Njia za kuzuia Malaria kwa wajawazito
Posti hii inahusu zaidi njia mbalimbali za kuzuia Malaria kwa wajawazito na watoto wao wakiwa bado tumboni, tunajuwa wazi kuwa wajawazito wakipata Malaria inaweza kupelekea mimba kutoka kwa hiyo ili kuzuia tatizo hili zifuatazo ni njia zilizowekwa ili kuz
Njia za kuzuia Malaria kwa wajawazito.
1.Kuwapatia wajawazito neti pindi wanapoanza mahudhurio ya kliniki.
Hii ni mojawapo ya njia ambayo inafanya kila mahali nchini ambapo kila mwanamke mwenye mimba akija kuanza mahudhurio ya kliniki anapewa neti ili aweze kulala ndani yake wakati wa usiku na kuzuia mbu wanaoeneza Malaria wasimpate akilala ndani ya neti, kw hiyo akina Mama wale wazembe wa kuhudhuria kliniki mnapaswa kwenda ili kuepukana na Ugonjwa wa Malaria.
2.Pia kuna watu wenye mila potofu wakipewa neti badala ya kuitumia wakati wa kulala wanaitumia kufugia kuku na kufunika mazao ili yasiliwe na wadudu kwa hiyo elimu ni ya msingi kwa jamii ili kuepuka vitu vya namna hivyo na wanaofanya mambo kama haya wanapaswa kuchukuliwa na sheria kwa sababu hizi neti ni bajeti ya serikali.
3.Na njia nyingine ni kutoa dawa za SP kila mwezi pale ambapo Mama anakuja kwenye mahudhurio ya kliniki. Kila mwezi kwenye vituo vyote akina Mama upewa dawa za SP lengo ni kuzuia wadudu wanasababisha malaria kutofikia mtoto, maana dawa hizi ukaa karibu na plasenta ikitokea mdudu amefika uweza kuuawa na hawezi kupata Malaria, kwa hiyo akina Mama wanaoanza kliniki wakiwa na miezi sita hawapati dawa hizi kwa wakati kwa hiyo wanaweza kuwa katika hatari ya kupata Maambukizi.
4.Kuna baadhi ya mila na desturi za watu wakipewa dawa hizo uleta visingizio wakidai watatumia wakiwa njiani eti zinawasumbua na wakienda nyumbani hawatumii wanatumia madawa ya kienyeji hali hii usababisha mama kujifungua mtoto mfu au mimba kutoka, kwa hiyo hakina Mama jaribu kujali maisha yenu na watoto pia nenda kliniki kwa wakati, tumia kila dawa ipasavyo na nakuhakikishia utajifungua salama achana na mila na desturi za zamani maisha yamebadilika kuna magonjwa mengi na vitu vingi kwa hiyo okoa maisha yako na mtoto wako.
5.Njia nyingine ni kupima Malaria kwa wajawazito pindi tu wanapoanza mahudhurio ya kliniki, hii inatumika kila sehemu ambapo wanawake wanapoanza kliniki kati ya vipimo vinavyopikwa na Malaria nayo imo kwa kuft hivyo ni kutafuta njia ili kutokomeza ugonjwa huu. Kwa hiyo akina Mama wale wazembe wa kuhudhuria kliniki Malaria ipo na inaweza kumshika mjamzito na kusababisha madhara makubwa kama vile mimba kutoka na kuzaa mtoto mfu, kwa hiyo acha uvivu nenda kliniki
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Simulizi za Hadithi Audio 👉2 Dua za Mitume na Manabii 👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉4 Bongolite - Game zone - Play free game 👉5 Madrasa kiganjani 👉6 Kitabu cha Afya
Post zinazofanana:
Mimi kwenye korodani yai moja limezungukwa na majimaji ,na haya maji yamekuwepo toka utotoni mwangu lakin bado sijayaona matatizo yake , je kitaaramu hii inaweza kua na athari gani? ,Naombeni ushauri
Korodani ni kiungo muhimu kwa mwanaume, katika afya ya uzazi. Unaweza kusema ni kiwanda cha kutengeneza mbegu za kiume. Kiungo hiki ni sawa na ovari kwa mwanamke.
Soma Zaidi...Umuhimu wa maji yaliyomo kwenye mfuko wa mtoto akiwa tumboni mwa mama
Post hii inahusu zaidi umuhimu wa maji yaliyomo kwenye mfuko wa mtoto akiwa tumboni. Ni maji ambayo kwa kitaalamu huitwa (Amniotic fluid)
Soma Zaidi...Kutokwa na damu baada ya tendo la ndoa
Kutokwa na damu baada ya tendo la ndoabkunaweza kuashiria kuwa kuna majeraha yametokea huwenda ni michubuko ilitokea ndio ikavujisha damu. Lakini kwa nini hali kama hii itokee. Posti hii itakwwnda mujibu swali hili.
Soma Zaidi...Niharisha siku ya pili baada ya tendo. Jana hadi leo sijapata choo inawezakua nimeshika ujauzito?
Hivi unadhani kuharisha ni katika dalili za mimba, vipi kuhusu kutopata choo pia inaweza kuwa ni ujauzito?
Soma Zaidi...Kondo la nyuma kuwa mbele ya mlango wa kizazi
Posti hii inahusu zaidi sababu za kondo la nyuma kuwa mbele ya mlango wa kizazi, kwa kawaida kondo la nyuma huwa nyuma ya mlango wa kizazi ila Kuna wakati kondo la nyuma ujishikisha mbele ya mlango wa kizazi.
Soma Zaidi...Dalili za mimba kutoka.
Post hii inahusu zaidi dalili za mimba kutoka, hizi ni dalili ambazo ujitokeza kwa mimba zote ambazo utaka kutoka kama ifuatavyo.
Soma Zaidi...