio zenye kuendelea. Na katika kuendelea hko wengi katika wajawazito wanapatwa na changamoto kadhaa. Hapa nitakueleza nini cha kufanya.
1.KichefuchefuKichefuchefu kinaweza huweza kuchelewa kujitokeza lakioni kinaweza kuwa ni chenye kuendelea. Kwa baadhi ya wanawake kinaweza kwenda mpka miezi kadhaa mbele, ila kwa wengi kinaweza kukata kufikia wiki ya 28. Hii ni changamoto kwakweli kwa wajawazito. Maana kichefuchefu kinaweza lumkoseshea amani wakati mwingine.hali ya kutema mate, kuhisi kutapika ama kichefuchefu kwa ujumla huwasumbua wajawazito. Wataalamu wanaeleza kuwa hasa chanzo cha kichefuchefu ni mabadiliko ya homoni mwilini. Na huwenda pia kuna sababu nyingine.
Kama utakuwa unasumbuliwa na hali hii fanya hivi. Epuka kukaa maeneo yenye joto sana. Epuka kunywa maji wakati unakula. Tumia tangawizi, kwenye chai ama tafuna. Unaweza kuiweka kama unga ama vipande vidogovidogo. Unaweza kutumia bigjii maalumu kwa ajili ya wajawazito.
2.Maumivu ya tumbo:Kwa wajawazito maumivu ya tumbo mara kwa mara ni hali ya kawaida na yenye kuendelea. Maumivu haya yanaweza kuchukuwa muda mchache na kuondoka. Pia ni yenye kuvumilika yaani mwanamke anaweza kuendelea kufanya shughuli zake. Ila endapo yatakuwa ni makali sana kutovumilika inaweza kuashiria kuna shida kwenye afya ya mwanamke huyu. Ni vyema kufika kituo cha afya kupata ufafanuzi wa hali.
Katika hali ya maumiovu haya ya tumbo mwanamke anaweza kutumia dawa za kupunguza maumivu. Pia zipo tiba mbadala kupunguza maumivu. Ila mwanamke awe makini sana maana anaweza kuingia katika hatari endapo atatumia dawa kiholela.
3.Kutokwa na damu:Kama ilivyo dalili nyingine huendelea basi si jambo ;la kushangaza kwa mwanamke mjamzito kujikuta nguo yake ya ndani kuwa na vitone vya damu. Damu hii si yenye kuchuruzika ama yenye kutoka kwa wingi kama damu ya hedhi. Endapo mjamzito atakuwa anatokwa na damu nyingi eidha iambatane na maumivu makali ya tumbo ama isiambatane ni vyema awahi kituo cha afya kupata uthibitisho juu ya mabadiliko hayo. Maana wakati mwingimne damu inaweza kuashiria shida katika ujauzito.
4.Mabadiliko katika hisia, matakwa na matamanio katika vyakula na vitu vingine.Haswa mwanamke anaweza kujishangaa mwenyewe inakuweje hali hii. Mwanamke anaweza kuona kuwa nachukia vitui ama kuna watu anawachukia ghafla. Wakati huo huo anaweza kupenda mtu flani sana. Pia kuna wakati atakuwa anachukia baadhi ya vyakula na vitu vingine. Yaani kwa ufupi ni mabadiliko tu katika saikolojia yake. Huu si ugonjwa hivyo hali hii isimpe mawazo saana mwanamke. Watu walio karibu na wajawazito wawe makini pia maana wanaweza kufanya makosa makubwa kama kumpiga na vinginevyo.
5.Kuvimba ama kujaa kwa uso na miguu.Yes hii ni changamoto kwa kweli. Hii haiwapati wenye mimba ya miezi ya mwanzo, hali hii hutokea wakati mimba imesha komaa miezi ya mbeleni. Kuvimba ama kujaa kwa uso na miguu kwa wajawazito sio jambao la ajabu. Hali huweza kukaa sawa atakapojifungua. Kama mwanamke anasumbuliwa na hali hii, ahakikishe anapumzika katika maeneo yenye utulivu na yaliyopa yaani aepuke kukaa maeneo yenye joto. Pia aepuke kubvaa nguo za kabana. Aepuke kukaa chini katika mkao mmoja kwa muda mrefu.
6.Kuenda haja ndogo mara kwa mara.Hii ji changanmoto hasa kwa wale ambao ndio ujauzito wao wa kwanza.Hapa pia kuna wajawazito wanajitahidi kujizuia eti wapunguze kuenda haja ndigo. Hii sio sawa kabisa. Mjamzito anatakiwa anaposikia haja kakaitoe wala asihofu kitu huu si ugonjwa na ni kawaida kabisa. Kwa kuwa moyo wake umeongeza utendaji wa kazi hivyo uchujwaji wa damu ni mkubwa. Kwa maendeleo mema ya afya yake na afya ya ujauzito wake, mjamzito asihofu kitu, aende tu haja.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowUmeionaje Makala hii.. ?
Posti hii inahusu zaidi fangasi za ukeni, hili ni tatizo kubwa ambalo linawakumba watoto, akina dada na wanawake kwa hiyo na vizuri kujua Dalili zake na kuweza kuchukua hatua mapema.
Soma Zaidi...Post hii inakwenda kukupa sababu zinazoweza kupelekea uke kuwa mkavu yaani kukosa majimaji wakati wa kufanya tendo la ndoa.
Soma Zaidi...Posti hii inaelezea kuhusiana na nguvu za kiume zinavyopungua na Ni Mambo gani yanayofanya zipungue
Soma Zaidi...Posti hii inazungumzia kuhusiana na Mambo ambayo mama mjamzito anatakiwa kuzingatia katika kipindi Cha ujauzito au mimba
Soma Zaidi...KUVIMBA VYA MIGUU KWA WAJAWAZITO Kuvimba kwa miguu ni hali inayowapara wengi katika wajawazito.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi uhusiano uliopo kati ya Mama Mjamzito na kibofu cha mkojo.ni mwingiliano unaokuwepo ambao usababisha Mama kukojoa sana wakati wa ujauzito.
Soma Zaidi...Mimba inaweza kutoka kutokana na maradhi, majeraha ama misukosuko mimgine. Kutoka kwa mimva haimaanishi ndio mwisho wa kizazi.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi sababu za kuvunjika kwa mtoto wakati wa kuzaliwa, kuna wakati mtoto anapozaliwa anaweza kuvunjika kwenye sehemu mbalimbali kwa sababu zifuatazo.
Soma Zaidi...Post hii itakujulidha mambo ambayo hupunguza nguvu za kiume
Soma Zaidi...Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu sababu za maumivu ya tumbo wakati wa tendo la ndoa
Soma Zaidi...