image

Dalili za UTI

Somo hili linakwenda kukuletea dalili za UTI

Dalili za UTI

1.Kukojoa mara kwa mara

2.Kuhisi kuunguwa ama umoto wakati wa kukojoa

3.Kutoa mikojo kwa uchache

4.Mkojo kuwa mchafu, kama mawingu ama mwekundu uliopauka

5.Harufu kali ya mkojo

6.Maumivu ya kwenye njonga kwa wanawake

7.Maumivu ya mkundu na puru kwa wanaume.

 

Dalili za UTI zinaweza pia kuwa tofauti na hizo hapo juu. Dalili hizi hutofautiana kwa kulingana na aina ya UTI. Kama unataka kuzijuwa dalili zaidi za UTI endelea kusoma makala hii mpaka mwisho.

 

Aina za UTI na dalili zake.

Ugonjwa wa UTI umegawanyika katika makundi mbalimbali. Makundi hayo ni kama:-

1.UTI ya kwenye figo (acute pyelonephritis). UTI hii huathiri figo, na kusababisha dalili kama:-

1.Maumivu ya mgongo kwa juu

2.Homa kali

3.Kuhisi baridi na kutetemeka

4.Kichefuchefu

5.Kutapika.

 

2.UTI ya kwenye kibofu (cystitis). hii ni aina ya UTI ambayo huathiri kibofu cha mkojo. Dalili zake ni:-

1.Maumivu ya nyonga

2.Maumivu ya tumbo kwa chini ya kitovu ama mvurugiko wa tumbo kwa chini

3.Kukojoa mara kwa mara huku ukiwa na maumivu.

4.Kukojoa damu, ama mkojo wenye rangi nyekundu ya kupauka.

 

3.UTI ya kwenye mrija wa mkojo (urethritis). mrija wa mkojo kitaalamu unaitwa urethra. Huu ndio mrija unaotoa mkojo kutoka kwenye kibofu na kuuleta nje. Dalili za UTI hii ni kuhisi kuunguwa wakati wa kukojoa.





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 2087


Sponsored links
๐Ÿ‘‰1 kitabu cha Simulizi     ๐Ÿ‘‰2 Kitabu cha Afya     ๐Ÿ‘‰3 Kitau cha Fiqh     ๐Ÿ‘‰4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

Je na kwa upande wa mwanaume kuumwa upande wa kushoto wa tumbo kuna shida gani?
Maumivu ya tumbo upande wa kushoti, kwa mwanamke huwenda ikawa ni ujauzito ama shida nyingine za kiafya kama tumbo kujaa gesi, kukosa choo na kadhalika. Sasa vipi kwa wanaume ni ipi hasa sababuรขยโ€ Soma Zaidi...

Minyoo na athari zao kiafya
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu minyoo na athari zao kiafya Soma Zaidi...

Yajue mashambulizi ya bacteria kwenye Ngozi (cellulitis)
Mashambulizi ya bacteria kwenye Ngozi hujitokeza sehemu yenye jeraha pia huonyesha wekundu wenye upele,Uvimbe na malengelenge. Soma Zaidi...

Maumivu ya tumbo kitomvuni, sababu zake na dalili zake
Hapa utajifunza sababu za kuwepo na maumovu ya tumbe kitomvuni. Soma Zaidi...

Tatizo la damu kutokufikia tishu baada ya kutokea jeraha kwenye tishu (gangrene)
Posti hii inazungumzia kuhusiana na tatizo la damu kutokufikia tishu baada ya kutokea jeraha kwenye tishu ambao hujulikana Kama gangrene inahusu kifo cha tishu za mwili kutokana na ukosefu wa mtiririko wa damu au maambukizi ya bakteria. Ugonjwa wa gangre Soma Zaidi...

FAIDA ZA KIAFYA ZA MINYOO: kupunguza aleji, kuchochea utungaji wa mimba, kupona kwa vidonda vya ndani
FAIDA ZA KIAFYA ZA MINYOO Wakati mwingine kuwa na aina flani ya minyoo kunaweza kuwa na faida katika afya. Soma Zaidi...

Swali langu ni hivi ,napata maumivu kwa mbali kwenye njia za mkojo pia napoteza ham na uwezo wa kushiriki tendo la ndoa kadiri siku zinavoenda je,hizi ni dalili za tezi dume?
Hivi umeshawahikujiuliza kuhusu tezi dume. Wacha nikujuze kitu kimoja, ni kuwa tezi dume huwapata watu kuanziamiaka 40 na kuendelea. Na ifahamike kuwa tezi dume sio busha ama ngiri maji. Pia itambulikekuwa rozi dumehutibika. Soma Zaidi...

Dalili za UKIMWI huonekana baada ya muda gani
Hapa utajifunza muda mabao dalili za VVU na UKIMWI huonekana, na kwa muda gani mgonjwa ataishi na UKIMWI bila ya kutumia ARV Soma Zaidi...

Fahamu matatizo ya ini kuwa na kovu
kovu (Fibrosis) ya ini inayosababishwa na aina nyingi za magonjwa na hali ya ini, kama vile Homa ya Ini na unywaji pombe kupita kiasi. Ini hufanya kazi kadhaa muhimu, ikiwa ni pamoja na kuondoa vitu vyenye madhara katika mwili wako, kusafisha damu yako Soma Zaidi...

Madhara ya kutotibu uvimbe kwenye kibofu Cha mkojo
Post hii inahusu zaidi madhara ya kutotibu ugonjwa wa uvimbe kwenye kibofu Cha mkojo,ni madhara yanayotokea kwenye mfumo mzima wa kupitisha mkojo na via vya uzazi kama ifuayavyo. Soma Zaidi...

Sababu zinazopelekea tumbo kujaa gesi
Kiufipi posti hii inaelezea kuhusiana na dalili na sababu zinazopelekea tumbo kujaa gesi Soma Zaidi...

Dalili na ishara za shambulio la moyo
Posti hii inazungumzia kuhusiana na Dalili na ishara za shambulio la moyo. Shambulio la moyo huzuia damu yenye oksijeni kufika kwenye moyo hivyo hupelekea tishu kufa. Na Ugonjwa huu mtu akicheleweshewa matibabu huweza kupata mshtuko wa moyo mpaka kifo. Soma Zaidi...