Umuhimu wa uzazi wa mpango kwa Mama

Umuhimu wa uzazi wa mpango kwa Mama

Posti hii inahusu zaidi faida za uzazi wa mpango kwa akina Mama, tunajua wazi kubwa kuna faida kubwa za uzazi wa mpango kwa akina Mama pindi watumiapo njia hizi kwa uhakika zaidi.

Umuhimu wa uzazi wa mpango kwa akina Mama.

1.Kwanza kabisa tunapaswa kujua kuwa uzazi wa mpango ni huduma ambayo inatolewa kwa jamii ili kuweza kupata idadi ya watoto wanaohitajika na kuwapatia nafasi kutoka kwa mtoto mmoja kwenda kwa mwingine kwa hiyo zifuatazo ni faida za uzazi wa mpango kwa akina Mama.

 

2.Akina mama wanapata afya nzuri na kupumzika kutoka kwa mtoto mmoja kwenda kwa mwingine.

Ni wazi kabisa mama akiwa na mimba uweza kupata uchovu na masumbuko mbalimbali na kwa wakati mwingine kuna ambao wakati wa mimba wanaweza kuugua na kukosa nguvu mda wote lakini wakijifungua wanakuwa kawaida kwa hiyo na wakati wa kujifungua mama Upata uchungu na kuangaika sana wengine hata kutoa damu nyingi kwa hiyo wakipata mda wa kupumzika kutoka kwa mtoto mmoja kwenda mwingine watakuwa na afya njema kuliko kubeba mimba kila mara na afya udhoofika.

 

3.Uzazi wa mpango uzuia vifo vya akina Mama ambavyo utokea wakati wa kujifungua.

Ni kweli Mama akina mama wengi wanaweza kuingia kwenye hatari ya kufariki  wakati wa kujifungua kwa hiyo kutokana na kuwepo kwa uzazi wa mpango kumefanya kupunguza vifo vya akina Mama kwa sababu ya kujifungua kwa mda kutoka kwa mtoto mmoja kwenda kwa mwingine kuliko kujifungua karibu kila mwaka na viungo vya mwili vinakuwa bado na hali hiyo usababisha kuvuja damu nyingi au kupasuka wakati wa kujifungua na Mama anaweza kupoteza maisha.

 

4.Uzazi wa mpango umesaidia akina mama ushiriki kwenye kazi mbalimbali za kiuchumi kwa sababu Mama anakuwa na nguvu za kutosha kuweza kuleta maendeleo kuliko kukaa katika kulea watoto ambao wamefuata na kama mapacha kwa hiyo kutokana na kuwepo kwa uzazi wa mpango akina Mama wengi wameweza kushiriki kazi mbalimbali za kiuchumi.

 

5.Uzazi wa mpango umefanya akina mama kubwa na idadi ya watoto wanaowapenda na kuwatunza na wameweza kuwa na nafasi kutoka kwa mtoto mmoja kwenda mwingine na pia watoto wenyewe wanaweza kuleana na kusaidiana kwa sababu ya kuwepo kwa nafasi kubwa kutoka kwa mtoto mmoja kwenda mwingine.

 

6.Kwa hiyo tunaona wazi umuhimu wa uzazi wa mpango kwa akina Mama kwa hiyo kama jamii tunapaswa kuwahimiza akina mama kushiriki kwenye uzazi wa mpango ili kuweza kupata idadi ya watoto wanaowahitaji na kuepuka kutumia mda mwingi kulea watoto wanaofuatana na kufanya kushuka kwa uchumi.

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu Rajabu
Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Uzazi Main: Post File: Download PDF Views: 1949

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Dua za Mitume na Manabii     👉5 Simulizi za Hadithi Audio     👉6 Bongolite - Game zone - Play free game    

Post zinazofanana:

NAMNA YA KUBORESHA MBEGU ZA KIUME, NA VYAKULA VYA KUBORESHA NGUVU ZA KIUME

Njoo ujifunze vyakula vya kuboresha mbegu za kiume na nguvu za kiume.

Soma Zaidi...
Fahamu kuhusu fangasi za ukeni

Posti hii inahusu zaidi fangasi za ukeni, hili ni tatizo kubwa ambalo linawakumba watoto, akina dada na wanawake kwa hiyo na vizuri kujua Dalili zake na kuweza kuchukua hatua mapema.

Soma Zaidi...
Madhara ya kiafya ya kupiga punyeto

Post hii inakwenda kukutania madhara ya kuoiga punyeto kwa afya yako.

Soma Zaidi...
Maandalizi ya mama mjamzito kwa ajili ya kujifungulia.

Postii inafundisha maandalizi ya mama kwa ajili ya kujifungulia hii Ni muhimu Sana kwa wale ambao hawajawahi kujingua Ni mara yao ya kwanza wanatakiwa kujua na kuelewa vifaa na mahitaji kujifungulia na kwa wale wanaohudhuria clinic huwa wanafundisha.

Soma Zaidi...